Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Huyu mzee haeleweki hata anachoongea, go straight to the point, huwezi kukopa kujenga madarasa na vyoo na ukapiga pasu pesa nyingi zikaenda kuijenga zanzibar ukilinganisha eneo lake na idadi ya watu.........kwa nini viongozi wa nchi hii ni wanafiki sana!?
Toa upumbavu wako hapa,au na wewe toka hadharani uongee haya.
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
Ndugai mhuni Kama wahuni wengine, anaomba msamaha so what
 
Na hapa ndo hoja ya katiba mpya inapopata nguvu, inakuwaje spika wa bunge anaongea kinyonge namna hiyo, anazidiwa hata na kiongozi wa TUCTA......
Duuu
JPEG_20220103_124935_6757002900567553557.jpg
 
Unatuambia ile clip imeeditiwa na wajanja ili wakuchafue na wakugombanishe wewe na serikali alafu muda huohuo unaomba msamaha kwa kuwakwaza watanzani kwa kile ulichoongea kwenye ile ile clip unayodai imeeditiwa.

Duuuh! hatupo siriaz kabisa kwenye mambo ya msingi.

Taifa lina watu na viongozi wa ajabu sana.
 
Rekebisha kidogo heading ni
"Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana "
Spika kawa mdogo kama piriton!
P
In criminal law unlike in Politics, confession is used as an evidence to convict you upon all accusation raised unto you, but in Politics confession is a measure of strength and maturity. As it was said by political gurus, if you lack HONEST, intelligence and Energy looses their meaning
 
In criminal law unlike in Politics, confession is used as an evidence to convict you upon all accusation raised unto you, but in Politics confession is a measure of strength and maturity. As it was said by political gurus, if you lack HONEST, intelligence and Energy looses their meaning
 
Spika Job Ndugai ameungana na watanzania mbalimbali kuukataa uzushi na ghiliba za wapinga maendeleo wanaotamani kuona mhimili wa Bunge ukitofautiana na serikali kuu. Mhe. Spika ameomba radhi dhidi ya usumbufu uliojitokeza kutokana na maudhui yaliyotengenezwa kwa malengo ya kuwapotosha watanzania.

Kama ilivyo kwa maeneo yote nchini, Mhe. Spika Job Ndugai, ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwezesha mkopo unaojenga madarasa ya kisasa nchi nzima ikiwemo Kongwa iliyopata madarasa zaidi ya 100 kwaajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu.

Pamoja na pongezi za Mhe. Spika kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu, huduma nyingine za jamii kama vile Hospitali na miradi ya maji inatekelezwa kwa kasi katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwa upande wa uchumi, hadi kufikia Disemba 2021, ukubwa wa soko la hisa umeongezeka kwa karibu 4.5% kutoka Trilioni 15.4 hadi Trilioni 15.8, ikiwa ni karibu Bilioni 500. Hii imetokana na sera nzuri za uchumi zinazotekelezwa na Rais Samia Suluhu katika kuimarisha uchumi wa nchi.

Aidha, kutokana na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini, ukusanyaji wa mapato umeongezeka kwa kasi, kwa Mwezi Disemba pekee kiasi cha Trilioni 2.51 kimekusanywa na kuandika historia ya fedha nyingi zaidi kwa mwezi tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya mapato nchini(TRA).

Katika kipindi cha mwezi July hadi Disemba 2021, kimekusanywa kiasi cha Shilingi Trilioni 11.1, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Rekodi hii inatoa dira ya ushindi kwa wapenda maendeleo na uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
 
Tuliwaambia BAVICHA wakashindwa kuelewa, Mwenyekiti wa CCM ndio injini kuu ya nchi
Mtu kama Ndugai tukimwambia alete hesabu za pesa za matibabu India anazo? Si mwizi tuu huyo kadanganya serikali.

Rais alishasema atagombea Urais 2025 na lengo ni kuwazima watu dizaini ya kina jobu na wanaowatuma.

They have to shut up their mouth and respect the President.Na PM nae alishasema tunaenda na Samia sasa hao wengine wanaweza shindana na Rais kashika dola,Katiba haimzuii nk?
 
Back
Top Bottom