Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Spika siku zote huwa upande wa Serikali dhidi ya CAG badala ya kuwa kinyume chake

Yani Ndugai bwana. Yani hapo tayari anafanya mzaha wa uchama — CCM vs CHADEMA. Sijui kwa faida ya nani?
 
Huyo ameflash akili zake siyo Kama za enzi za Jakaya na Magufuli. Kila msimu anajiflash
 
Wakuu ama kweli kuishi kwingi kuona mengi. Jana Mbowe alifanya press kuzungumzia mambo kadha wa kadha yahusuyo nchi na suala zima la COVID 19.

Hapo jana pia mh Zito Kabwe alikuwa live katika kituo cha ITV akiichambua ripoti ya CAG katika muktadha wa kitaalamu.

Katika wanasiasa hawa wawili ni Zito pekee ndiye aliyezungumzia ripoti ya CAG kwa ujumla wake lakini cha ajabu spika wa bunge Job Ndugai amemlaumu Mbowe kwa kupotosha taarifa na ripoti ya CAG ilihali Mbowe hakuchambua ripoti ya CAG.

Je huyu spika ana ugomvi binafsi na Mbowe? na kama hapana kwanini anapenda kutumia mamlaka ya umma kumuatack mtu personaly?
 
ACT chama washirika toka kulindwa kwake,haupendi kumkwaza kiongozi mkuu wa tawi
 
Nami sioni hekima na ulazima wa kutajwa mtu bungeni ambae hawezi kujitete hukohuko bungeni. Hajakaa sawa
Hapo ndio najiuliza hili Bunge ni la wananchi ama ni la serikali.?
Mimi pia najiuliza Spika ni mteule wa Serikali au Wabunge. Akumbushwe wajibu wake na wajibu wa Bunge. Anatuzalilisha wanachama hata Kama uelewa wetu mdogo
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya CAG na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne, kwa kuwa inapotoshwa huku akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa mmoja wapo

Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.

Mwananchi
CAG hana huruma na mzaha kabisa.
Nimeona ametoa hati ya mashaka Wilaya ya Bahi. Mkurugenzi wa Wilaya ni mke wa Ndugai.

CAG ameweka wazi ufisadi wa sh.364,107,100 mapato ya ushuru yaliyotafunwa bila kupelekwa benki.
 
Risiti ya m499 ziwepo za m1 zisiwepo kisha mkaguzi aandike kuna utata wa m500? Ukaguzi wa wapi huo?
 
Ndugui ni bora ukakaa kimya kwani wewe ni mtu ambae hujawahi kueleweka!
Ndugai wewe ni mtu ambae hujawahi kuwa na msimamo wako zaidi ya kupelekeshwa!
Wewe ni spika wa kwanza kulifanya bunge kuwa dhaifu kuliko mabunge yote.
Sitaki kuelezea unapopigia debe mradi wa bandari Bgmy kwani nilishasema wewe ni kigeugeu usie na msimamo kamwe.
Kikubwa kumbuka wewe ni mbunge wa kongwa tofauti na Mbowe ambae ni m.kiti wa chama kikubwa sana na mtu maarufu duniani wakati wewe ni maarufu kongwa tu.
 
Ndugai yuko sahihi.

Mbowe amechambuliwa huko ulaya taarifa ya CAG akameza anakuja kujiropokea hapa Bongo.

Kwa tunaojua mambo ya kihasibu hatushangai na hua hatukurupukii taarifa ya CAG maana mkaguzi asipoelewa kitu basi hukibeba kama kilivyo kwenye report yake.

Ndio maana cases nyingi ambazo hua CAG anataja, watuhumiwa wakiitwa kwenye kamati za Bunge hua majibu yanatolewa na baadae zinaonekana hazina msingi.

Sasa Mbowe ametafsiriwa report na wazungu huko anakuja kujiropokea tu hapa.
Wabongo bana Dubai ni ulaya?
 
ATCL kujua kama imepata faida au hasara CAG alitakiwa achukue hiyo bilioni 60 loss ya kwenye vitabu atoe pesa ambayo ATCL ilitoa gawio yaani dividend kwa serikali halafu atoe Kodi zote ambazo ATCL imelipa kwa seikali kuanzia VAT za tiketi za ndege ambazo kila abiria hulipa na kodi zingine zote ATCL imelipa nk
Hiyo hasaracya bilioni 60 CAG alikose A compute upya
 
CAG hana huruma na mzaha kabisa.
Nimeona ametoa hati ya mashaka Wilaya ya Bahi. Mkurugenzi wa Wilaya ni mke wa Ndugai.

CAG ameweka wazi ufisadi wa sh.364,107,100 mapato ya ushuru yaliyotafunwa bila kupelekwa benki.
haya ndio yanamfanya ndugai kuwa kigeugeu na mtu asie na msimamo. aibu sana
 
Anamshutumu Mbowe wakati hata bunge lenyewe bado halijachambua report ya CAG.
 
Huyu Ndungai akae kimya. Hana uhalali wowote wa kuwa speaker.Huyu si alipitishwa ubunge bila kupingwa kwa taratibu za kihuni?

Halafu Bunge analoliongoza wabunge wake walipita kwa wizi wa kura .Hana kibali toka kwa wananchi ,wapiga kura kuwa speaker wa Bunge.

Kungekuwa na mahakama iliyo huru hakika Ndungai asingekuwepo katika hicho kiti.YEYE pamoja na wabunge anao waongoza!
 
Hakika sipati picha kwanini kuna baadhi ya Watu wanajaribu kutumia mpaka Nguvu zao zote kupinga Ripoti ya CAG .CAG ni Mteule wa Hayati Magufuli,Hayati Magufuli alimwamini CAG ndio maana Akamteua leo iweje mpinge Utendaji wa CAG aliyeteuliwa na Hayati Magufuli?

Mnavyomwamini Hayati Magufuli kwa Utendaji Wake basi Muaminini na CAG kwa Ripoti yake Acheni Unafiki .CAG ameripoti kile Alichokagua na kuelezwa na Watendaji Wenyewe.Ripoti ya CAG iheshimiwe na ndio Sababu Rais Wetu Ameipokea.
 
Marehemu Magufuli siyo hayati tena.

Ripoti haipingwi ila inajadiliwa na kujadiliwa na kufafanuliwa undani wake na watu wenye uelewa japo mengine hayahitaji hata uelewa.
 
Hakika sipati picha kwanini kuna baadhi ya Watu wanajaribu kutumia mpaka Nguvu zao zote kupinga Ripoti ya CAG .CAG ni Mteule wa Hayati Magufuli,Hayati Magufuli alimwamini CAG ndio maana Akamteua leo iweje mpinge Utendaji wa CAG aliyeteuliwa na Hayati Magufuli? Mnavyomwamini Hayati Magufuli kwa Utendaji Wake basi Muaminini na CAG kwa Ripoti yake Acheni Unafiki .CAG ameripoti kile Alichokagua na kuelezwa na Watendaji Wenyewe.Ripoti ya CAG iheshimiwe na ndio Sababu Rais Wetu Ameipokea.
Ni ujinga tu unawasumbua, ripoti zote kila mwaka ziko hivyo,zinaonyesha mapungufu katika maeneo mbalimbali na hazimhukumu mtu moja kwa moja bali zinaacha jukumu la kurejebisha au kuwajibisha kwa mamlaka husika.

Sioni sababu ya povu linalowatoka watu na kumlaumu CAG kana kwamba ametoa hukumu kwa Rais wa awamu ya tano. Wanaofanya hivi wana agenda ya siri ya kumhujumu Mama Samia.
 
Back
Top Bottom