Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.


Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!

Maisha yanapita kasi sana, kufumba na kufumbua Ndugai na Bashiru hawana political power, hatari.
 
Back
Top Bottom