Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

ndugai kawachezea mind game nanyie mkajaa, yule ni sukuma gang pure na wana mikakati yao siku za usoni, endeleeni kuwatch movie hii mpaka ze end ndo mtajua hamjui.
 
Sasa anaomba radhi ya nini? Hawa ndio Punguani aliowasema James Mbatia
1EA63F7E-3B66-4D52-812D-6709E92F0924.jpeg
 
Kwa unavyoelewa wewe. Nini makosa ya Ndugai katika kusema habari ya madeni ya taifa na kupiga makofi watu wakishangilia, tena wajinga wasiojua kwamba mikopo isiyo tija ni mizigo hatarishi? Jadili
Ni wazi kauli yake imeleta uharibifu na mkanganyiko Mkubwa sana. Kwanini alikawia kuomba radhi? Tena badala ya kufafanua akadai anasemwa kwasababu yeye ni Mgogo!

Ndugai angeweza hata kutoa press release kama kweli alikuwa anaumwa kama anavyodai lakini aliamua kukaa kimya mpaka leo Je alikuwa anapima nini?

Je radhi yake ni ya kweli? Au ni namna ya kuwakabili wabunge kwenye kamati zinazotarajiwa kuanza?

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
msamaha ni pale unapotakiwa kusema "nimekosea, niliteleza, nisamehe". ukisema sikuwa na nia mbaya, ila naomba unisamehe kwa sintofahamu, hapo haujaomba msamaha kwasababu haujakirikosa. lazima ukirikosa ndio msamaha ufuate, hata kwa Mungu huwa tunaenda hivyo. unamwambia Mungu nimezini, nimeiba, nina makosa, mimi sio msafi nilijichafua, naomba unisamehe, unioshe uchafu wangu. basi. tusifanywe kwama watoto wadogo hapa.
Samahani haitoshiiii
 
Watu makini wamebuni mulemule Mh. Spika alichokisema. Kuomba radhi na blabla zingine ooh wa-medoctor hotuba yangu.
 
Wakuu
Hii press ya Job leo unaichambuaje?

Je, Ndugai & The Gang walikuwa wanaupima upepo?

Je, wananchi ama wanaharakati wangeonesha kumuunga mkono angefanya hii submission press ya leo?

Thinkers wa JF, mnaiangaliaje hii move ya Ndugai kuomba radhi hadharani leo akiwa kama mkuu wa Mhimili huru wa Bunge? Jambo hili limekaaje
Kisiasa
Kiusalama
Kidemokrasia

Pascal Mayalla
Mshana Jr
figganigga
Mzito Kabwela
Mchambuzi87
 
Wakuu
Hii press ya Job leo unaichambuaje?

Je, Ndugai & The Gang walikuwa wanaupima upepo?

Je, wananchi ama wanaharakati wangeonesha kumuunga mkono angefanya hii submission press ya leo?

Thinkers wa JF, mnaiangaliaje hii move ya Ndugai kuomba radhi hadharani leo akiwa kama mkuu wa Mhimili huru wa Bunge? Jambo hili limekaaje
Kisiasa
Kiusalama
Kidemokrasia

Pascal Mayalla
Mshana Jr
figganigga
Mzito Kabwela
Mchambuzi87
Ni kati ya fasihi bora kuiona kwenye ulingo wa siasa kwa miaka ya karibuni.
Hii ni namba moja. Ikifuatiwa na ile ya Rutengwe, PhD.
Na kwa bahati mbaya Watanzania wengi hawajui fasihi.
Ngoja tuone upande wa pili wataitikiaje.

Hongera sana kwa Job Yustino Ndugai na kundi lako kwa kuweza kuja na somo bora la fasuhi.
 
Back
Top Bottom