Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

UJUMBE MKUU WA SPIKA NDUGAI: " NIMEKOSA MIMI , NIMEKOSA MIMI , MIMEKOSA SANA , MUNGU ANISAMEHE ; WATANZANIA NISAMEHENI !"

Mheshimiwa Spika wa Bunge Job Ndugai, leo 03-01-2022 akizungumza na waandishi wa habari, kwenye ukumbi wa Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma muda mfupi uliyopita; ameweza kumwomba msahama Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu mikopo ya nchi. Alisema kwamba “Katika mazungumzo yale baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya watu wakakatakata mambo, wakawasilisha ujumbe nusu, ujumbe nusu ule umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu, ambao mjadala umesababisha usumbufu wa hapa na pale”

Aliendelea kusema “Kwa hiyo niliona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa, hapakuwa na lolote la kukashifu wala kudharau juhudi zozote za Serikali, tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono. Katika mazungumzo yetu niliwataka wenzetu pamoja na mambo mengine tulipe kodi, ushuru na tozo mbalimbali huo ndio ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu”

"Wakati huu mwaka unaishilia hii wiki ya mwisho kabisa niliugua sana, hata sauti bado haijakaa sawa sababu nilikuwa kitandani, namshukuru Mungu nina nafuu kubwa sasa, na wakati nipo kitandani naumwa yakajitokeza mambo mbalimbali,"- Spika Job Ndugai

"Baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya watu wakakata mambo wakawasilisha ujumbe nusu, ambao umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu na kusababisha usumbufu wa hapa na pale; na Hapakuwa na lolote la kudharau juhudi zozote za serikali, serikali ni Baba yetu na Mama yetu, tunahitaji serikali na tunaiunga mkono, na niliwataka wenzangu kujiimarisha kiuchumi, tulipe kodi na tozo huo ndiyo ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu; Likajitokeza jambo la kama vile Spika anapinga mkopo wa serikali wa Trilioni 1.3, hilo binafsi limeniuma sana, kwa sababu kadhaa.’’

Spika Job Nduga alisisisitiza kwamba "Kama nimetoa neno lolote la kumvunja moyo Rais Samia Suhuhu Hassan katika juhudi zake za kuijenga nchi, namuomba radhi sana pamoja na wananchi wote kwa ujumla. "Nimekosa mimi ,Nimekosa mimi ,Mimekosa sana ,Watanzania Nisameheni.

"Nchi imetulia, iko salama katika mikono ya Rais Mama Samia, ni kitu cha kutengeneza tu lakini hakuna ukweli. Wale wote niliowakwanza niwaombe radhi na mimi ni Yule yule. Nimekosa mimi, nimekosa sana. Mungu anisamehe. Watanzania nisameheni sana . Popote pale kama nilivyonukuliwa kuwa nimebeza kazi zinazofanywa na Rais na kuwakwaza wananchi wengine naomba nichukue nafasi hii kusema naomba radhi,sisi tunaongozwa na Ilani ya CCM niseme tu sijawahi kudharau kazi zinazofanywa na Rais wetu na haitokuja kutokea.

Aliendelea spika Ndugai kusema "Serikali ni baba yetu, Serikali ni mama yetu, tunaihitaji Serikali na tunaiunga mkono. Katika mazungumzo yetu niliwataka wenzetu tujiimarishe kiuchumi, tulipe kodi, ushuru, tozo; Hakukuwa na namna nyingine tofauti na serikali, na sikuongea vitu tofauti na hotuba yangu ililenga kuwahamasisha wananchi walipe kodi niliongelea kuhusu kujitegemea na niliongelea wabunge kuhusu kulipa kodi. "Hatukuwa na mazungumzo yote naamini na nakiri mitandao sasa hivi ina nguvu limetokea kuwa eti spika anapinga mkopo uliotolewa jambo hili limeniumiza sana kama spika lakini kwenye jimbo letu pia mkopo huo umeweza kutusaidia.

SPIKA NDUGAI ALISEMA "MITANDAO SIKU HIZI INA NGUVU, INAWEZA IKATENGENEZA AJENDA, IKAPELEKA AJENDA AMBAKO WALA HAIKUWA, NA MJADALA UKAWA NI WA MOTO SANA.
Nikasema,endapo wenzetu mnaona wabunge tulifanya jambo baya kupitisha tozo,basi mtatuhukumu huko mbele. Sikumaanisha taasisi nyingine yoyote. Kufuatia hilo likajitokeza jambo la kama vile Spika anapinga mkopo wa Serikali wa tril 1.3, IMENIUMA MNO HILI.
Kwenye ujumbe wangu, hakukuwa na lolote la kudharau juhudi za serikali, serikali ni baba yetu na mama yetu, tunahitaji serikali na tunaiunga mkono na niliwataka wenzangu kujiimarisha kiuchumi, tulipe kodi na tozo, huo ndiyo ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu.

