Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

Doh!! kumbe mbunge analipwa posho ya 240,000/- kwa siku (sawa na mshahara wa walimu weeengi kwa mwezi)
Hamnaga ata cha maana wanafanyaga maana nchi inaenda kwa mawazo ya mwenyenchi.
 
Hili bunge Ni genge LA kulipana pesa kihuni.unawalipaje watu kabla ya wakati? Pengine mapesa mengi wanajichotea tu.spika kwa kikao laki tano, kwa wiki 2 kashakunja milioni 7 duh
 
Vifo vya wabunge bado sio tiket yakuondoa watu bungeni!! Kama ni watu waliostahili kukimbia basi ni manesi lakini ndio wanaoshinda na wagonjwa kwa kuendekea na majukum yao japo wao ndo wako kwenye hatari zaidi!!! Mkuu ebu jaribu kuliangalia upande mwingine sio hko ulipoelekea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko serious kweli? Hao manesi hujasikia wanavyowakimbia wagonjwa? Na kwa mawazo yako manesi wanaohudumia wale wanaohisiwa kuwa wameambukizwa COVID 19 wafanye hivyo bila kupewa vifaa vya kujilinda kwa sababu tuu ni kazi yao? Wewe ndio unaopaswa kuangalia upande wa pili. Spika angewahikikishia kuwa hakuna hatari ya kuambukizwa huo ugonjwa kwa kuchukua hatua za kuwapikia wabunge na wafanya kazi wote wa Bunge angeeleweka. Tukumbuke kuwa huu ugonjwa unaambukizwa kirahisi sana kwa hiyo mtu kujiweka katika nafasi ya kuambukiza ni kuwatia hatarini watu wote walio karibu na wewe. Uamuzi unatakiwa uwe wa mbunge anaehusiks, sio kwa watu wengine kumlazimisha.
Amandla...
 
Mtu si anatakiwa kutoa maelezo ya matumizi ya per diem? Na kama mtu hajahudhuria vikao lakini yuko Dodoma utamkataje per diem yake? Ni utaratibu wa kawaida na palikuwa hamna haja ya kutangazia umma.

Amandla....
Kwani wanaenda kikazi au kulala hotelini? Usipoenda kaziini ina maana hauko dodoma kinachojulisha spika kuwa uko dodoma Ni.daftari la mahudhurio kazini bungeni
 
ndugai kajivua nguo..,ameonyesha kuwa huwa wanalipana kabla ya kazi...

inamaana hata wabunge waliofariki walikuwa na madeni pia maana wamefariki huku wakiwa wamelipwa pesa amabayo hawajaitendea kazi.

kweli Bunge letu ni dhaifu na kituko machoni pa wale wenye ubongo.
IMG_5835.JPG



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ukiangalia Bunge liko tupu. Sio wa Chadema peke yao ambao hawapo. Alitakiwa kusema wale wote ambao hawahudhurii vikao wanatakiwa kurudisha posho za vikao. Kwa jinsi alivyozungumza amewalenga waliojiweka karantini peke yao. Hiyo sio haki na ni dalili ya kutaka kukomoana na kuchafuana.
Mtu akilipwa kimakosa au isivyo stahili yake, anayetakiwa kuwadai ni Accounting Officer na sio Speaker.
Btw. Hata kama una kibali cha kutokuwa Bungeni bado haustahili kulipwa posho ya vikao. Kwa hali inavyoonekana ni wengi mno ambao wanatakiwa kurudisha pesa.

Amandla.....
Kwa Tangazo LA ndugai Leo nimegundua bunge Ni kichaka cha wizi.je hela waliyopewa kina mahige, ndasa Na rwakatare itarudi? Unalipaje wabunge posho ya kikao kabla ya vikao? Hili bunge lilipaswa kukaguliwa Ni wizi mtupuu
 
Wapiga kura tuko njia panda huku tumeambiwa wabunge watoro waliojiweka kwenye karantini ndani ya saa ishirini na nne wawe Dodoma halafu tukaskia tena warudishe fedha na wakapimwe kama hawana virusi vya corona ndio watakanyaga bungeni!! Hatuja kaa sawa mwingine kakamatwa na na bunduki 16 na risasi mia tano !! Naona kama mzee Ndugai sasa anachanganyikiwa ashugulike na jangili au watoro?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri hoja nikwamba wamelipwa pesa kwa kazi ambayo hawafainyi hivyo wairudishe.
Ni jambo rahisi Kama Mtu kalipwa kwa kazi ambayo hajaifanya anarudisha fedha sioni tatizo kwa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wabunge wa Chadema waliamua kukaa karantini kwa muda wa siku 14 na baada ya hapo wanaweza kuendelea na vikao vya Bunge. Kwa kuwa Bunge bado litaendelea na vikao vyake hata baada ya muda wa malipo yaliyokwisha fanywa kwao nadhani wanaweza kufidia kwa siku unless kama wataamua kutoendelea na vikao vyote.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapiga kura tuko njia panda huku tumeambiwa wabunge watoro waliojiweka kwenye karantini ndani ya saa ishirini na nne wawe Dodoma halafu tukaskia tena warudishe fedha na wakapimwe kama hawana virusi vya corona ndo watakanyaga bungeni !! Hatuja kaa sawa mwingine kakamatwa na na bunduki 16 na riaasi mia tano !! Naona kama mzes ndugai sasa anachanganyikiwa ashugulike na jangili au watoro???

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu wa Bunduki 16 na risasi 500 ni mwenzetu au wa kwao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jangili pia 2018 alikwepo kwenye list ya wabunge watoro ,alikuwa hahudhurii bunge .

Watoro watajirekebisha tuhangaike na jangili kwa sasa
 
Mliwalipaje inadvance?

Ndugai anapaswa kujiuzulu kwa uzembe!
Ndugai kapwaya unamlipaje mtu posho hajafanya kazi? Kwa minajili hiyo kuna mawaziri nao wamelipwa posho hawapo bungeni wapo ziarani mikoani wanakula posho za wizara hii si ni double payment ya posho?
 
Back
Top Bottom