Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Akikazia mawazo ya wabunge kama kawaida yake nimemsikia Mh Speaker ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwaongezea masomo ya kufundisha walimu kwa maana ya kuwafundisha kuyafundisha tangu wakiwa vyuoni hasa vyuo vikuu ili kupunguza uhaba wa walimu na kuongeza tija kwa wanafunzi.

Akitolea mfano wa Balozi Mbelwa Kairuki alichomsimulia kule China mwaka jana, Ndugai amesema kuwa kule China vijana wanajua mambo mengi sio kama hapa Tanzania ambapo kijana anajua kazi moja tu kama ni fundi ujenzi ni ujenzi tu na kama ni kuchomelea ni kuchomelea tu.

"Kwanini mwalimu wa high school nafundisha somo moja" eti mmesomea kufundisha somo moja tu ili iweje na uhaba huu wa walimu alihoji speaker Ndugai.

Anatakiwa afundishe masomo matatu, manne au hata kuendelea .hali iliyoibua hoja ya mkwamo wa walimu wanaongojea kazi serkalini na kujiuliza watakwenda wapi? Kama wazo la speaker litafanyiwa kazi
Ha ha ha kwani walimu wameisha mitaani ambao hawana ajira?.Ashauri pis walimu walioacha ualimu na kwenda kwenye ubunge wawe wanafundisha wakati ambao sio wa vikao vya bunge,ili kupunguza uhaba huo, mfano mzuri ni rais wetu mpendwa Dr.John Pombe Magufuli alikuwa anafundisha pindi huko chato wakati ambao sio wa vikao vya bunge.
 
Speaker kaongea pumba kwanini asishauri serikali iajiri maelfu ya walimu walioko mtaani?
Kuliko kulundikia hao walimu mzigo.
Hivi mazingira ya ulaya na hapa kwetu yanalingana?kea Nini tunapenda kujilinganisha na mataifa makubwa wakati hata Angola wanatuzidi kiuchumi?Ni aibu.
 
Kweli tumepatwa awamu hii... Huo uhaba wa walimu mashuleni ni kwa sababu hatuna vijana wahitimu wa ualimu mitaani ama ni kwamba serikali haiajiri?
Kama hizi ndizo fikra za Spika wa chombo Cha uwakilishi nchini,Basi Kama Taifa tayari tumezama matopeni... Kuna mamb yanatia kichefuchefu
 
MATAGA njooni muitete spika yenu huku.

Juhudi za mataga kutetea zinaenda zinapungua kila siku.

Hii ngoma Ni Kama msalaba wajumuia hauruki nyumba

Mitano Tena .
 
Mwambieni deportivo inapenda watu wenye kisukari mnoo, angejikita kwenye kujikinga zaidi kuliko hizi tantarira.
Kila nikiona mtu kaandika deportivo nacheka mpaka mbavu zinauma.
Anyway huyu Ndugai anyamaze tu. Yeye yupo huko bungeni hamna cha maana anachokifanya na bado analipwa hela nyingi.
Asitukaushe kizazi mfyuuuu
 
Haina shida,ndugai yuko sahihi. Maana walimu wa shule za msingi wanafundisha masomo yote ndo maana hakuna uhaba wa walimu katika shule za msingi.Ndugai ni akili kubwa ,kumuelewa hadi uwe na PhD,na nionavyo Mimi kwa Tanzania ya sasa hatuhitaji madaktari wa meno,sijui figo,moyo nk. Ni upotevu wa pesa haiwezekani daktari yeye kazi yake ni kutibu meno tu au macho,ni matumizi mabaya ya raslimali watu,daktari wa meno inapidi pia asomee ubongo,figo nk.ili kuwa na matumizi sahihi ya raslimali watu.

Safi sana,kuna wakati viongozi wetu huwa wanatoa maoni /kauli hadi unashindwa kujua hii kauli ilitolewa na huyu kiongozi akiwa katika khali gani.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
dah, uliwaza kwanini shule za msingi ndani yakata zinaweza kua hata tano lakini shule ya sekondari ipo moja,? pia elewa huyu mwalimu alipo faulu form four kwenda five anasoma masomo 3 na anapoenda chuo kikuu anasoma masomo mawili tu
 
Hayo madaftari 1500 ili usahihishe inabidi kwanza wafanye swali moja tu,pili usifundishe siku nzima usahihishe.
Kama swali ni kujieleza na linachukua dakika tatu kulipsahiisha zidisha kwa 1500 = 4500 kisha gawa kwa 60 ni masaa mangapi? Zaidi ya masaa 70 kama siku 3 mfululizo bila ya kupumzika. Kiujula hata kama muda ni chini ya hapo siku moja haitoshi.
Sasa hii ni elimu gani?
Ni sawa na kutoa dozi moja ya mseto vidonge 24. Kwa wagonjwa 24 ukiamini watapona!
 
Bwashee mbna nmekuelewa nusu
Wagogo wanaomba kujengewa maghorofa makubwa makubwa Dodoma!

Yaani kila kitu wanaomba hawajuwagi kujiongeza.

Taratibu wanaondolewa mjini kisayansi watabakia pembezoni tu Kibaigwa, Bahi na Mtera.

Warangi nawakubali sana akina Kimbisa ni watu wa kujiongeza sana!
 
Kwel aliewaita mataga hakukosea na ww n taga kuu ipo cku utashikwa makaadu na utasema ni sawa tu

Back
Top Bottom