Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

Wasipokuelewa hapa hawatakuelewa tena.
 
Inaçhekesha na kukera sana! Yaani mtu asiyelipa kodi ndo anakuja na wazo la kodi ya uzalendo!! Waxiolopa kodi wote siyo wazalendo wala tusidanganyane!! Yesu alilipa kodi, kwa hiyo hakuna sababu ya mtu yeyote kutokulipa kodi! Awe padri, mchungaji, askofu, mufti, Rais, askofu, mbunge, waziri nk lazima alipe kodi.0
 
Wabunge wenye kipato cha uhakika kila mmoja akatwe sh 2,000,000/= kwa mwezi,tutapata pesa nzuri tu
 
Uwezo wa kufikiri ndiyo umefikia peak, hawezi kufikiri zaidi ya hicho alichosema
 
Wenyewe wanakuambia wapiga kura wetu. Kuna wamachinga anaingiza zaidi ya milioni 2 ila halipi kodi.Nchi Ina walipaji kodi wachache Sana kwa ajili ya siasa zetu za kipuuzi.
 
Hivi Ndugai anaisemea serikali au ana wasemea Wagogo wenzake wa Kongwa?
Huyu jamaa ni zero kabisa.
Wabunge wana takiwa kuwasemea wananchi na sio kuisemea serikali.
Sasa naamini Ndugai ana faili Mirembe.
 
kwanza acheni kununua magari ya kifahari, punguzeni posha ya Tshs 300,000.00 kwa siku kwa wabunge, mna wachumi kwa nini kabla ya kupitisha hizo tozo msiwaulize wananchi mnauliza sasa? huo ni ujinga mkubwa na ulevi wa madaraka
Kateni posho za vikao vya Bunge(Sitting allowances) na mishahara ya wabunge,wawalazimishe kampuni za simu wapeleke serikalini mabaki ya dakika,SMS na bando ambazo hazijatumika na wateja baada ya kujirusha na viongozi wote wa serikali walipe kodi kuanzia Rais mwenyewe.
Serikali iache kutumia magari ya kifahari na waote wapewe Noah/Prado,SUZUKI/MARUTI au RAV 4 ili kuokoa fedha.
Pia tuondoe ma-RC&DC's maana hawana kazi yoyote ya kuinua uchumi.
Mawazo mbadala ya kuinua kipato cha serikali ni mengi ila viongozi wanafikiri wao tu ndiyo wenye mawazo mazuri.
Ndugai yupo tayari kupewa ushauri?Kulikuwa na ulazima wa kuweka tozo kubwa kiasi hicho?Nani kawaambia kuwa turning point I we 2025?Sisi wengine tunadhani hizo tozo ni matokeo ya hofu yao kuwa miradi hiyo isipokamilika 2025 CCM inaenda kukosa kura?
 
You nail it....wajinga hawataelewa🙌🙌👏👏
 
Utakuta mwalimu mwenye mshahara wa laki 3 anakatwa Kodi ila machinga hawalipi
Wenyewe wanakuambia wapiga kura wetu. Kuna wamachinga anaingiza zaidi ya milioni 2 ila halipi kodi.Nchi Ina walipaji kodi wachache Sana kwa ajili ya siasa zetu za kipuuzi.
 
Uzalendo siyo kuvaa skafu za kijani na kuandika majina yako kwenye mawe nchi nzima. Tuonyeshe huyo first clasa yako unaimudu vipi kusaidia vyanzo vya mapato.
Vijana mnawaambia wajiajiri na watumie elimu zao kujenga nchi wkt wewe na mfirst class wako umezusha taaruki kubwa.
 
Huyu kibushuti apuuzwe tu ana faili Mirembe
 
Sasa hayo mawazo mbadala si yalitakiwa yachagizwe bungeni na wabunge wenye akili?
Ninyi wa sisiem hapo ndio mwisho wenu wa kufikiri.
Wale wenye uwezo wa kufikiri mlikula njama za kuwaengua kwa hila halafu sasa mnaomba mawazo yao.
Achieni bunge upinzani ulichukue halafu uone maendeleo ya watu bila kuwapora fedha zao kinguvu kwa kivuli cha mshikamano.
 
Auwezi kutengeneza lindude lisilo na maana halafu utuambie kama atulitaki utuletee mbadala, hilo dude liuwe tu alina mbadala, linavunja sheria uwezi ingia mifukoni mwa watu uchukue fedha zao bila kujuwa wamepata wapi!
 
Kwa hiyo kumbe lile agizo la Rais hiyo tozo iangaliwe upya ilikuwa ni usanii? ndio maana mpaka leo kimya.
Hivi tozo ni nini? Naona kama unyang'anyi tu, ujui fedha nimepata wapi we unachukuwa tu!
 
Kama yeye na vyanzo vyote vya Habari na kuwepo Bungeni kwa muda mrefu hajui, basi tutakuwa na tatizo kubwa la kiuongozi.
Na anakuwa sio msaidizi mzuri kwa Raisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…