Spika Ndugai, pamoja na Msamaha kukataliwa atembee Kifua mbele

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mheshimiwa Ndugai kwa kutoa maoni yake kama mtanzania na kama mbunge hakuvunja sheria yoyote.

Kilichofuata baada ya kauli yake hakuna asiyekijua.

Labda ilikuwa katika kudhania afunike kombe, kumbe hapo tena ndipo sasa wale nyuki wa mama walipokuwa wanasubiri!

Kwa matukio mawili haya sasa tunayo picha kamili ya watu wanaotuongoza:

IMG_20220105_143355_470.jpg

Watu hawa ni muda sasa uthabiti wao wa kutuongoza ukahakikiwa kwa kura ya kuwa na imani nao.

"Job Ndugai tembea kifua mbele."

Kama vipi fikiria kuitisha kikao cha bunge cha dharura kabisa kwa ajili ya kadhia hii.

Taifa lina stahili viongozi thabiti.

Nchi huendeshwa kwa mujibu wa katiba.
 
Mbaya sana kumuomba msamaha anaejua amekosea, matokeo yake atafanya kila awezalo kuonesha aliekosea ni muomba msamaha kumbe yeye aliyeombwa msamaha ndie aliekosea, nimejifunza ni kosa kubwa kumuomba mjinga msamaha.

Sasa anapewa sapoti kwasababu ya nafasi yake, kundi kubwa la watu liko nyuma yake kumpongeza "kwa ushindi" aliopata, simply sasa hivi kama taifa akili ndogo ndio ziko juu kwenye chati zinashangilia, halafu werevu wameinamisha vichwa vyao chini.
 
Tatizo tayari Ndungai ameikana hoja yake,sidhani kama atapata uungwaji mkono kwa hoja hewa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app

Uungwaji mkono haukuwapo hata kabla ya yeye hatimaye kujaribu kukubali yaishe.

Kwani hao wa kumwunga mkono walikuwa wanasubiri muda upi basi?

Kama jamii tunayo ya kujifunza:

"Bila kujua tumechangia kwenye kuuchelewesha ukombozi."

Huo ni ukweli mchungu.
 
Ayubu anajua anachofanya..
Hata msamaha wake ulikuwa na dokezo juu ya kinachofuata.

Ayubu hajaachiwa jumba bovu? Kwa body language ya jana? Si ndiyo ya akina Shibuda na CCJ?

Ayubu alistahili waungaji mkono hadharani na kutokea kambi zote.
 
Nyie msaidieni Mh Spika haya yaleo ni matokeo ya kauli yake kuhusu Bandari Bagamoyo muda mfupi baada ya JPM kutwaliwa wengine tukiwa bado tunaomboleza.

Mungu si dhalimu. JPM alimheshimu sana Mh Ndugai hatukutegemea aseme maneno aliyo ya sema kuhusu Bandari ya Bagamoyo.
 
Sizani kama alikurupuka..
Ila nachoamin kuna watu wanamuunga hasa wakubwa.
 
Hili si suala la kumsaidia mtu. Kinachogomba hapa ni Katiba. Mwendelezo wa ukiukwaji huu wa katiba ifike mahali iwe mwisho.
 
"Job Ndugai tembea kifua mbele."

Kama vipi fikiria kuitisha kikao cha bunge cha dharura kabisa kwa ajili ya kadhia hii.
Asijaribu, mpaka sasa kama ni ball possession amezidiwa sana.
 
Mheshimiwa Ndugai kwa kutoa maoni yake kama mtanzania na kama mbunge hakuvunja sheria yoyote.

Kilichofuata baada ya kauli yake hakuna asiyekijua.

Labda ilikuwa katika kudhania afunike kombe, kumbe hapo tena ndipo sasa wale nyuki wa mama walipokuwa wanasubiri!

Kwa matukio mawili haya sasa tunayo picha kamili ya watu wanaotuongoza:

View attachment 2069426

Watu hawa ni muda sasa uthabiti wao wa kutuongoza ukahakikiwa kwa kura ya kuwa na imani nao.

"Job Ndugai tembea kifua mbele."

Kama vipi fikiria kuitisha kikao cha bunge cha dharura kabisa kwa ajili ya kadhia hii.

Taifa lina stahili viongozi thabiti.

Nchi huendeshwa kwa mujibu wa katiba.
The moment atakapoitisha kikao tu, kabla jogoo hajawika mungu atakuwa ameshampenda zaidi kwa kupigiwa risasi nyingi zaidi ya za lisu. This is Africa!!
 
Asijaribu, mpaka sasa kama ni ball possession amezidiwa sana.
Hivi unaona kuna mshindi hapa ?

Ni kama watu wawili waliamua kuanza kurushiana matope mmoja akaamua basi yaishe mwingine ndio kaamua kabisa kuingia mtaloni hili kumwongesha mwenzake....

Huyo anyemwongesha mwenzake aangalie sana sababu na yeye kushika kwake matope na kuyarusha anajichafua....
 
O
Asijaribu, mpaka sasa kama ni ball possession amezidiwa sana.

Hahahaa haa itabidi umtake radhi.

Hadi sasa mbona kwa uelewa wake mechi mbona bado sana?

Mbona hata hajajipambañua katika first 11 yake nani ni nani?
 
The moment atakapoitisha kikao tu, kabla jogoo hajawika mungu atakuwa ameshampenda zaidi kwa kupigiwa risasi nyingi zaidi ya za lisu. This is Africa!!

Hamna kitu mkuu. Zama za giza nene tulishatoka huko.
 
Nyie msaidieni Mh Spika haya yaleo ni matokeo ya kauli yake kuhusu Bandari Bagamoyo muda mfupi baada ya JPM kutwaliwa wengine tukiwa bado tunaomboleza.

Mungu si dhalimu. JPM alimheshimu sana Mh Ndugai hatukutegemea aseme maneno aliyo ya sema kuhusu Bandari ya Bagamoyo.
Unafiki unafiki unafiki unafiki unafiki
 
Sizani kama alikurupuka..
Ila nachoamin kuna watu wanamuunga hasa wakubwa.
Alitakiwa jana alipoitisha press na waandishi wa habari asiikane kauli yake hapo bado watu wangekuwa nae lkn baada ya kukana alichokisema hakuna atakae kuwa nyuma yake
 
Back
Top Bottom