Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

Mkuu afadhali umekemea huu upumbavu. Umejaa sana humu jukwaani haswa baada ya kifo cha JPM. Wanavyoombea watu wafe utadhani wao kwa sasa wanaishi mbinguni na duniani kwa wakati mmoja.

Ni aina fulani ya mawazo ambayo ni ya kipuuzi sana.
Ni hivi, wafe tu wapuuzi kama dogo jobu amfuate dikteta hayawani ila tozo liko pale pale na ninaliunga mkono.
 
Akizungumza mapema leo Julai 23,2021,katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai amesema "Sisi kama Bunge tulikaa kwa pamoja na kujadiliana kisha tukaamua kuwa na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi,"amesema na kuongeza;

"Tumepitisha na tukatunga sheria , tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofaut,CCM hoyee,nimemaliza,"amesema Spika huyo
 
Anachukua kwenye miamala ili ziwe zinamsaidia India.Huku maskini wanakwenda na dumu la maji hospitalini.
India wenyewe na Corona yao wanatafuta pakukimbilia huyu ataishia pale MNH au BMH hapo Dodoma Mungu ni mwema siku hizi tupo sawa mwenye uwezo asiyekuwa na uwezo wote tunakutana viwanja vya nyumbani leo utasikia huyu Regency huyu Muhimbili huyu Hindu Mandal alimradi hakuna anayetoka nje ya mpaka.

Muda wake unakuja mwache tu azungumze jeuri ipo siku.
 
Wale wa kuhamia Burundi hamie fasta, haka kagonjwa ka akili kameshaamu na ndiyo imetoka hiyo.
Katakufa muda si mrefu lakini haitabadisha kitu kwenye issue ya tozo.
IMG_20210723_170036.jpg
 
M
Spika Ndugai amesema wabunge wameshapitisha tozo ya kizalendo kwenye miamala ya simu na sasa ni sheria hivyo asiyeitaka atupe njia mbadala ya kutufikisha 2025

Roho wa Bwana akamshukia mtumishi wake Jerry Slaa mbunge wa Ukonga naye akajibu; Wabunge tuanze kulipa kodi.

Labda kama Spika ana swali lingine....lakini sidhani.

Ijumaa kareem?

---
Baada ya mijadala mingi kuhusiana na tozo ya miamala ya simu hususani kwenye mitandao ya kijamii ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameibuka na kudai kuwa tozo hizo ni halali na kwamba fedha hizo zitachagiza masuala ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii kama vile shule,hospitali na maji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu huku akipigilia msumari kwenye tozo hizo kwa kudai kuwa Bunge ndio limepitisha na kwamba wanaopinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania iwe Taifa tofauti katika suala la Maendeleo.

Akizungumza mapema leo Julai 23,2021,katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai amesema "Sisi kama Bunge tulikaa kwa pamoja na kujadiliana kisha tukaamua kuwa na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi,"amesema na kuongeza;

"Tumepitisha na tukatunga sheria , tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofaut,CCM hoyee,nimemaliza,"amesema Spika huyo.

Chanzo: Malunde
Mshahara wako mwenyewe hukatai Kodi. Tutapata pesa kutokana na Kodi za mishahara ya wabunge.tuanzie hapo
 
Bila unafiki sijawahi kuskia point ya maana toka kwa spwika KABISAAAA sijawahi! zaidi ya kuona mihasira,kupigana na micheko ya dharau hamna lolote la maana nimeshuhudia kwake!! Kwamimi kanizidi uzee,ufupi,ujinga na cheo baaasi
 
Kuna makundi mengi ya Watanzania hayalipi kodi..

Kuna mdau The Boss alishayaweka humu kwa urefu kabisa
Watanzania wote tunalipa.kodi, ukinunua pipi unalipa Kodi nguo unalipa Kodi, watafute Mbinu nzuri ya kusanya Kodi, hata huko kwenye miamala wanakata Kodi mbili, asilimia 18 na Kodi ya uzalendo ambayo inaenda sambamba na faida ya mtoa huduma au mbunifu
 
Mkuu afadhali umekemea huu upumbavu. Umejaa sana humu jukwaani haswa baada ya kifo cha JPM. Wanavyoombea watu wafe utadhani wao kwa sasa wanaishi mbinguni na duniani kwa wakati mmoja.

Ni aina fulani ya mawazo ambayo ni ya kipuuzi sana.
Ukiwa mdhalimu na mnyang'anyi lazima uombewe kifo ili usilete madhara zaidi, na bahati nzuri maombi yao yanajibiwa positively!
 
Watanzania wote tunalipa.kodi, ukinunua pipi unalipa Kodi nguo unalipa Kodi, watafute Mbinu nzuri ya kusanya Kodi, hata huko kwenye miamala wanakata Kodi mbili, asilimia 18 na Kodi ya uzalendo ambayo inaenda sambamba na faida ya mtoa huduma au mbunifu
We ishia hapo hapo

viwango tunapishana
Mbunge na mtumishi wanalipa kodi sawa?
Mbunge analipa PAYE?.
Machinga wanalipa kodi kwenye vipato vyao?
Usitucharue

Mbinu ni makundi yote nchini yalipe kodi kwenye vipato vyao
 
Nadhani kuna sehemu watanzania hatuelewani sisi kwa sisi hali zetu! Sijui tutumie njia ipi tuelewane kuanzia viongozi mpaka sisi raia.

Tufikirie njia nzuri ya kuelewana, vinginevyo hali si nzuri huko mbele.
 
Back
Top Bottom