Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
Unafurahia ujinga?Najua unajua na hauhitaji kiambiwa, ila ujue tu, Mungu ni mwaminifu na hutenda Kwa wakati.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unafurahia ujinga?Najua unajua na hauhitaji kiambiwa, ila ujue tu, Mungu ni mwaminifu na hutenda Kwa wakati.
Hivi mdingi atakuwa anaingia bungeni na kuwa mzee wa ndiooooooooo au ndio anaenda kwa shemeji yake kapernaumu a.k.a kongwa?Kimeumanaaaaaaa,,sasa wale covid 19 ,,wajiandae...maana baba yao ndo huyo anaelekea galilaya wilaya ya kapernaumu .
Sasa aliomba radhi ya nini yule mgogo?Kosa la ndugai liko wapi kwa mjibu wa sheria? Je, ndugai kavunja katiba katika kutoa maoni yake...!
Kosa la ndugai, linapaswa liwe la kichama na si kama anavyosakamwa aachie ngazi!
Kwa katiba ipi na sheria ipi inayodai sipika akitoa maoni yake kuhusu jambo la kiserikali atawajibika/wajibishwa?
Chama ndicho chaweza kumwajibisha ikiwa ziko taratibu za aina hiyo ila si kwa kumvua madaraka ya usipika!
Ngoja litokee hili, Tutajiona mapanzi mbele ya dunia kwa jinsi itavyoonyesha katiba yetu isivyiheshimiwa na kujitoshereza!
Sasa nimeelewa kwamba, Tz katiba yetu ni mbovu kuliko chochote!
Kwa nchi zenye watu wenye kupima ukweli wa jambo kupitia katiba walizonazo, Kusingeeleweka ikiwa sipika anashinikizwa kuachia ngazi kwa jambo ambalo halipo kikatiba
Mh Sipika ni mkuu wa mhimili unaojitegemea, lkn pia ni RAIA wa Tz mwenye Uhuru wa kutoa maoni yake katika jambo lolote lile huku akizingatia sheria za nchi
Niko na Ndugai na hana kosa kisheria na kikatiba
Sukuma gang ni imagination tu!Sukuma gang mnapigwa matukio mfululizo. Unajua bado nini?
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni
Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama
#JamiiForums
Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.
Hapo awali akizungumza Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada
“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.
Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni.
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi...www.jamiiforums.com
RAIS SAMIA ASHANGAZWA NA SPIKA NDUGAI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.
Akizungumza Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia alionyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.
“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.
"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", amesema Rais Samia.
Soma:
Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"
Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.
“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza
“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge
View attachment 2070821
Hawana uwezo huo!..Narudia Tena.
Magufuli Asinge Ua Upinzani, 2025 ilikuwa ni wakati sahihi wa Upinzani Kuchukua Nchi.
Bado hawajachelewa wajipange… Katika Historia Ya CCM , Basi CCM hii ndio CCM yenye Mpasuko Mkubwaaaa kuliko ile ya 2025. Yaani Yanayotokea CCM na Yatakayo Tokea Hadi 2025 ni Makubwa Kuliko Haya Ya Ndugai, Subiri Baraza Livunjwe na Mengine Mengi.
CCM hii Iko Vipande Vipande mpaka Mama Atakapo Acha Unzanzibar
Ndio matatizo ya kumtegemea SPONSOR, anapokufa ndio utajua kumbe ulikuwa huju!!kwani juzi tu mjumbe mmoja wa ccm alihoji juu ya hao covid 19, kuwa wapo bungeni kutokana na kiburi cha spika.Kwa tabia ya wana ccm lazima watawakali kooni hao covid hadi watolewe bungeni
Hakuwa na uwezo wa kuongoza muhimili mkubwa kiasi hicho.Yaani
Kakubali vipi kurudisha mpira kwa kipa kirahisi hivi yaani kaniangusha sana maneno uyaogope kweli
Zitto anasubiri uteuzi ikulu, na maskini ya Mungu hajui system imemkataa.Hivi katika hili sakata kuna mahala zitto kwabwe kaccoment hata mara moja?
Huyo ni LemaWalio na utabiri wa Lema au wowote kwa Ndugai watupe maana alikuwa mbabe mno ndani ya Bunge.
Kwahiyo hiyo demokrasia hamkuiona kwa Benard Membe?Kwani Ndugai akisema 2025 watz wakitaka mamchague mwingine inakuaje ni uasi?
Si ndio democrasia hiyo?
Safi sana.tusonge mbele.je?Katiba inasemaje?akijiuzulu spika inakuwaje?.tutajua hatujuiHii fake.
Tuondolee hizi bangi zenu.Huyo ni LemaView attachment 2071023
Chizi weweMaskini shotii