Spika Ndugai ahoji shughuli za Serikali kurudi Dar, ataka kujua ni nani anayedhibiti matumizi ya Serikali kwa sasa

Spika Ndugai ahoji shughuli za Serikali kurudi Dar, ataka kujua ni nani anayedhibiti matumizi ya Serikali kwa sasa

Mmeanza kiunana wenyewe kwa wenyewe sasa! Safi sana, hadi akili ziwarudie.
 
Hawezi kuongea straight maana wote wale wale.Wanapopishana maslahi ndipo vimaneno maneno utavisikia ila wakichovya wote kwenye chombo cha mema ya nchi hutasikia neno zaidi yakusifia nakusema kila kitu kiko vizuri.

Hapo umepigila pale pale
Wote ni maslahi tu na upigaji na hakuna mwenye huruma na maskini
 
Mbona amenena vema kabisa au ulitaka alopoke na kutukana, au kwamba ulipendelea bunge lake lote likae lijadili hilo swala akat PM wako nae mule na wote ni Kada moja. Linao wahusu watalichukua ikiwa wataona umuhimu wa kufanya hivyo, vinginevyo basi wanayafanya hayo kwa maslahi yao.

Wanaviziana tu na mmoja akifaidika zaidi lazima kiumane
Siasa na imani ni mbali mbali
Siasa ni ulaghai na hata dini inakaa pembeni na utu ndio sahau
 
JPM alikua anafanya kazi kwenye ofisi zipi
Na ndio maana kama uliwahi kuona kuna picha yuko ofisini watu wakabeza ofisi kama ya mkuu washule. Rais ni taasisi kubwa ina wasaidizi na ofisi ya Rais bado haijakamilika. JPM alikuwa ana residence temp tu na ndio maana hakuwa moja kwa moja pale. Kikwete aliongelea hili kuwa kulikuwa na mawazo ofisi ya Rais ijengwe mjini ila changamoto ya safari haikuwa nzuri kwa salama. Ujenzi wa ofisi unajengwa ili ofisi ya Rais ihamie na wafanyakazi wote.
 
Eti mtu akisema chochote utasikia Mbona hukusema wakati wa JPM!

Kwa hiyo watu wasiseme chochote isipokuwa walivyosema wakati wa JPM?

Watu wakisema wanaambiwa wanamuonea mama eti!

Kwa vipi sasa?

Tena hii kauli ningekuwa mimi ndiye Mama ningewaonya mara moja wale wanajidai kunihurumia kwa kusema Eti naonewa!

Naonewa kivipi?

Yani supreme leader anaonewaje kwa mfano?!

Na wala haina maana kuanza kutumia dola kuwazuru au kwaweka watu kizuizini kuwakomoa la hasha! Bali ni swala la kujitambua na kuonekana kuwa unajitambua hata machoni na kimwenendo!

Hata kina Mboe kinachowagarimu huenda ndio hicho!

Eti Kwanini hawakudai Katiba wakati wa JPM?

Kwa hiyo kama ni hitaji la nyakati ya sasa wasiseme sababu hawakulisema wakati wa JPM?

Inferiority complex ni ya kuepuka kabisa kuanzia kwenye mawazo yetu!

Kuonewa au kutokuonewa ni mind set ya mtu.

Maisha ni mwendelezo kuna mawazo mapya yanaibuka, mitazamo mipya, mabadiliko n.k!
 
Makao ni Dodoma watulie huko ndipo mahali palipochaguliwa sawa Ndugai
 
  • Thanks
Reactions: nao
Serikali hii imejaa matumizi ya hovyo sana. Miradi yao mikubwa ni ujenzi wa vyoo, madarasa na hospital.
Hii nchi ni linii rais naye ataambiwa ukweli?? Naye Dar kilaleo sio mawaziri tuu...
😀 😀 Sterling wa movie hatari, kila siku safari kama miguu imelambwa na mbwa vile.
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai leo wakati wa kuahirisha shughuli za bunge, amewahoji mawaziri ni kwa nini kwa sasa wameamua kufanyia makongamano, warsha na semina nyingi Dar es Salaam na kuacha kufanyia Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi.

Ndugai ametaka kujua ni nani anayecontrol expanditure za serikali kwa sasa kwani kila mawaziri wanapofanya hizo safari za Dar wanalipana posho za kutisha pamoja na wasaidizi wao huku wakiwaacha wananchi masikini wakiwa hoi hoe hae bila huduma muhimu za jamii.

View attachment 1932327
Tangu Ndugai amuone yesu na mkewe Akili kama zimerudi sehemu yake.
 
