Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

dah nimefikia kwenye kipande cha "watanzania nisameheni sana, tuombeane afya irudi vizuri zaidi" mliosikiliza spika wetu ametukosea nini wajameni
 
Huyu mzee haeleweki hata anachoongea, go straight to the point, huwezi kukopa kujenga madarasa na vyoo na ukapiga pasu pesa nyingi zikaenda kuijenga zanzibar ukilinganisha eneo lake na idadi ya watu.........kwa nini viongozi wa nchi hii ni wanafiki sana!?
Mbona TRA ipo zanzibar pia?
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
Nilisema kuwa ataikana Ile clip
 
lipo japo moja serious katika nchi kuna mahala litatulete shida maana tunaishi kinafiki..

TANZANIA KUNA UDINI NA UKABILA MBAYA SANA...
Hakuna udini wala ukabila nchini ila Kuna katiba iliyompa raisi nguvu kubwa. Bishana nae utaelewa.
 
Rekebisha kidogo heading ni
"Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana "
Spika kawa mdogo kama piriton!
P
Alichofanya Ndugai ni kumuongezea nguvu Maza.... Wakati huo huo yeye kajimaliza kabisa. Asifikiri watamsamehe kwa hilo pamoja na kujifanya anajibebesha msalaba wake mwenyewe kwa niaba ya wote.

Imagine pamoja na kutukanwa kote kule kashindwa kumuita mtu yeyote kwenye ile kamati yake ya Maadili. Kwa udhaifu aliouonyesha sasa asubiri watakanyompanda mpaka kichwani.

Mbaya zaidi kutubu hadharani kwa design ile, Spika wa Bunge.... Only in Tanzania.
 
Back
Top Bottom