Spika Ndugai asema Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mahakama pekee wanaweza kumuambia kuwaondoa Bungeni Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Kosa kubwa la ndugai ni kujifanya kichwa maji. Kikatiba akipewa taarifa rasmi na katibu mkuu wa CHADEMA kwamba wale wabunge 19 Sio Wanachadema, spika anapaswa kuwaondoa bungeni. Uhalali wa kuwafukuza chamani yeye haumuhusu
 
Naona Spika anaendelea kumjibu Spika wa zamani kiaina, wafuatiliaji wa mambo wanaelewa
 
Kosa kubwa la ndugai ni kujifanya kichwa maji.Kikatiba akipewa taarifa rasmi na katibu mkuu wa chadema kwamba wale wabunge 19 Sio wanachadema, spika anapaswa kuwaondoa bungeni.Uhalali wa kuwafukuza chamani yeye haumuhusu
Kipengele kipi cha katiba? Sidhani kama uko sahihi
 
Huyu spika anachoongea ni tofauti kabisa, kwanini asiwe mkweli japo mara moja, halafu chadema haijamtaka spika kuwafukuza wabung ile imewafukuza wanachama wake kwa kukiuka taratibu na katiba ta chama, hayo ya ubunge haiwahusu chadema

Kweli ccm ipo juu ya sheria

Ama kweli awamu hii inatia fora
 
Kipengele kipi cha katiba? Sidhani kama uko sahihi
Huo ndo ukweli wenyewe, ukitaka kubisha we bishana tu, ndo maana kina Sofia Simba na wale wabunge wa cuf walivyotimuliwa uwanachama waliondoka bungeni Mara moja. Ndugai aweza kuwa na chuki na mbowe, lakini Hilo ni swala la katiba yetu.Kumbuka hatuna wagombea binafsi
 
Kwa mujibu wa Katiba na sheria ipi wakati Kamati Kuu ya Chadema imesema haikukaa kuteua majina ya hao COVID19? Na saini ya Mnyika kwenye fomu husika iligushiwa? Usiwe unaandika ujinga ujinga tu bila kutafakari kwa kina kuhusu issue yote husika.
Spika Ndugai amesema aliwaapisha wabunge 19 wa CHADEMA baada ya kupokea majina kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na pia kuyasoma majina hayo katika Gazeti la Serikali...
 
Ni baada ya NEC kumtaarifu Spika. Sema mambo yalienda fasta sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…