Spika Ndugai: Vijana wa Tanzania hawaaminiki, wakiachiwa biashara bila kuiba wanajiona wajinga


MK254 tusaidie kumuuliza Spika,imekuwaje na yeye ametumia zaidi ya Bilioni 30 kwenye matibabu? Au alienda kutibiwa sayari ya Mars? Hivi akiachiwa nchi na yeye si ataifilisi?
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Tanzania kuna tatizo la vijana kutokuwa waaminifu.

Katika maelezo yake kiongozi huyo wa Bunge amesema, “tunalo tatizo katika nchi yetu la ujumla wake la uaminifu, sasa sijui hili tutalifanyaje wawekezaji wengi wamekuwa wakilalamikia uaminifu hasa wa vijana Watanzania, ikishawekwa mradi basi vijana uaminifu unakua mdogo.”

“Atajikuta mtu amefilisika tu asipoangalia yaani eneo hili sijui dawa yake ni nini lakini basi waheshimiwa wabunge watakapokua wanachangia ni moja ya eneo la kulitazama kiwango cha uaminifu ni kikubwa kwa kiasi gani.”

Amewataka viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kuhubiri kuhusu uaminifu, akitaka jambo hilo kufanyika shuleni na hata wazazi majumbani.

“...,na kijana akiwa na fursa kama hiyo akaachiwa asimamie biashara asikuibie wenzake mtaani watasema mjinga sana yule alipewa goli lipo wazi akaliacha mjinga kweli jamaa mwaka mzima yupo bungeni kule wala hasimami yeye kakaa tu unaona sasa yaani hilo, lakini uaminifu unalipa sana katika maisha.”

“Ukiaminiwa katika kidogo anayekuamini anaweza kukuamini katika kikubwa zaidi na akakuamini katika kikubwa zaidi na zaidi na wewe ukawa ni sehemu ya mafanikio makubwa zaidi,” amesisitiza.
 
Wao Wanasiasa na watumishi wa umma ndiyo waliolifikisha Taifa hapo lilipo. Wao wanaona ni sawa kuiibia serikali halafu siyo sawa kuibiwa.
 
Ukweli maisha yamekuwa magumu sana,kiasi kwamba vujana wengi wanakosa uaminifu kwa sasa hata biashara tuu wengi wamekuwa madalali,iwe kazi,iwe chumba cha kupanga,shamba ni balaa!
 
Mie nadhani ccm ndo wametufikisha hapa..mnakaa huko kusign mamikataba ya ajabu mnapiga hela wananchi hatupati huduma stahiki unadhan wasipopata gape wasipige? Msituchoshe..mtuache kula yetu tu shida...tena mtukome
 
Ndio spika mjinga kuliko maspika wote duniani plus spika mwenye marukanga
 
Atueleze bilioni 30 alizutumiaje kwenye matibabu?
Kwani mkikaa kimya bila ku comment mtachekwa?

Kila kitu mko kinyume, mna matatizo gani?

Kuna vingine mnakaa kimya kama Mmeshindwa kukisapoti.
 
Like sons like father's,hata wao ni wezi,wizi wao umeanzia mbali tangu wakiwa vijana,hata hawa wazee waleo,walikuwa vijana jana,walikuwa vibaka tangu kipindi hicho.sasa wamekomaa
 
Mie nadhani ccm ndo wametufikisha hapa..mnakaa huko kusign mamikataba ya ajabu mnapiga hela wananchi hatupati huduma stahiki unadhan wasipopata gape wasipige? Msituchoshe..mtuache kula yetu tu shida...tena mtukome
TETESI..
kuna uwezekano nkapewa u DG bandari
Mjiandae [emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
Kwani mkikaa kimya bila ku comment mtachekwa?

Kila kitu mko kinyume, mna matatizo gani?

Kuna vingine mnakaa kimya kama Mmeshindwa kukisapoti.

Na yeye Ndugai akikaa kimya kuna tatizo? Kama yeye ametumia bil 30 kwa matibabu je akikabidhiwa nchi(hazina) si ataifilisi? Au nyani haoni LENDUKU?
 
Kama yeye ni spika wa hovyo hovyo anatazamia vijana watakuwaje? Ukitaka kumulika njia, anzia miguuni?
 
Ndugai ana hasira na chuki sana kwa Vijana sababu Vijana ndio tupo mitandaoni tukimpa makavu yake,tunamalizia file la Mke wake hapa ndio atajua anaopambana nao ni Vijana wa kisasa wenye akili kuliko yeye.
 
Mgogo huyu aliupataje uspika!!! mbona hoja zake ni za kipuuzi mno. Hivyo jitu lenye uwezo duni huu wa kufikiri alistahili vipi kutumia takribani Tshs. 30 bilion za walipa kodi huko India wakati hana tija yeyote kwa taifa !!!!!?!!.
 
Itakuwa kuna vijana wake wame mliza visenti kadhaa sasa akaona aje a generalize

Wanaiga kwa baba zao!!! Baba zao kwa vile ni wezi wanaona kuiba ni jambo la kawaida tu; hawajui kuwa tabia hiyo inaweza kuharibu maisha yao huko mbele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…