Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sukuma gang mnapigwa matukio mfululizo. Unajua bado nini?Msiba upi?
Unafikiiri ccm itaninyonga mimi pekeangu?
Najua unajua na hauhitaji kiambiwa, ila ujue tu, Mungu ni mwaminifu na hutenda Kwa wakati.Unachofurahia ni nini sasa?
Kwanini Spika awasilishe barua ya kujiuzuru kwa katibu mkuu CCM. Je katibu mkuu ndio kiongozi wa juu wa Bunge?Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni
Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama
#JamiiForums
Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.
Hapo awali akizungumza Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada
“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.
Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni.
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi...www.jamiiforums.com
RAIS SAMIA ASHANGAZWA NA SPIKA NDUGAI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.
Akizungumza Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia alionyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.
“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.
"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", amesema Rais Samia.
Soma:
Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"
Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.
“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza
“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge
View attachment 2070821
Kwa sababu ni spika kupitia tiketi ya CCM! NI CCM ndio walimhidhinisha kugombea kiti!Kwanini Spika awasilishe barua ya kujiuzuru kwa katibu mkuu CCM. Je katibu mkuu ndio kiongozi wa juu wa Bunge?
waige wale kwako au polisi, acha hizo!TUMEKUELEWA NDUGAI
Kusema ukweli aliyekuwa spika wa Bunge la JMT Job Yustino Ndugai ameonesha uwezo mkubwa wa uwajibikaji (accountability). Hii hali kwa Afrika ni jambo gumu sana na hufanyika kwa nadra sana. Ameonesha njia ya kidumisha misingi ya demokrasia, hivyo ni muda wa viongozi wengine kuiga mfano wake.
Usinpake mafuta Kwa mgongo was chupa kwenye democrasia no mfano was kuepikwa, kwenye kuijiwajibisha angalau Kwa Sasa nampa30 %TUMEKUELEWA NDUGAI
Kusema ukweli aliyekuwa spika wa Bunge la JMT Job Yustino Ndugai ameonesha uwezo mkubwa wa uwajibikaji (accountability). Hii hali kwa Afrika ni jambo gumu sana na hufanyika kwa nadra sana. Ameonesha njia ya kidumisha misingi ya demokrasia, hivyo ni muda wa viongozi wengine kuiga mfano wake.
Mhimili wa bunge haupo,tangia chini ya Nyerere mpaka leo. Labda siku ikitokea speaker anatoka chama tofauti na chama tawala.Kitendo hiki kimelidhoofisha sana bunge! Ni kama mhimili wa bunge haupo tena
At least kaonesha uthubutuUsinpake mafuta Kwa mgongo was chupa kwenye democrasia no mfano was kuepikwa, kwenye kuijiwajibisha angalau Kwa Sasa nampa30 %
Kaonesha njiawaige wale kwako au polisi, acha hizo!