Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Spika Ndugai ataka Walimu waongezewe kazi wafundishe masomo kuanzia matatu ili kupunguza uhaba wa Walimu

Ni simpo tu, kila kipindi ni dakika 10 na mada inalainishwa kama mlenda. Twende tukapige kazi mtani. Unaumiza akili ya nini wakati tupo uchumi wa kati?[emoji86][emoji86][emoji86][emoji86]
 
Kwa hilo somo moja au hayo masomo mawili tayari MTU ana load ya kutosha, vpi wakimwongezea masomo mengine!!! This is absurd.

Uhaba wa walimu hautatuliwi kwa kumrundikia mzigo mwalimu mmoja bali kuajiri walimu wengine.
 
Akikazia mawazo ya wabunge kama kawaida yake nimemsikia Spika ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwaongezea masomo ya kufundisha walimu kwa maana ya kuwafundisha kuyafundisha tangu wakiwa vyuoni hasa vyuo vikuu ili kupunguza uhaba wa walimu na kuongeza tija kwa Wanafunzi.

Akitolea mfano wa Balozi Mbelwa Kairuki alichomsimulia kule China mwaka jana, Ndugai amesema kuwa kule China vijana wanajua mambo mengi sio kama hapa Tanzania ambapo kijana anajua kazi moja tu kama ni fundi ujenzi ni ujenzi tu na kama ni kuchomelea ni kuchomelea tu.

"Kwanini mwalimu wa high school nafundisha somo moja" eti mmesomea kufundisha somo moja tu ili iweje na uhaba huu wa walimu alihoji speaker Ndugai.

Anatakiwa afundishe masomo matatu, manne au hata kuendelea hali iliyoibua hoja ya mkwamo wa walimu wanaongojea kazi Serikali na kujiuliza watakwenda wapi? Kama wazo la Spika litafanyiwa kazi.

Tanzania hatuna uhaba wa walimu bali hatuna pesa ya kuajiri walimu kama inavyohitajika, tatizo letu tunawaza kumkamua ng'ombe maziwa wakati hatumpi chakula cha cha kutosha
 
Kazi ya kuongea ndio Rahisi ikifatiwa na Kazi anayofanya mwenzako
 
Akikazia mawazo ya wabunge kama kawaida yake nimemsikia Spika ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwaongezea masomo ya kufundisha walimu kwa maana ya kuwafundisha kuyafundisha tangu wakiwa vyuoni hasa vyuo vikuu ili kupunguza uhaba wa walimu na kuongeza tija kwa Wanafunzi.

Akitolea mfano wa Balozi Mbelwa Kairuki alichomsimulia kule China mwaka jana, Ndugai amesema kuwa kule China vijana wanajua mambo mengi sio kama hapa Tanzania ambapo kijana anajua kazi moja tu kama ni fundi ujenzi ni ujenzi tu na kama ni kuchomelea ni kuchomelea tu.

"Kwanini mwalimu wa high school nafundisha somo moja" eti mmesomea kufundisha somo moja tu ili iweje na uhaba huu wa walimu alihoji speaker Ndugai.

Anatakiwa afundishe masomo matatu, manne au hata kuendelea hali iliyoibua hoja ya mkwamo wa walimu wanaongojea kazi Serikali na kujiuliza watakwenda wapi? Kama wazo la Spika litafanyiwa kazi.

Kama mtu hajawahi kufundisha na hajui ugumu wa kazi hiyo asibwabwaje, afunge bakuli lake, walioweka mfumo wa walimu kusomea masomo machache hawakuwa wajinga kama yeye
 
Ila maswala ya kiuledi /utaalamu yafanyiwe research sio kuongea tuu

Mh. Mkapa Kuna Jambo aliwah sema kuhusu Elimu inahitaji Taasisi (kamat MAALUMU)
 
Kwa kifupi anatuambia serekale haina pesa za kuajiri.

Tubanane na hawa waliopo.

Sisi hapa wizarani tumeshaanza lifanyia kazi. Soon linashushwa kwa maafisa elimu kwa utekelezaji.

Hakuna anayetaka kutumbuliwa kwa sasa. Tutajua mbele ya safari.
 
Speaker kaongea pumba kwanini asishauri serikali iajiri maelfu ya walimu walioko mtaani?
Kuliko kulundikia hao walimu mzigo.
Wanataka kuwafanya cheap labour. Wasiwaajiri walimu waliyobobea masomo husika tutaendelea na 'education suicide' nchini.

Basi kupunguza gharama pia waziri mmoja ashikilie wizara 5 na jibu watalielewa mbele ya safari.
 
Kwa kifupi anatuambia serekale haina pesa za kuajiri.

Tubanane na hawa waliopo.

Sisi hapa wizarani tumeshaanza lifanyia kazi. Soon linashushwa kwa maafisa elimu kwa utekelezaji.

Hakuna anayetaka kutumbuliwa kwa sasa. Tutajua mbele ya safari.
Serious mkuu?
 
Haina shida,ndugai yuko sahihi. Maana walimu wa shule za msingi wanafundisha masomo yote ndo maana hakuna uhaba wa walimu katika shule za msingi.Ndugai ni akili kubwa ,kumuelewa hadi uwe na PhD,na nionavyo Mimi kwa Tanzania ya sasa hatuhitaji madaktari wa meno,sijui figo,moyo nk. Ni upotevu wa pesa haiwezekani daktari yeye kazi yake ni kutibu meno tu au macho,ni matumizi mabaya ya raslimali watu,daktari wa meno inapidi pia asomee ubongo,figo nk.ili kuwa na matumizi sahihi ya raslimali watu.

Safi sana,kuna wakati viongozi wetu huwa wanatoa maoni /kauli hadi unashindwa kujua hii kauli ilitolewa na huyu kiongozi akiwa katika khali gani.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Wewe akili zitakurudia mshahara ukichelewa kutoka!!

Kwa sasa endelea kuimba pambio.
 
Wanataka kuwafanya cheap labour. Wasiwaajiri walimu waliyobobea masomo husika tutaendelea na 'education suicide' nchini.

Basi kupunguza gharama pia waziri mmoja ashikilie wizara 5 na jibu watalielewa mbele ya safari.
You said it all
 
Duu! Hatari a nusu! Kuna shule za binafsi ukienda unakuta wamechapisha kibao kimeandikwa..."Hatuajili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kufyndisha katika shule hii kwasababu hawakusomea ualimu"! Sasa kama hiyo hoja ya spika itatekelezwa maana yake hata form six watakuwa na sifa ya kufudisha mashulei sababu hata walimu sasa watafundisha masomo ambayo hawakusomea chuoni!
 
Wanataka kuwafanya cheap labour. Wasiwaajiri walimu waliyobobea masomo husika tutaendelea na 'education suicide' nchini.

Basi kupunguza gharama pia waziri mmoja ashikilie wizara 5 na jibu watalielewa mbele ya safari.
Yani watu wakipata madaraka makubwa wanakuwa wajinga kwelikweli
 
Hiyo ni kauli ya kiongozi wa bunge, kwamba mwalimu mmoja afundishe masomo matano tofauti.
Mheshimiwa spika wakishafundisha hayo masom 5 hawa walimu ambao hawajaajiriw watafundisha nin? Au kwao ajira ndo imetoka ivo?
 
Back
Top Bottom