Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

wabunge waongezewe kazi, isiishie tu kupiga makofi Bungeni , waongezewe majukumu ya kufanya usafi nyumba za wazee na mayatima maana Serikali ina upungufu wa watumishi.
 
Haina shida,ndugai yuko sahihi. Maana walimu wa shule za msingi wanafundisha masomo yote ndo maana hakuna uhaba wa walimu katika shule za msingi.Ndugai ni akili kubwa ,kumuelewa hadi uwe na PhD,na nionavyo Mimi kwa Tanzania ya sasa hatuhitaji madaktari wa meno,sijui figo,moyo nk. Ni upotevu wa pesa haiwezekani daktari yeye kazi yake ni kutibu meno tu au macho,ni matumizi mabaya ya raslimali watu,daktari wa meno inapidi pia asomee ubongo,figo nk.ili kuwa na matumizi sahihi ya raslimali watu.

Safi sana,kuna wakati viongozi wetu huwa wanatoa maoni /kauli hadi unashindwa kujua hii kauli ilitolewa na huyu kiongozi akiwa katika khali gani.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
no offense lakin wagogo ni kabila lililo zubaa kijinga.
yaan wameridhaka na ile level ya ufukara walionao.. hawataki kwenye extra mile.

sasa pale dodoma mjini wameshaondolewa na wageni. taratiiibu watajikuta kongwa wakikaa vibaya.
hawashtuki tu
 
Hayo madaftari 1500 ili usahihishe inabidi kwanza wafanye swali moja tu,pili usifundishe siku nzima usahihishe.
 
Duh ko kama shule ina PCB awepo mwalimu mmoja HKL mwalimu mmoja sasa hapo wanataka kuomgeza ajira au kupinguza ajira mbona hyo solution haieleweiki! Je ufanisi wa mwali katika ufundishaji utakuwaje aandae mambo ya kufundisha kwa hayo masomo duh kwel hii n bongo
 
Masomo matano hapana itaua motisha na itakuwa ilimradi niliingia darasani wanafumzi waelewe wasielewi watajua wenyewe ,bora angesema waajiriwe ....mbona wako wengi sana mtaan? Kuwaongezea ina maana kuna uhaba wa walimu wakati graduates wako wa kutosha.
 
heee! sasa mtu kasomea in deep masomo mawili a -level mpaka university leo umpangie afundishe masomo manne yapi tena na kwa uelewa upi alionao! eati wengine jamani sijui wanafikiria kwa kutumia nini!
 
Hivi huyu mtu ana elimu gani(amesomea nini??) ningependa kujua maana katika empty set ninazozijua huyu ni wa kwanza yaan katika sector ya poor reasoning nampa cheo cha brigedia general
Mtaalamu wa wanyama pori huyo

Ana akili nzuri sana tu namfahamu, sema hata ungekuwa wewe ungekuwa katika nafasi yake ungefanya kinachoendana na mfumo

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
what makes me so happy is the fact that we all gonna die someday! na sheikh wangu ananiambia kuwa ni siku ngumu sana hiyo; utatamani hata upate dakika moja ya kutubu kwa uliowaonea, uliowadhulumu, uliowakera kutokana na kiburi au shibe ya upendeleo n.k. Utatamani urudishe au ugawe ulivyovuna kwa mgao usio sawa wala haki.

Mwenyezi mungu nijaalie kifo chema kwa kuniweka mbali na majivuno, kejeli, kebehi, ulafi, dhulma n.k. AMEEEN!!!!!
 
Speaker angeonekana wa maana endapo angeshauri serikali iajiri walimu wengi zaidi kutatua tatizo la uhaba wa walimu lakini kusema waongezewe masomo ni kuongeza mzigo kwa walimu.
 
Mbona wao wamekimbia hiyo kazi wapo mule kupasha tu joto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…