Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

Tutafuta odd 5 kila siku halafu tuwe tunabetia makampuni ya kibeberu tu 1XBET, BET360 etc hapo tutatoboa.
 
Wabunge wapewe salary ya M 3,na posho iwe laki

Fungu lingine lote liende kwa maendeleo
 
Huyo atakuwa hajitambui kidogo!!, sasa atuambie baada ya 2025, kodi hiyo itasitishwa??!!---- yaani Bunge litapelekewa Muswada wa kufuta hiyo kodi???
Hiyo haitafutwa kamwe, hapo mnapigwa geresha muizoee then watawajia na hadithi nyingine, wako hatua kadhaa mbele yenu.
Hiyo wameshamaliza na sasa wanapiga hesabu za mbele kupata vyanzo vingine, mtafinywa sana tu.
 
Wazo jemaa KABISA kuchangia nchi yangu na maendeleo yake
wakati muafaka Kama wananchi tusikomae tu iondoelewr

TUTOE ushauri nn kifanyike seerikali iendelee kupata pesa za KUFANYA maendeleo ya NCHI yetu

nimeona dini zilizoea Kupitisha.mizigo bila Kodi leohii zinalipa...

Hili la wabunge kulipa.kodi.nalo n wazo jemaa pia na ikiwezekana kuwe na punguzo ktk posho wanazopata KUSAIDIA kuendeleza maendeleo ya NCHI yetu

kingine serkl ingekaa wakubaliane kiasi KIDOGo kaama n 200 ama 500 kilamhamala si mbaya huku kampuni zikiendelea kulipa kodizao kama kawaida....mwananchi atajisikia amechangia nchi yake..

kuwe na costant amount ushauri 200-500 KIla.mhamala SI.mbaya isiangalie kiasi anachotuma mtu...

nawatakia mjadala mwema nikisubiri wabunge nao wapewe hiihoja kujadili MBADALA wa hii tozo

kulipa mtalipa nchi iendee tuombee majadiliano mema

Mungu ibariki Tanzania

#VAAABARAKOA
#NAWAMIKONO
#COVID
#INAUA

Makato Makubwa sana ,imagine ukitaka kumtumia mtu na ya kutolea unatwangwa kote kote ,ukituma unakatwa tozo na ile ya kutolea na yenyewe ina tozo ,ni hatari sana ,tozo muhimu ila walizoweka ni kubwa sana , imagine kwa sasa ukitaka kumtumia mtu Tsh 70,000 basi inabidi uwe na 4000 Tsh ya ziada ambayo awali haikuwepo.(2000 Tozo ya kutuma + 2000 Tozo ya kutolea) maana ukimtumia mtu elfu 70 lazima uweke na ya kutolea ili atoe 70k kama ilivyo.
 
Ura
Spika Ndugai amesema wabunge wameshapitisha tozo ya kizalendo kwenye miamala ya simu na sasa ni sheria hivyo asiyeitaka atupe njia mbadala ya kutufikisha 2025

Roho wa Bwana akamshukia mtumishi wake Jerry Slaa mbunge wa Ukonga naye akajibu; Wabunge tuanze kulipa kodi.

Labda kama Spika ana swali lingine....lakini sidhani.

Ijumaa kareem?

---
Baada ya mijadala mingi kuhusiana na tozo ya miamala ya simu hususani kwenye mitandao ya kijamii ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameibuka na kudai kuwa tozo hizo ni halali na kwamba fedha hizo zitachagiza masuala ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii kama vile shule,hospitali na maji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu huku akipigilia msumari kwenye tozo hizo kwa kudai kuwa Bunge ndio limepitisha na kwamba wanaopinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania iwe Taifa tofauti katika suala la Maendeleo.

Akizungumza mapema leo Julai 23,2021,katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai amesema "Sisi kama Bunge tulikaa kwa pamoja na kujadiliana kisha tukaamua kuwa na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi,"amesema na kuongeza;

"Tumepitisha na tukatunga sheria , tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofaut,CCM hoyee,nimemaliza,"amesema Spika huyo.

Chanzo: Malunde
Weka mawasiliano ya mtu wa kkupewa hizo taarifa.
 
Tuingie betting tu, mheshimiwa Spika...ukitupa bilioni 10 vijana wako wa kazi weekend moja unawezashangaa tunakuletea triliions🤣🤸🐒
 
Wabunge wapewe salary ya M 3,na posho iwe laki

Fungu lingine lote liende kwa maendeleo
Laki ya nini,madakitari na walimu wanalipwa hiyo posho?
Wabunge walipwe mshahara tu na isizidi 5ml kwa mwezi na wakatwe kodi.italeta kuwapata wabunge wazalendo hata rushwa hutasikia.Tuna wasomi wengi tu hata 2ml watakubali kulipwa.
Nchi hii tunachezeana sana Tsh 12,000,000 kwa kazi gani?
 
