Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Juzi tarehe 26 nilikuwa kwenye shughuli nikazungumza baadhi ya mambo baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya Watu wakakata baadhi ya mambo wakawasilisha ujumbe nusu ambao umesababisha mjadala mkubwa katika Nchi yetu mjadala ule umesababisha usumbufu wa hapa na pale nimeona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa” – Spika Ndugai.
 
Ishu ni ujumbe wake umefika,

Hizo nyingine mbwembwe tu
Ujumbe gani?. Mtoa ujumbe amekanusha ujumbe aliotoa na kusema alinukuliwa vibaya. Kitendo Cha kukanusha ujumbe kutoka kwa mtoa ujumbe kunafanya ujumbe uwe batili maana tutakaye mnukuu ameubatilisha ujumbe wake.
 
Huyu jamaa aache uoga, maana tukichekeana hapa tutakuja kupigwa mnada kama alivyosema mwanzo, huwezi kukopa trillion 10 ndani ya miezi 9 kwa miradi isiyo ya kimkakati tena bila idhini ya bunge halafu tukabaki salama, no way!!
Wanasiasa wengi ni waoga hapa Tanzania ukiwatishia ugali wao wanapatwa na muhaho na kubadili misimamo yao. Spika mzima wa bunge anashindwa kuwa na msimamo. Amezidiwa na akina pole pole.

Hapa kilichobaki ni kusubiria mwezi wa nne Tundu Lissu arudi maana ndio mwenye misimamo isiyoyumba.
 
Ni wazi kauli yake imeleta uharibifu na mkanganyiko Mkubwa sana. Kwanini alikawia kuomba radhi? Tena badala ya kufafanua akadai anasemwa kwasababu yeye ni Mgogo!

Ndugai angeweza hata kutoa press release kama kweli alikuwa anaumwa kama anavyodai lakini aliamua kukaa kimya mpaka leo Je alikuwa anapima nini?

Je radhi yake ni ya kweli? Au ni namna ya kuwakabili wabunge kwenye kamati zinazotarajiwa kuanza?

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Ujumbe gani?. Mtoa ujumbe amekanusha ujumbe aliotoa na kusema alinukuliwa vibaya. Kitendo Cha kukanusha ujumbe kutoka kwa mtoa ujumbe kunafanya ujumbe uwe batili maana tutakaye mnukuu ameubatilisha ujumbe wake.
Ni sawa na ule wa Vick Kamata wa kumnanga marehemu Magu kisha baadae akaufuta, lakini meseji ilikuwa imeshafika.

Ujumbe wa Ndugai siku ile hauwezi kufutika kirahisi
 
Mi naona ndugai kaleta changamoto nzuri kwa uongozi wala hakukosea kitu.
Watu wanakuja tu na mapesa yao kuwakopesha kwa nguvu ili mnunue matakataka au bidhaa au huduma toka makampuni yao halafu nchi inakopa tu

Wanapata faida tupu mara mbili. Kwanza kuwakopesha mnalipa riba pili mnanunua toka kampuni za kwao tena bei kubwa tu. Sisi ni hasara tupu. Kwanza kisaikolojia wanakufanyeni tegemezi na wajinga. Pili mnachokopea hakina maana tena hela za mkopo zinaliwa na wao kushirikiana na vibaraka wenyeji. Unakuta hakuna impact yoyote kwa nchi.

Alichosema ndugai tuwe na mikopo ya kuamua wenyewe kufuatana na mipango yetu sio kusukumiziwa mikopo ya kilaghai na kinyonyaji.
 
Wanasiasa wengi ni waoga hapa Tanzania ukiwatishia ugali wao wanapatwa na muhaho na kubadili misimamo yao. Spika mzima wa bunge anashindwa kuwa na msimamo. Amezidiwa na akina pole pole.

Hapa kilichobaki ni kusubiria mwezi wa nne Tundu Lissu arudi maana ndio mwenye misimamo isiyoyumba.
Kwakweli, maana hamna namna tena
 
Kwa msamaha alioomba spika Jobo Sasa anayetaka kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti ccm 2022 ,ajiandae Kuchapwa bakora na jobo Kabla hujarufisha fomu
 
Spika wa Bunge la Senate la Marekani amelaani kitendo kilichofanywa na Spika wa Bunge la Tanzania kwa kumwomba Rais waTanzania kwa kitendo Cha kutoa mawazo yake kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Pia Spika huyo ameongeza kua, kitendo kilichofanywa na Spika wa Bunge la Tanzania linathibitisha malalamiko ya muda mrefu kuwa Bunge la Tanzania siyo chombo huru bali linaongozwa na Serikali kwenye maamuzi yake.

Spika wa Bunge la Senete ameshauri ndugu Job Ndugai Spika wa Bunge la Tanzania aweze kujiuzulu nafasi yake ya Uspika ili kulinda hadhi ya Mabunge kote ulimwenguni kwani kitendo alichokifanya haikubaliki kwenye taratibu ya kuendesha Mabunge.

Chanzo: CNN
 
msamaha ni pale unapotakiwa kusema "nimekosea, niliteleza, nisamehe". ukisema sikuwa na nia mbaya, ila naomba unisamehe kwa sintofahamu, hapo haujaomba msamaha kwasababu haujakirikosa. lazima ukirikosa ndio msamaha ufuate, hata kwa Mungu huwa tunaenda hivyo. unamwambia Mungu nimezini, nimeiba, nina makosa, mimi sio msafi nilijichafua, naomba unisamehe, unioshe uchafu wangu. basi. tusifanywe kwama watoto wadogo hapa.
 
Mi naona ndugai kaleta changamoto nzuri kwa uongozi wala hakukosea kitu.
Watu wanakuja tu na mapesa yao kuwakopesha kwa mguvu ili mnunue matakataka au bidhaa au huduma toka makampuni yao halafu nchi inakopa ttu

Wanapata faida tupu mara mbili. Kwanza kuwakopesha mnalipa riba pilinanunua toka kampuni za kwao tena bei kubws tu. Sisi ni hasara tupu. Kwanza kidaikolojia wanakufanyeni tegemezi na wajinga. Pili mnachokopea hakina maana tena hela za mkopo zinaliwa na wao kushirikiana na wenyeji. Unakuta hakuna impact yoyote kwa mchi.

Alichosema ndugai tuwe na mikopo ya kuamua wenyewe kufuatana na mipango yetu sio kusukumiziwa mikopo ya kilaghai na kinyonyaji.
Ndugai ana hoja ya msingi sn tatizo ni bunge kuwa dhaifu
 
"Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana"

Tangu kuzaliwa kwangu sijawahi mwungamia binadamu mwenzangu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mi naona ndugai kaleta changamoto nzuri kwa uongozi wala hakukosea kitu.
Watu wanakuja tu na mapesa yao kuwakopesha kwa mguvu ili mnunue matakataka au bidhaa au huduma toka makampuni yao halafu nchi inakopa ttu

Wanapata faida tupu mara mbili. Kwanza kuwakopesha mnalipa riba pilinanunua toka kampuni za kwao tena bei kubws tu. Sisi ni hasara tupu. Kwanza kidaikolojia wanakufanyeni tegemezi na wajinga. Pili mnachokopea hakina maana tena hela za mkopo zinaliwa na wao kushirikiana na wenyeji. Unakuta hakuna impact yoyote kwa mchi.

Alichosema ndugai tuwe na mikopo ya kuamua wenyewe kufuatana na mipango yetu sio kusukumiziwa mikopo ya kilaghai na kinyonyaji.
Nadhani aliona Noah Nyeusi zinazunguka maeneo ya nyumbani
 
Back
Top Bottom