Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Yani yeye akizani Rais anaweza kuchezewa kama Pasco?

Uspika wa Ndugai unashikiliwa na kadi ya ccm, wakichukuwa kadi yao uspika na ubunge kwishney.

Rais ni jambo lingine kabisa, nadhani leo Humphrey Polepole atakuwa amepata clear msg kwamba wanaokwambia tupo nyuma yako yakikukuta ukigeuka nyuma hutowaona.
Ubunge wenyewe ameupewa na mwendazake kama unavyompa mwanao kitumbua au andazi.
 
Kwa Press hii ya Ndugai tukubaliane kwa pamoja Sukuma gang ndio imezikwa rasmi leo.

Asiyekubali hili hatokuwa na tofauti na kenge mpaka damu zitoke masikioni ndio ataelewa.

R.I.P Sukuma gang mwendo mmeumaliza.
Nakubaliana na wewe 100 %.

Ile statement ya "Nimekosa mimi, nimekosa sana...." ndiyo imeconclude kila kitu.
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
Ifuatiwe na kujiuzulu ndio protocali zilivyo,
Akiendelea kushika nafasi ya uspika maana yake bado anaendelea kumbeza rais na makundi yake
 
Dah mgogo kawa mdogo kama Piriton

Kwani Sukuma gang wanasemaje?

Mama kaupiga mwingi kinoma
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
Ok nimeelewa. Tatizo ni Clip
 
Kawabwaga mchana kweupeeee
Kuna Wapumbavu wa Sukuma gang humu niliwaambia, kama mlikuwa hamumtaki mama mlikuwa na mambo mawili tu ya kufanya.

1. Mngezuia asiapishwe

2. Kama ameapishwa kuwa Rais mngekiteka Chama kwamba mwenyekiti lazima ashindanishwe kwenye uchaguzi, ungefanyika uchaguzi na Sukuma gang wangeweka mwenyekiti wao ambao Rais lazima acompromise nao.

Yote mawili wameshindwa Samia ndio Rais, ndio Amiri jeshi mkuu na ndio mwenyekiti wa chama.

Ni kichaa peke yake ndio unaweza kupingana na mtu mwenye status hii.

Mama ajiombee afya tu, Mungu akimpa kibali yupo ikulu mpaka 2030 loud n clear.
 
Kuna mtu jana alisema RAIS WA TANZANIA ANAWEZA KUAMUA MKEO ACHEPUKE NA AKACHEPUKA.
Rais ana power zile alizokuwanazo Governor enzi za Ukoloni. Enzi zile ilikuwa ni kulinda maslahi ya Ukoloni.

Nyerere alipokua Rais hakutaka mabadiliko ili iwe rahisi kwake kutawala, kumbuka kulikua na mgawanyiko wa makabila na kidini.

Sasa hivi absolute power imebaki kulinda maslahi ya CCM.
 
Kuna mijamaa ilitaka kujenga mnara mrefu ufike kwa Mungu,Mungu akaaamua kuwagonganisha lugha wakaanza kuchanganyana mmoja anaagiza zege mwenzake analeta mbao na mnara haukujengwa hadithi hi inatufundisha Nini ?????
 
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai bwashee
Spika Ndugai amesema kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate uhuru watoto wa wilaya ya Kongwa wanakwenda kusoma katika madarasa ya kisasa kabisa yanayofanana na chumba cha mkutano cha ofisi ya Spika.

Ndugai amesema madarasa yao yana madirisha ya aluminium, chini yana tiles na mabati ni yale ya kijani siyo yale mabati sufuria waliyoezekea shule nyingine.

Spika Ndugai amemshukuru sana Rais Samia kwa maono makubwa aliyonayo.

Source: Ayo tv
 
Back
Top Bottom