Spika Ndugai amesema wabunge wameshapitisha tozo ya kizalendo kwenye miamala ya simu na sasa ni sheria hivyo asiyeitaka atupe njia mbadala ya kutufikisha 2025

Roho wa Bwana akamshukia mtumishi wake Jerry Slaa mbunge wa Ukonga naye akajibu; Wabunge tuanze kulipa kodi.

Labda kama Spika ana swali lingine....lakini sidhani.

Ijumaa kareem?

---
Baada ya mijadala mingi kuhusiana na tozo ya miamala ya simu hususani kwenye mitandao ya kijamii ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameibuka na kudai kuwa tozo hizo ni halali na kwamba fedha hizo zitachagiza masuala ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii kama vile shule,hospitali na maji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu huku akipigilia msumari kwenye tozo hizo kwa kudai kuwa Bunge ndio limepitisha na kwamba wanaopinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania iwe Taifa tofauti katika suala la Maendeleo.

Akizungumza mapema leo Julai 23,2021,katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai amesema "Sisi kama Bunge tulikaa kwa pamoja na kujadiliana kisha tukaamua kuwa na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi,"amesema na kuongeza;

"Tumepitisha na tukatunga sheria , tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofaut,CCM hoyee,nimemaliza,"amesema Spika huyo.

Chanzo: Malunde
Huyu mzee ni mpumbavu sana.
 
Wale jamaa awajahi kuwa na hurumaa mkuu.n kusaidiana kuomba serkl wapunguzee hi kitu na iwe kiasi fulan cost Kila mhamala sio kwakutegemea unachotuma hataree...naona msg za tugopesa eendelea kutumia kama vile awaoni sijawagusa Tena Toka mamboyao
 
Bunge lifutwe maana Bunge la ndugai limetuthibitishia kuwa Tanzania haifadiki na wananchi hawafaidiki na uwepo wa Bunge hilo zaidi ya kurudia kilichosemwa na serikali na kupiga makofi!
 
Mimi naunga mkono hoja, tulipe kodi, maendeleo yana gharama yake, moja wapo ni kulipa kodi.

Alafu kodi ya miamala ni wakati unatumia miamala hiyo tu, usipotaka usitumie, tumieni ATM au Bank transfer. Tulipe kodi kwa maendeleo ya wote. Na tuna haki ya kuuliza matumizi ya kodi zetu. Tulipe kodi plz
 
Hii inanikumbusha stori ya Binti yangu wa chekechea
"Yaani namlipia ada na kilakitu pamoja na usafiri kilakitu ili apate elimu asome aweze kutatua changamoto za kielimu, lakin kila akirudi nyumbani ananipa Homework walizopewa shuleni etii nimsaidie kufanya" Sasa najiuliza nalipa ada ili iweje ikiwa homework nafanya mimi?
Wabunge tunawalìpia kilakitu ili Waje na Mawazo mbadala ya kodi lakini still wanatuambia sisi tuwasaidie hii homework. Just imagine wabunge zaidi ya 350 wa CCM wameshindwa kubuni njia nzuri zaidi wameishia kukubali kodi hii tuilipe?
 
Wabunge walipe Kodi kwenye mapato yao yote,utalii utangazwe zaidi na vivutio viwepo,madini yauzwe kwenye masoko ya ndani hata kama muuzaji hana leseni mradi anayo auze tu,tuna gesi za aina mbali mbali ziuzwe bila ujanjaunjanja kama awamu ya NNE ilivyouza gesi ya mtwara.
 
Mkuu afadhali umekemea huu upumbavu. Umejaa sana humu jukwaani haswa baada ya kifo cha JPM. Wanavyoombea watu wafe utadhani wao kwa sasa wanaishi mbinguni na duniani kwa wakati mmoja.

Ni aina fulani ya mawazo ambayo ni ya kipuuzi sana.

..Magufuli aliumiza watu na ndio maana wako baadhi ya wachangiaji hapa JF wamevunja mwiko wa Watz na kushangilia kifo chake.

..Natumaini tunachokishuhudia hapa kitakuwa funzo kwa viongozi wa sasa na wajao.

..Uongozi ni pamoja na kuheshimu UTU wa wale unawaongoza. Kiongozi hapaswi kuwa na CHUKI au VISASI haswa anapokuwa na madaraka makubwa ya kidola kama Raisi wa Tanzania.

..Sifurahishwi na hawa wanaochekelea kifo cha Magufuli. Natamani wakome muenendo huo. Lakini pia naelewa kwanini wamefikia hatua hiyo.
 
Back
Top Bottom