hivi ulazima wa spika kutoa taarifa ya mambo ya jana unatoka wapi? kama swala la kukusanya maoni lina umuhimu kiasa cha spika kulitolea taarifa mbona TBC tv ya umma haikurusha live? hawa swala la muhimu ni lile la wananchi kuonesha wanapinga serikali na shughuli za kichama za ccm kama maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama?
Ndg zangu amini nawaambia serikali na bunge wapo kwenye mapambano makali dhidi ya CHADEMA kiasi cha kupata upofu na hivyo kushindwa kuona na kutofautisha ni lipi la CHADEMA na lipi ni la wananchi, bado wanazani wananchi ni wajinga hivyo wanaodai haki wametumwa na CDM.Katika mantiki hii tusitegemee jema lolote kutoka serikalini na bungeni kwani mliotazama bunge nazani mmeona jinsi wabunge wa ccm walivyopiga makofi, mkumbuke tu kwamba sio tu walipiga makofi bali walipiga makofi kabla spika ajamaliza kuongea, hii inaashilia nini? hii inaonesha kuwa wabunge hawa bado hawajakomaa kifikra kiasi cha kuipinga serikali inapoitajika, hivyo bila shaka wataupitisha mswaada ambao binafsi najua watarekebisha kidogo lakini bado utakua na mapungufu mengi tu.
Ndg zangu inasikitisha sana kuona vyombo muhimu vya dola yaani bunge na serikali vinageuka na kuwa vyombo vya kupambana na chama cha siasa(CHADEMA) matokeo yake kujikuta inapambana na wananchi ikizani inapambana na chama, tatizo hapa sio CHADEMA, tatizo ni wananchi wamepoteza imani na serikali, hivyo kupambana na CHADEMA ni kupoteza rasilimali za nchi kama mabomu ya machozi, mafuta n.k ambazo wangeweza kutumia rasilimali hizo kurudisha imani ya wananchi na kumaliza tatizo, kwani wanayofanya sasa ndo yanaongeza tatizo.