Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Kuna Wapumbavu wa Sukuma gang humu niliwaambia, kama mlikuwa hamumtaki mama mlikuwa na mambo mawili tu ya kufanya.

1. Mngezuia asiapishwe

2. Kama ameapishwa kuwa Rais mngekiteka Chama kwamba mwenyekiti lazima ashindanishwe kwenye uchaguzi, ungefanyika uchaguzi na Sukuma gang wangeweka mwenyekiti wao ambao Rais lazima acompromise nao.

Yote mawili wameshindwa Samia ndio Rais, ndio Amiri jeshi mkuu na ndio mwenyekiti wa chama.

Ni kichaa peke yake ndio unaweza kupingana na mtu mwenye status hii.

Mama ajiombee afya tu, Mungu akimpa kibali yupo ikulu mpaka 2030 loud n clear.
Watakuwa ni wa kuanzisha uzi kila kukicha ili wapate kuungwa mkono wakidhani hiyo inawasaidia. Kumbe ni kujifariji tu.

Rais ni mtu mkubwa sana hapa Tanzania. Ndio bosi wa kila taasisi.
 
Wewe ni nani hadi nifuate ushauri wako
Cha

Cha kushangaza utarudi hapa kuongea kutokana na alichosema
Kam unajua anachosema na hakuna haja ya wandishi basi teambie weww na kisha usirudi kuchangia maana unajua kila kitu.

Rekebisha kidogo heading ni
"Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana "
Spika kawa mdogo kama piriton!
P
Hatimaye mbabe kapata mbabe wake
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
Ukanyagi katiba unamu"torment". Na bado. They are other evils in offing.
 
Ni kama mlevi,akiutwika akutukaane uhalisia..
Na kesho yake asubuh zikimtoka akuombe radhi...

Sasa kazi kwako ila ujumbe umefika.
 
Kwa lugha ya picha ya Ndugai leo, akili yake iko kwa mwendazake ila tumbo liko kwa mama Samia. Hapa ndipo msongo wa mawazo unapomtesa mh. Spika [emoji16][emoji16]
 
Ndugai kaboa, mbona kaongea ukweli anaomba radhi ya nini?
Anaomba raisi amsamehe sana. Amuonee huruma maana amekosa sana na haikuwa dhamira yake kuleta taharuki bali janja janja tu za watu kutaka kumchafua.

Wewe ulitaka afanyaje? Aache mshahara, rupurupu, aingie kwenye vita na amiri jeshi mkuu?
 
Na Ndio maan TU nataka katibampya Ili kuwe na transparency, separation of powers katika mihimili ya Taifa
 
Ndugai kamtunishia mama msuli, Mama kaupIga kimyaa, Ndungai kaanza kujinyea. UKIMYA WA MAMA UNATISHA
 
Kuombaomba misamaha kwa kosa ambalo hujafanya ni udhaifu mkubwa
 
Huyu jamaa aache uoga, maana tukichekeana hapa tutakuja kupigwa mnada kama alivyosema mwanzo, huwezi kukopa trillion 10 ndani ya miezi 9 kwa miradi isiyo ya kimkakati tena bila idhini ya bunge halafu tukabaki salama, no way!!
 
Back
Top Bottom