SISI BUNGE NI SEHEMU YA HIZI FEDHA TSH TRILIONI 1.3, ITAKUWA NI DHAMBI KUBWA KUWAVUNJA NGUVU VIONGOZI WETU. TUMTIE MOYO RAIS WETU, TUMTIE NGUVU.

Spika Ndugai aliongeza kusema “Nchi nzima inafurahia kwa jinsi mkopo huu ulivyokwenda na uwazi wake. Kwa wale wote walioguswa, niwaombe radhi. Niwahakikishie mimi ni yule Yule. Nitakua nimechuma dhambi sana kwa mafanikio haya na kazi ya hawa wanao katakata clip wasitake kumvunja moyo Rais wetu nakutugombanisha naye,Tumtie moyo Rais wetu Samia Suhuhu Hassan kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa siku zote akutukanae hakuchagulii tusi.

“Huko nyuma ndugu zangu mlikuwa mnatengeneza bajeti, lakini mkija mwisho wa mwaka mnakuta zilizotakiwa ziende huku zimezolewa zimepelekwa kule, Wizara fulani ilitakiwa ipate pesa imepata 18% walichotakiwa wapate,Sio safari hii, kila kitu kimekwenda kilivyopangwa. "Haijawahi kutokea fedha nyingi zikaelekezwa kwenye maendeleo ya watu kama katika kipindi hiki cha Mama Samia... Tumepata fedha nyingi mpaka sisi wenyewe tunashangaa... Haijawahi kutekelezeka bajeti smoothly kama mwaka huu. Kila kitu kimekwenda kilivyopangwa.

Neno la msingi spika Ndugai alisisitiza kwamba "Popote pale kama nilivyonukuliwa kuwa nimebeza kazi zinazofanywa na Rais nakuwakwaza wananchi wengine naomba nichukue nafasi hii kusema naomba radhi,sisi tunaongozwa na Ilani ya CCM niseme tu sijawahi kudharau kazi zinazofanywa na Rais wetu na haitokuja kutokea. Na tena alisema "Nipende kuwaambia kamati za Bunge zinakaribia kwahiyo nitumie fursa hii kuwaambia wabunge wajiandae kwaajili ya kamati,sisi hatuna migogoro ni ufundi tu wa watu kutengeneza maneno ambayo hayana maana mitandaoni,wale waliorusha matusi tuwasamehe tuu hawajui walitendalo" na mwisho "Nimekosa mimi ,Nimekosa mimi Mimekosa sana ,Mungu anisamehe Watanzania Nisameheni! ASANTENI SANA.
 
Halafu jambo jingine, nitamshangaa sana ndugai asipojiuzulu.......maana si kwa spana zile alizoshushiwa kutoka kule pande za njombe.....
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990

Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Anatakiwa aitwe na kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ahojiwe kama ilivyokuwa kwa Gwaji Boy, Slaa na Humphrey Slow slow vinginevyo ni utakuwa uonevu kwa akina Gwaji boy endapo Subwoofer hatahojiwa
 
Kuhusu mkopo tufanye ni kweli amenukuliwa vibaya. Na ile ya kusema serikali kufanya kazi zake Dar na kuongeza gharama kwa serikali imekaaje? Hiyo si alienda mbali akasema ukipiga gharama za posho, usafiri zinakua juu? Hadi akahoji nani anasimamia expenditure za serikali?

Hatuko wajinga kiasi hicho wanavyotuchukulia.
 
"Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana"

Tangu kuzaliwa kwangu sijawahi mwungamia binadamu mwenzangu.
Ishu ni ujumbe wake umefika,

Hizo nyingine mbwembwe tu
 
Mama akimsamehe atakuwa amefanya kasa kubwa mno. Ndungai ni nyoka mwenye sumu kali sana anayetafuta timing ya kung'ata
 
Laaana ya kuharibu uchaguzi mkuu inafanya kazi
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990

Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Spika amekuwa mnyonge sana lkn ujumbe wke ulifika na kueleweka tunahitaj katiba mpya tumupungizie madaraka rais na kuwa na mihili uhuru bila kuingiliwa hapo tutapata maendeleo ya kweli na utakuwa mwisho ccm
 
Back
Top Bottom