Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Hapa ni kumsubiri Tundu Lissu arudi ili atusemehe maana Hawa wengine wamechagua upande wa ajira, heshima binafsi na vyeo.
 
Kulikuwa hamna namna zaidi ya hiki anachokifanya leo naona ile mikwara ya asipofika mbele ya kamati ataletwa kwa pingu naye imemkuta akawa hana cha kufanya zaidi ya kuja kulialia na kuomba radhi kwa staili ya mtu mzima, siku nyingine achunge kauli zake
 
Spika amuomba radhi Rais "Nitumie fursa hii kupitia kwenu kumuomba radhi Rais" hayo ni maneno ya Spika akiomba radhi

6D1EE007-F576-4C7C-91F5-65C8264ADD81.jpeg
 
Watu hamtaki kuamini anachosema spika ila mnaamini clip iliyokatwakatwa. Baasi chagueni mnayotaka kuamini😂😂
 
Spika Ndugai amesema kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate uhuru watoto wa wilaya ya Kongwa wanakwenda kusoma katika madarasa ya kisasa kabisa yanayofanana na chumba cha mkutano cha ofisi ya Spika.

Ndugai amesema madarasa yao yana madirisha ya aluminium, chini yana tiles na mabati ni yale ya kijani siyo yale mabati sufuria waliyoezekea shule nyingine.

Spika Ndugai amemshukuru sana Rais Samia kwa maono makubwa aliyonayo.

Source: Ayo tv
 
Back
Top Bottom