Mnakosea sana mnapilinganisha awamu ilopita na hii kwa kusema “Eti wakati wa JPM angeyasema hayo”?

Hiyo ni inferiority complex!

Basi muulize pia je wakati wa JK mtu angeyasema hayo?

Watu wenye mawazo kama yako iwapo wakiwa karibu ya Rais mtamfanya aanze kujisikia -inferiority complex kitu ambacho sio kizuri.

Epukeni kabisa hiyo hali ya kujiuliza Eti ingekuwa wakati wa JPM angeyasema hayo? So what?

Madhara ya inferiority complex yanajulikana!

Uongozi si lelemama, unapaswa kuwa na kifua kipana cha kukabiliana na mambo mazito!
Narudia tena acheni kumhujumu Rais Samia. Ndugai analalamika Mawaziri na Rais Samia kuonekana DSM lakni wakati JPM alipohamia Chato tena kwenye hoteli yake na convoy kubwa ya wasaidizi wake hakulalamikia hiyo expenditure wala Dodoma kuwa jeopardized. Wanafiki na wasaga sumu wakubwa.
 
Kwa hiyo watu walokuwa wanaongea wakati wa JPM warudie kusema yale yale wakisema mapya wataambiwa Kwanini hawakusema wakati wa JPM?

Wale ambao hawakusema chochote wakati ule waendelee kukaa kimya maana Kwanini hawakusema wakati wa JPM?

Likija wazo au mtazamo mpya wa kinyakati asiwepo mtu au watu wako-raise issue yoyote maana wataulizwa Kwanini hamkusema wakati wa JPM?

Hivi waTZ tunakwama wapi ndugu zangu?
 
Narudia tena acheni kumhujumu Rais Samia. Ndugai analalamika Mawaziri na Rais Samia kuonekana DSM lakni wakati JPM alipohamia Chato tena kwenye hoteli yake na convoy kubwa ya wasaidizi wake hakulalamikia hiyo expenditure wala Dodoma kuwa jeopardized. Wanafiki na wasaga sumu wakubwa.


Hilo la hujuma ni tafsiri yako tu!
Kikubwa ni kujiamini tu hainahaja haja ya kuwa na mtazamo hasi katika kuyachukulia mambo kimtazamo!

Msimfanye Rais kuwa na inferiority complex spirit.

Inferiority complex sio kitu kizuri.

She is capable kujisimamia mwenyewe kuliko kumjaza mitazamo hasi !
 
Kuna jamaa yangu mmoja yuko hapa Dar wiki hii ya pili sasa, kituo chake na familia yake ni Dom... Chakula malazi na kinywaji vyote ni hotelini.... Najiuliza hizi gharama zina uhalali wowote ?
 
Kaa chini utafakari ulichoandika


Haya mambo ya kuonesha kwa nini kuhamishia Makao Makuu Dodoma ni makosa niliyasema tangu mpendwa Hayati JPM akiwa hai. Na alipona hoja zinamshinda akapiga mkwara wakati anazindua ujenzi wa fulaiova ya Hayati Kijazi Ubungo akisema, 'kama jambo haulipendi si unyamaze.'

Ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote. Kufukia kodi za Watanzania Kwa kigezo cha Makao Makuu Dodoma ni ukengemfu. Ikiamliwa DSM iendelee kubakia kuwa Makao Makuu ya nchi hii leo. Na kukaingiwa gharama za maboresho, ukajengwa mji mpya wa kiserikali DSM na Ikulu mpya bado gharama hizi hazitafikia nusu ya gharama za kuifanya Dodoma kuwa na hadhi ya Makao Makuu.

Faida yake ni kubwa zaidi, DSM itaendelea kutoa kodi kubwa zaidi. Majengo mengi ya Mifuko ya kijamii yaliyo DSM na ya wadau wengine yatapata wapangaji, yange ongeza ajira, serikali itakusanya kodi kuliko sasa ambapo yako idol tu na ni hasara kwa serikali na walio fanya huu uwekezaji.
 
Narudia tena acheni kumhujumu Rais Samia. Ndugai analalamika Mawaziri na Rais Samia kuonekana DSM lakni wakati JPM alipohamia Chato tena kwenye hoteli yake na convoy kubwa ya wasaidizi wake hakulalamikia hiyo expenditure wala Dodoma kuwa jeopardized. Wanafiki na wasaga sumu wakubwa.
Watanzania watawaonyesha kazi ,wezi wa mali za uma nyinyi
 
Back
Top Bottom