Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Nafikiri ndugai na wewe mleta uzi pamoja na tbc Ccm mna matatizo. Mnyika hajamfokea mtu. Mnyika amehoji kuhusu utaratibu/procedure za kupitia mpaka kupata mbunge wa vitu maalum. Yule ndugai anaongea ujinga tu. Leo mdee na bulaya sio wasaganaji yena ni mashujaa?
 
Namna pekee ya kuthibitisha uhalali wa hawa wabunge ni NEC kuonyesha barua ya uteuzi wao kutoka Chadema. Na kuweka wazi fomu walizojaza kukubali uteuzi huo zikiwa na sahihi za viongozi wenye mamlaka ya kufanya hivyo....
Bravo mkuu
 
Lisu alipotangaza Seif kuwa ndio mgombea wao wa urais Zanzibar, kuna kikao gani kilikaa?
Acha upuuzi wako wewe. Raisi/mwenyekiti wa yanga akisema tutaishangilia simba jumamosi mpaka pawe na kikao???? Kuna tofauti gani kati ya hilo na Lisu aliposema tunamuunga mkono swift?? Ulisoma shule gani wewe? Hujui hata comparison??
 
Ila sidhani kama Mnyika kamwelewa. Mnyika kupayuka hadharani bila kujuwa msimamo wa wakubwa wake ukoje na maamuzi ya vikao vya juu yatakuwaje ni kupwaya kwenye wadhifa wake wa katibu mkuu. Aliyoyasema yalipaswa kusemwa na katibu mwenezi au mwenyekiti mwenyewe ambao nao ingalikuwa ngumu kusema hayo kabla ya maamuzi ya vikao vya chama.

Kama kamati kuu ya chama itaamua kinyume na alichokisema, Mnyika atapaswa kujiuzuru ukatibu mkuu.
Hivi mnaamini Mnyika alijisemea tu? Ikumbukwe kuwa yeye ni Mtendaji Mkuu wa Chama hicho kwa hiyo sio mtu mdogo.

Amandla...
 
Ndugai anapaswa akajifunze kwa Mama Anna Makinda au Msekwa maana bunge chini ya Ndugai limekuwa kama kijiwe cha kahawa,limepwaya!
Sio cha kahawa ni kijiwe cha kupanga utapeli na dili ndio zinafanyika hapo sasa
 
Mnyika tafuta kazi
IMG-20201126-WA0042.jpg
 
Kama mnyika anapaswa kujifunza ukatibu kwa bashiru basi MAGUFULI akajifunze uraisi kwa waliomtangulia maana hata alitumia sms na PM anasema hadharani. Ndugai hayupo sawa kichwani yule
 
Wanunueni waingie CCM Kama mnawataka. Pia CCM ukumbuke kile kitabu chai chenye kurasa 303.
Wababaishaji tu.
Ilani iliyopita ilikuwa na kurasa chache sana walishindwa kumaliza pamoja na vingine kuvitupa njiani.
Walikuwa busy sana na manunuzi ya 'watu'.
Safari hii wameanza mapema zaidi
 
Hata hivyo Bunge ni dhaifu,goigoi hawawezi kitu chochote zaidi ya kutumia miguvu badala ya kufuata Sheria!
 
Wapinzani ambao mwenyekiti wa CCM amekuwa akiwaaminisha wananchi kwamba wanaokwamisha maendeleo mbona sasahivi wanaliliwa kwa nguvu hivi [emoji23]
 
Hivi mnaamini Mnyika alijisemea tu? Ikumbukwe kuwa yeye ni Mtendaji Mkuu wa Chama hicho kwa hiyo sio mtu mdogo.

Amandla...
Tofautisha mtendaji mkuu na msemaji mkuu wa tasisi. Ulishaona wapi kwa mfano katibu mkuu wa wizara akawa ndiyo msemaji mkuu wa wizara? Kipi kitampata kama atakayoyasema siyo msimamo wa wizara yake au waziri wake?

Mnyika anafanya uanaharakati badala ya ukatibu mkuu. Ndiyo maana wahusika wamemunyamazia. Kesho ataona mziki wake. Akina Mdee, Matiko na Bulaya siyo watu wadogo kwenye hicho chama. Wana uwezo wa kuendesha mapinduzi kwenye hicho chama.
 
Back
Top Bottom