Spika Ndugai: Mnaogopa nini kuleta viambatanishi ili tuwavue Ubunge kwa Haki?

Sio kazi ya ndugai kamwe...kwa Sofia Simba na wabunge wa cuf hatukuyasikia hayo..
 



Huyu mzee drama sana Je huko nyuma ndiyo walikuwa na utaratibu huu au ni utaratibu mpya?
 
Ndugai anajiamini sana inaonekana kuna kitu anakijua na mkiendelea kumtukana kuna siku atakisema.

Tatizo misukule ya chadema tukisema hili chezo Mbowe na Mnyika wanalijua hamtaki kuelewa, ndio maana wenzenu waliwaita nyumbu!

Upuuzi mtupu, enzi za JK alikuwa naibu spika, mikataba ya gas ilipitia hapo bungeni kwa hati ya dharura, leo hii tunaambiwa gas sio yetu, yeye amebaki kuendekeza ushindani wa siasa za kijinga alizoachiwa na yule dhalimu. Mambo ya maana yanamshinda, kabaki kuendekeza siasa chafu kwenye hicho kiti.
 



Unasema tuwavue !!! Je wameingiaje hapo bila Chama kuwapitisha ?? Hapo ndiyo pa kuanzia Je utaratibu gani umetumika kwa spika kuwakubali hawa wabunge? Barua ziko wapi za kuwateuwa?
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke.

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao.
kwani chadema waliwapa ubunge? mbona mnajitoa ufaham?
 
Hakuna anachoelewa yule. Ni ujinga tu. Suala siyo kufukuzwa uanachama, bali CHADEMA hawakuwahi kuteua wabunge wa viti maalum. Spika aseme alipata wapi majina?
Kwani barua waliyopeleka Bungeni ilikuwa ya kukana kuwa hawajapeleka majina NEC au ilikuwa ya kumtaarifu Spika kuwa ao watu waliopo humo Bungeni tumewafuta uanachama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPUUZI MTUPU! Yeye kwanini asilionyeshe Taifa vielelezo vyote kuhusu kikao cha kuwateua hao COVID-19?
 
hivi mbona hamna akili nyie documents za nini? barua ya kuwateua waliipata wapi waeleze hilo kwanza
 
Huyu mzee drama sana Je huko nyuma ndiyo walikuwa na utaratibu huu au ni utaratibu mpya?
Issue sio huko nyuma ila yeye anaongoza kwa sheria, kanuni na hekima pia hivo basi wataoluja huko mbele kuwa Maspika watamrefer pia Ndugai kuwa unapofukuza mwanachama ambae ni mbunge ili kuweka taarifa sawa basi wasilisha pamoja na muhtasari wa kamati tendaji na katiba yenu.

Nafikiri Ndugai hajakosea kwakweli ila shida hipo upande wa pili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana nikakwambia hizo ni siasa hivyo huwezi kusema eti ndugai hampendi Mbowe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…