Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hivi katika hili sakata kuna mahala zitto kwabwe kaccoment hata mara moja?
 
Narudia Tena.

Magufuli Asinge Ua Upinzani, 2025 ilikuwa ni wakati sahihi wa Upinzani Kuchukua Nchi.

Bado hawajachelewa wajipange… Katika Historia Ya CCM , Basi CCM hii ndio CCM yenye Mpasuko Mkubwaaaa kuliko ile ya 2025. Yaani Yanayotokea CCM na Yatakayo Tokea Hadi 2025 ni Makubwa Kuliko Haya Ya Ndugai, Subiri Baraza Livunjwe na Mengine Mengi.

CCM hii Iko Vipande Vipande mpaka Mama Atakapo Acha Unzanzibar
 
Nyie endeleeni kushangilia tu wakati Mwenzenu tayari Maisha alishayapati siku nyingi tu. Na huenda ana nyumba Kaperinaumu
 
Acha apotelee mbali kwa uonevu mkubwa aliowah fanya ktk bunge ...malipo Ni hapa hapa dunian
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni

Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama

#JamiiForums

Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.

Hapo awali akizungumza Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada

“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.

Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni.

RAIS SAMIA ASHANGAZWA NA SPIKA NDUGAI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.

Akizungumza Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia alionyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.

“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.

"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", amesema Rais Samia.

Soma:
Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza

“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge
View attachment 2070821
Kwanini Spika awasilishe barua ya kujiuzuru kwa katibu mkuu CCM. Je katibu mkuu ndio kiongozi wa juu wa Bunge?
 
Kwanini Spika awasilishe barua ya kujiuzuru kwa katibu mkuu CCM. Je katibu mkuu ndio kiongozi wa juu wa Bunge?
Kwa sababu ni spika kupitia tiketi ya CCM! NI CCM ndio walimhidhinisha kugombea kiti!
 
TUMEKUELEWA NDUGAI

Kusema ukweli aliyekuwa spika wa Bunge la JMT Job Yustino Ndugai ameonesha uwezo mkubwa wa uwajibikaji (accountability). Hii hali kwa Afrika ni jambo gumu sana na hufanyika kwa nadra sana. Ameonesha njia ya kidumisha misingi ya demokrasia, hivyo ni muda wa viongozi wengine kuiga mfano wake.
 
waige wale kwako au polisi, acha hizo!
 
Daah bora katoka tutasahau mambo ya kuitwa kwenye kamati za maadili na kuzarau taasisi zingine..
 
TUMEKUELEWA NDUGAI

Kusema ukweli aliyekuwa spika wa Bunge la JMT Job Yustino Ndugai ameonesha uwezo mkubwa wa uwajibikaji (accountability). Hii hali kwa Afrika ni jambo gumu sana na hufanyika kwa nadra sana. Ameonesha njia ya kidumisha misingi ya demokrasia, hivyo ni muda wa viongozi wengine kuiga mfano wake.
Usinpake mafuta Kwa mgongo was chupa kwenye democrasia no mfano was kuepikwa, kwenye kuijiwajibisha angalau Kwa Sasa nampa30 %
 
TUMEKUELEWA NDUGAI

Kusema ukweli aliyekuwa spika wa Bunge la JMT Job Yustino Ndugai ameonesha uwezo mkubwa wa uwajibikaji (accountability). Hii hali kwa Afrika ni jambo gumu sana na hufanyika kwa nadra sana. Ameonesha njia ya kidumisha misingi ya demokrasia, hivyo ni muda wa viongozi wengine kuiga mfano wake.
 
Job umetuangusha sana usingejiuzulu ungekaa bungeni usile wala kunywa na kulia tuu kuwa ulimi hauna mfupa na una familia ya kulisha!
 
Back
Top Bottom