Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Kaole kwenye ubora wao..
 
nimemsikiliza ikabidi nibadili channel,haeleweki,mara aseme amenukuliwa vibaya,mara aseme ni maneno ya mitandaoni ,mara aombe msamaha yani haeleweki huyo mzee
mara akarubishe wandishi wa habari dodoma kwa kuwa Rais kaidhinisha,mara atake kusema Rais ndio atakuwa mgeni rasmi ila anarukia tena mada nyingine
 
Amesifia mkopo wa sh. 1.3T, wakati mwanzoni aliuponda, sio bure mzee mzima katishwa
 
Hili ni swali muhimu sana.
Je ameomba radhi ya dhati aukatishwa?
alikuwa anaumwa na pengine alipotoka.
Je amehofia maisha yake?Je ameamua kujificha ili asidhirike ?Je ametishiwa ?
.Ndugai pamoja na uzuzu wake ametishwa kama vile alivyotishwa comrade Nape enzi zile na Pole pole awamu hii ya 6. Wote wamenywea kama puto
 
Ndugai hana uwezo nje ya madaraka, ameomba msamaha maana anaogopa kudhalilika kimaisha. Alikuwa na kiburi cha madaraka enzi za Magufuli, lakini hana chochote kimaisha baada ya kuona anaweza vuliwa madaraka huku akiwa na kundi kubwa linalomchukia.
 
Mi najiuliza ametishwa na chama au katishwa na Serikali, yeye kama kiongozi wa Mhimili nilitarajia asimamie msimamo wake, zaidi sana atoe ufafanuzi lakini sio kuomba msamaha maana kazi ya Bunge ni kusimamia Serikali.
 
Alichofanya Ndugai ni kumuongezea nguvu Maza.... Wakati huo huo yeye kajimaliza kabisa. Asifikiri watamsamehe kwa hilo pamoja na kujifanya anajibebesha msalaba wake mwenyewe kwa niaba ya wote.

Imagine pamoja na kutukanwa kote kule kashindwa kumuita mtu yeyote kwenye ile kamati yake ya Maadili. Kwa udhaifu aliouonyesha sasa asubiri watakanyompanda mpaka kichwani.

Mbaya zaidi kutubu hadharani kwa design ile, Spika wa Bunge.... Only in Tanzania.
God is sovereign....Nchi lazima ilindwe, acheni uchonganishi...Hakuna mkubwa mbele ya Tanzania hata huyo individual mnayempa power...Lazima kuwe na centre of power; ni hilo tu...Tanzania lazima ishinde na individuals lazima washindwe....Mungu ibariki nchi yangu Tanzania
 
Na hapa ndo hoja ya katiba mpya inapopata nguvu, inakuwaje spika wa bunge anaongea kinyonge namna hiyo, anazidiwa hata na kiongozi wa TUCTA......
Wewe ulitaka nchi ivurugike? Mbona mna penda ubinafsi hivyo?
 
Baada ya matamko kutoka viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali dhidi ya kauli ya Spika Job Ndugai kuhusu mikopo, leo Jumatatu saa 5:00 asubuhi, Ndugai anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli yake aliyoitoa Desemba 26, 2021 alipoalikwa kwenye tukio la makumbusho ya wagogo kuwa imechukuliwa vibaya na kuleta mkanganyiko

Amesema alikuwa anazungumza kuhusu sababu iliyoifanya bunge kukubali na kuipitisha tozo na sio kuwa alikuwa akizungumzia taasisi nyingine yoyote

Ndugai amesema video iliyosambaa ilikatwa bila kuleta ujumbe kamili aliokuwa amekusudia. Ameumia kuonekana anapinga mkopo wa serikali

NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho yake ili wanaotembelea ofisi hizo wajue historia ya bunge kwa namna ilivyokuwa

Jambo hilo amesema ni muhimu hata kwa taasisi nyingine kuwa na makumbusho yake ili watu waweze kujua kuhusu historia ya taasisi husika

Amesema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi za Bunge Dodoma

NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

Amesema yeye ni CCM ambao lengo lao ni moja hawawezi kutofautiana. Kuna watu wanaojaribu kuwafarakanisha lakini hawatafanikiwa

