Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Safari hii Bunge limepatwa kwa kuwa na spika wa ajabu haijawahi kutokea
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya CAG na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne, kwa kuwa inapotoshwa huku akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa mmoja wapo

Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.

Mwananchi
Ndugai bado hajaacha tu utopolo, au bado yupo kwenye awamu ya mwendazake
 
Ukiona mtu badala ya kujibu hoja, anasema watu wengine mara wametumwa, au fulani amekosa uzalendo, ujue huyo mtu kichwani hakuna kitu.

Mwenye akili atajibu juu ya kilichosemwa.
Hakika
 
Kwenye taarifa ya CAG si kuna audit queries za aina nyingi na sio tu za mapungufu katika matumizi ya fedha kama ilivyotolewa mfano na Mheshimiwa Speaker? Kuna clarification gani inaweza kutolewa kwa mfano kuhusu hasara ambazo ATC imeingia? Au tamko lake kuwa Feasibility study ya Stieglers Gorge ni ya miaka hamsini iliyopita? Au vifaa vilivyotumika kujenga baadhi ya miradi havikupimwa kama inavyopaswa? Au ile ya matumizi ovyo ya pesa katika wizara pendwa mojawapo ambapo ushauri ni wahusika washughulikiwe? Audit queries mnayozungumzia ni sehemu tu ya maswali yaliyoibuliwa.

Amandla...
 
****** itakua ni Ded wa Bai,Mbowe mbona hajaongelea ripoti ya CAG
 
Ndugai yuko sahihi.

Mbowe amechambuliwa huko ulaya taarifa ya CAG akameza anakuja kujiropokea hapa Bongo.

Kwa tunaojua mambo ya kihasibu hatushangai na hua hatukurupukii taarifa ya CAG maana mkaguzi asipoelewa kitu basi hukibeba kama kilivyo kwenye report yake.

Ndio maana cases nyingi ambazo hua CAG anataja, watuhumiwa wakiitwa kwenye kamati za Bunge hua majibu yanatolewa na baadae zinaonekana hazina msingi.

Sasa Mbowe ametafsiriwa report na wazungu huko anakuja kujiropokea tu hapa.

Sidhani kama Freeman Mbowe Jana ktk hotuba yake alifanya uchambuzi wowote specific wa ripoti ya CAG zaidi kwamba kutoa kauli za jumla tu ambazo kila mtu anasema akiwemo yeye mwenyewe Spika Ndugai...

Waliotoa uchambuzi wa ripoti ya CAG kwa ukamilifu na kitaalamu ni ACT WAZALENDO na ripoti yao iko humu...

By the way, mbona ripoti hiyo ya CAG iko wazi kwa kila mtu kuisoma na kuelewa, hao wabunge wanaoagizwa na Ndugai wa kamati za PAC na LAAC wanaweza kuja na utofauti gani kupinga ukweli wa ripoti yenyewe...?

This is ridiculous......right?

Yeye Ndugai angejielekeza kupinga tuhuma za yeye na wabunge wenzake wa CCM kuhongwa na Magufuli na serikali yake zilizotolewa na Freeman Mbowe ili waweke akili zao mfukoni ili kuwezesha uchafu huu ulioanikwa na CAG utendeke...

Likely, Ndugai hakusikiliza au kutazama hotuba ya Freeman Mbowe na labda kaambiwa tu huko...
 
ALIPOKUWA ANAUMWA ALIPANDA NDEGE KWENDA KWA MABEBERU KUTIBIWA. HUYU MTU NI TAAHIRA ASIYE NA KUMBUKUMBU.

YULE MWINGINE ALIKUWA ANAUMWA ILIBIDI AFE MIAKA MINGI ILIYOPITA ILA MABEBERU WAKAMUWEKEA BETRI KWENYE MOYO, NA KWA JINSI ASIVYO NA SHUKRANI AKAWA ANAWATUKANA WALIOSHIKA UHAI WAKE, Magofool!
🤗️🤗️🤗️🤗️
 
Sidhani kama Freeman Mbowe Jana ktk hotuba yake alifanya uchambuzi wowote specific wa ripoti ya CAG zaidi kwamba kutoa kauli za jumla tu ambazo kila mtu anasema akiwemo yeye mwenyewe Spika Ndugai...

Waliotoa uchambuzi wa ripoti ya CAG kwa ukamilifu na kitaalamu ni ACT WAZALENDO na ripoti yao iko humu...

By the way, mbona ripoti hiyo ya CAG iko wazi kwa kila mtu kuisoma na kuelewa, hao wabunge wanaoagizwa na Ndugai wa kamati za PAC na LAAC wanaweza kuja na utofauti gani kupinga ukweli wa ripoti yenyewe...?

This is ridiculous......right?

Yeye Ndugai angejielekeza kupinga tuhuma za yeye na wabunge wenzake wa CCM kuhongwa na Magufuli na serikali yake zilizotolewa na Freeman Mbowe ili waweke akili zao mfukoni ili kuwezesha uchafu huu ulioanikwa na CAG utendeke...

Likely, Ndugai hakusikiliza au kutazama hotuba ya Freeman Mbowe na labda kaambiwa tu huko...

Huyo Ndugai ana Mbowephobia ndio maana akajichanganya na uchambuzi wa Zito. Kimsingi mwanaccm yoyote anawahofia zaidi cdm kuliko ACT. Ndio maana inakuwa rahisi wao kujicontradict kwenye mambo ya ACT kuwa ni ya cdm.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya CAG na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne, kwa kuwa inapotoshwa huku akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa mmoja wapo

Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.

Mwananchi
Ukitapatapa utajikuta unajipiga mwenyewe.
 
Jamaa huyu hivi ilikuwaje akaukwaa uspika..aisee mtu anaongea hadi msikilizaji ndio unaona aibu
 
Huyu subwoofer Tanzania imepata subwoofer wa hovyo kuwahi kutokea ni bora niwasikilize watoto wasiojua kusoma na kuandika wataniuliza maswali clitical kuriko huyo mfuga nyuki hakuna anachokijua kabisaa...daah kila siku anaongea vitu vya hovyo utadhani ana ubongo wa kupandikiza sasa hapo ndio full kiyoyozi akili hizo angekua anatafuta kama sisi angekua zezeta...
 
Back
Top Bottom