Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.

Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!
Daaah ubongo umevimba mungu ni fundi sana,hatuna muda mrefu tutamlaki mawinguni
IMG_20201201_075951.jpeg
 
Spika wa bunge Job Ndugai amemtaka katibu mkuu wa CHADEMA akajifunze namna ya kuwa katibu mkuu kwa Bashiru Ally ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM.

Ndugai amesema kitendo cha Mnyika kuwasema hadharani, kuwahukumu na kuwashutumu wabunge wa viti maalum kwenye vyombo vya habari inaonesha wazi Mnyika hafai kuwa Katibu Mkuu.

Ndugai ameshauri mambo kama hayo huongelewa kwenye vikao vya ndani na kisha katibu mkuu hutoka na taarifa za kikao na kuwaambia wananchi sio kupayuka hadharani.

Sambamba na hilo Ndugai amesema kwamba yeye majina hayo kumi na Tisa(19) ya viti maalumu ya CHADEMA amepewa na Tume ya uchaguzi yeye kazi yake ni kuwaapisha tu Wabunge hao na ameshafanya hivyo. Na ameapa kuwalinda Wabunge hao hivyo amewataka wawe na imani kabisa.

Source: TBC ARIDHIO.
Hahaa ccm inaumia sana na maisha ya cdm kuliko watanzania,bashiru ndio katibu mkuu wa hovyo kuwahi kutokea ccm...huku bunge nalo likuwa na spika wa hovyo mwenye upungufu wa kinga mwilini
 
Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.

Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!

Spika anayo mamlaka ya kulizungumzia sakata hili, lakini mamlaka yake yana mipaka.
Spika alipokea horodha kutoka tume ya uchaguzi na kuwaapisha na kuwalinda kwa mujibu wa sheria, hapo ingekuwa amemaliza kulizungumzia hilo kwa mamlaka yake. Lakini kuingiza hoja kwamba wengine hawaja komaa kisiasa hivyo wakajifunze ccm kwa Dr Bashiru hii ni kuvuka mipaka ya mamlaka aliyo nayo kama spika wa bunge la JMT, labda mh spika awe ana imani kwamba yeye ni spika wa ccm hapo ndio angeweza kuzungumza hayo kama kada wa ccm.
 
Ni vyema CDM wakaachana na huyu mtu, waende zaidi kisheria, sidhani kama huyu mtu anastahili kuongea na watu kama Mbowe.
Ama kweli hekima ndio chanzo cha maarifa! ukikosa hekima kumbe binadamu unakuwa kituko kitupu mbele za watu!
 
Nguvu za Ndugai kujilindia yeye mwenyewe uspika hana,matokeo yake wamechukua cheo chao
 
Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.

Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!

Mtafute awalinde...
 
Na sasahivi bado anawalinda?
 
Huyu Mungu bana, imagine Jobo hayupo na Jiwe hayupo tena, afu kuna wapumbavu humu bado hawajifunzi
 
Back
Top Bottom