Ndugai amesema Rais anafanya vizuri lakini peke yake hawezi kwa hiyo ni jukumu la watu wote kumsaidia
View attachment 2066990
View attachment 2067070
Pia soma;
Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni
Mwanzo Ndugai alikuwa sawa kuikoromea serikali iache kuchukua mikopo isiyoeleweka kwa kuwa yeye ni kiongozi wa mhimili wa kuisimamia serikali, lakini Cha ajabu mhimili wa kuisimamia serikali ameugeuza kuwa mhimili wa kuinyenyekea serikali eti "Nimekosa Mimi, Nimekosa sana! Hii ni sala ya toba ya Kikatoliki wakiomba toba kwa Mwenyezi Mungu, Ndugai toba hiyo kaipeleka kwa Rais kulinda tumbo lake!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mama akimsamehe atakuwa amefanya kasa kubwa mno. Ndungai ni nyoka mwenye sumu kali sana anayetafuta timing ya kung'ata
Acheni uchonganishi...Nchi siyo NGO au SACOSS...Nchi inahitaji umoja, amani na utulivu kuliko hizi drama zenu
 
Leo Spika wa Bunge letu LA JMT Mh Job Ndugai ameongea na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali ya kibunge na mengineyo.

Moja kubwa lililowagusa wananchi ni kitendo chake cha kumuomba radhi Mh Rais Samia na watanzania wote kwa ujumla kutokana na sintofahamu iliyojitokeza ya kusambaa taarifa mitandaoni za kumkosoa Mh Rais kwa kile alichokiita "Nchi Kuuzwa kwa madeni"

Mm binafsi Nampongeza Mh Spika Ndugai kwa ukomavu wake wa kukiri makosa na kuomba msamaha kwa hilo.

Kuomba msamaha ni jambo dogo sana ila sio wote wanaoweza kufanya hivyo.kuomba msamaha ni kitendo cha kiungwana miongoni mwa waungwana iwe umekosea kweli or hujakosea.

Spika umeonyesha Utanzania wetu ulivyo kwa vitendo.Hongera sana.huu ndio Utanzania tuliorithishwa na wakubwa zetu waliotangulia.

Hapa katikati tulipitia maisha tamaduni na mazoea ya nchi zingine ambazo kimsingi tuliozoea Utanzania wetu tulikuwa tukipata tabu kuenenda na utamaduni Mpya ambao hatukuuzoea.

Watanzania utamaduni wetu ni Kukaa mezani kumaliza tofauti zetu na siku zote anaekubali kushindwa ndie mshindi.kuomba radhi na kukubali kubeba lawama iwe umehusika na kosa unalotuhumiwa nalo or hapana hii ndio sifa ya kiongozi mwenye busara.

Kuna wajinga wengi tu wanakukebehi na kukukejeli kwa kitendo chako cha kuomba radhi,naomba nikutie moyo kwamba tupo sisi ambao tunafikiri nje ya hizo dhihaka na kuona mantiki ya ulichokifanya kwa mustakali mwema wa nchi yetu.

Umeonyesha unazo sifa za kuwa kiongozi mwema,mzuri na unaeweza kubeba mizigo ya watu wengine kwa maslahi mapana ya watu wako.Hongera sana Mh Spika Ndugai.

Miaka ya Nyuma kidogo kwenye miaka ya 1980 Rais mstaafu wa awamu ya Pili Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi,aliwajibika kubeba mzigo wa watu wengine alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani kwa kujiuzulu nafasi yake kwa makosa yaliyofanywa na watu wa chini yake.

Inahitaji ukomavu wa hali juu,Uwajibikaji,Busara na hekima kuweza kubeba na kuzikubali "dhambi" hadharani na kuomba msamaha hadharani.kwangu mm hili ni jambo LA kishujaa kwa kiongozi mkubwa kaliba ya Spika wetu.

Huu ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine, kiongozi sio malaika nae ni binadamu kama binadamu wengine hivyo kukosea ni jambo LA kawaida iwe kwa kujua or kutojua.So kitendo cha kuomba msamaha kinaonyesha na kuthibitisha ubinadamu alionao kiongozi.

Nina mengi ya kuzungumzia Ushujaa huu ila naomba niishie hapa, Hongera Mh Spika Ndugai.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom