Kwenye kuendeleza kusimamia haki mwenye macho aambiwi tazama, viongozi wote wameona vilio vya wananchi wanyonge nani atawatetea tena.
Kwenye uchumi nadhani umeshakutana na msemo ‘Rome wasn’t built in a day’.
Sometimes sacrifices za leo ni lazima kwa faida ya kizazi kijacho. Watu waliojenga canals nchi za wenzetu, njia za train za juu na underground; na infrastructure zingine engineers walioshiriki kwenye main designing kwa umri wao wengi waliona mwanzo tu wa projects zenyewe.
Hii miradi ya leo ndio itamfanya mtu alie Arusha miaka ijayo badala kufikiria uwekezaji ni kwenye sector ya utalii tu; kuna opportunity ya kuleta alizeti kutoka Shinyanga mpaka Arusha na train na kukamua mafuta huku aki target soko la kaskazini na nchi jirani.
Watu wanafikiria kutokana na fursa zilizopo, uwezi kufikiria kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya maharage (tin packaging) Tanga wakati hujui utayotoa vipi kutoka mbeya. Lakini ukishawawekea wanatanga access ya barabara au train wanaweza kufikiria hizo possibilities ndio uchumi unavyokua.
Serikali aiwezi kusema iache kutoa elimu kisa inazalisha wasomi kushinda uwezo wa soko kuajiri, hiyo itakuwa ni kuwanyima raia wengine haki zao za msingi. Kwa sasa ni jukumu la wahitimu kuwa wabunifu.
Kupata kwao ajira baada ya kumaliza masomo sio jukumu la serikali, kazi ya serikali ni kuweka mazingira ya kuvutia uwekezaji zaidi ili ajira zizalishwe ndio alichokuwa anajaribu kuwafanyia Magufuli.
Umeshawai kuisikia hii hadithi ya ‘Walt Disney’, alifariki miezi michache kabla ya theme park yake ya kwanza kufunguliwa.
Siku ya uzinduzi mdogo wake akaulizwa “it’s a shame, Walt isn’t here to witness the opening” jibu lake lilikuwa lifuatalo “not at all, he saw all of this first in his head before any of us”. Ndio baadae mtakavyokuja kumuelewa Magufuli investment zikianza kuleta faida.