Kuna jambo moja ambalo Ndugai analikwepa, na pia kuna kosa Ndugai anafanya, hivyo naweza kusema anafanya makosa makubwa mawili kwa makusudi.
1.Spika huwezi kutoa agizo au maelekezo kwa chama cha siasa kwa mdomo bali anapaswa kufanya hivyo kwa kuwaandikia CHADEMA barua rasimi licha ya ukweli kuwa hata haki hiyo ya kuhoji maamuzi ya CHADEMA hana.
2.Pili, kama anataka nyaraka za kuwafukuza uanachama wabunge hao, atuonyeshe au ahoji pia nyaraka za wabunge hao kuteuliwa na CHADEMA kuwa wabunge wa viti maalumu kutoka kwa Mamlaka iliyowasilisha majina hayo kwake(NEC).
CHADEMA mawasiliano yote kuhusu hili sakata yako kimaandishi ila Ndugai anapiga porojo tu(naona anakwepa maandishi ingawa ana kinga na zaidi anafikiri CHADEMA watafanya anachokitaka).
Viatu alivyovaa Ndugai si size yake.