Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

Spika Ndugai: Wabunge watoro warejeshe fedha zote walizolipwa kuanzia Mei 1-17 jumla ya Tsh. Milioni 110

Wabunge wote Wa CCM kipindi cha Magufuli ambao walikuwa wakichukua posho za bunge za per diem na za vikao nk siku zote ambazo hawakuhudhuria bila kibali cha spika warudishe pesa zote na majina yao yakatwe wasigombee tena wanakula bure pesa za walipa kodi na ni wizi
 
Wabunge wote Wa CCM kipindi cha Magufuli ambao walikuwa wakichukua posho za bunge za per diem na za vikao nk siku zote ambazo hawakuhudhuria bila kibali cha spika warudishe pesa zote na majina yao yakatwe wasigombee tenawanakula bure pesa za walipa kodibna ni wizi
Naunga mkono hoja!
 
Wabunge wote Wa CCM kipindi cha Magufuli ambao walikuwa wakichukua posho za bunge za per diem na za vikao nk siku zote ambazo hawakuhudhuria bila kibali cha spika warudishe pesa zote na majina yao yakatwe wasigombee tenawanakula bure pesa za walipa kodi na ni wizi
Hawa ni wale waliogawana pesa za katiba mpya bila ya kufanya kazi.
 
Wabunge wote Wa CCM kipindi cha Magufuli ambao walikuwa wakichukua posho za bunge za per diem na za vikao nk siku zote ambazo hawakuhudhuria bila kibali cha spika warudishe pesa zote na majina yao yakatwe wasigombee tenawanakula bure pesa za walipa kodi na ni wizi
Leta orodha mbwiga wee
 
Na walio kufa warudishe
Adjustments.JPG



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unajua kwamba anayetakiwa kufanya hiyo kazi ni kichaa anayetumwa na kichaa ili kuongoza vichaa wanaoshangawa na wasio vichaa?
 
🔬CHADEMA kimemjibu Spika Ndugai kwa kumuambia kuwa kama anataka Wabunge warudi Bungeni wakiwa wamepima, basi aseme anataka wakapime wapi kwa kuwa Serikali imepoteza imani na Maabara yake na inaichunguza, na kuongeza kuwa yeye ndiye Spika wa kwanza kulipa posho kwa Mbunge hewa.
 
Tunawasikiliza Wabunge wanaojadili bajeti ya Wananchi bungeni

Hao waliokimbia bunge tutawajibu October
 
Nimemsikia kwa ufupi Sana, Speaker kwamba warudi bungeni wakiwa na certificate zinazoonyesha wako clean na Corona.

Nikawazaaaaaa,

Bado nawaza Na kutafakari Ila sipati majibu kabisa aisee.

Tusubirie Kama viinua mgongo vya watu havita potea hapa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunawasikiliza Wabunge wanaojadili bajeti ya Wananchi bungeni

Hao waliokimbia bunge tutawajibu October
Bajeti ya wananchi baada ya miaka 60 ya uhuru watoto wanakaa chini mashuleni?
Wengi hawajui kusoma na kuandika?

Mmenyima bunge live?
Mnapeana sumu hapo LUMUMBA NK
UMEKALIA KUANDIKA UMBEA NA UJINGA TU KUDHIHIRISHA WIZI WAKO WA MITIHANI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani bungeni, Mheshimiwa Mbowe, aliwaagiza wabunge wa Chama chake wasusie Bunge kushinikiza Bunge liwekwe kwenye 'lockdown' kwa ajili ya corona. Baadhi ya wabunge wake walitii agizo hilo, baada ya kuwa wamekwishapata posho ya kuhudhuria Bunge. Hivyo, Spika amekuja na agizo kwamba wote wanaosusia Bunge, warudishe masurufu waliyopewa kwa siku ambazo hawakuhudhuria vikao. Hili limezua mjadala, 'for and against'.

Nina maoni kadhaa katika suala hili.

Mheshimiwa Mbowe ana hoja ya msingi. Ubaya wake ni jinsi alivyoitoa. Alipaswa kuwasilisha Bungeni muswada wa dharura kuomba kusitisha shughuli za Bunge. Bunge lingejadili muswada huo kwa kulinganisha manufaa na madhara yatakayotokana na hatua hiyo. Upande unaoafiki watasema hatua hiyo itathibiti kuenea kwa ugonjwa. Wanaopinga watasema madhara kiuchumi na kijamii ni makubwa zaidi kuliko manufaa yatakayopatikana, kwani mpaka sasa ueneaji wa ugonjwa siyo mkubwa sana. Muhimu, watu kufuata tu masharti yanayoelekezwa na Serikali, kama kuvaa barakoa, kutosongamana kwa watu wengi, n.k. Aidha, wanaopinga muswada wataleta hoja kwamba Bunge liko ukingoni mwa muda wake na linabidi kukamilisha shughuli zake kabla ya kuvunjwa, kupisha uchaguzi mwishoni mwa mwaka. La sivyo, huenda ikalazimika kuahirisha uchaguzi, kitu ambacho sidhani kama upinzani watakipenda.

Zote hizo ni hoja nzuri (za kuunga mkono na za kupinga) na zinastahili kujadiliwa. Bunge lingezijadili na kufikia uamuzi. La muhimu ni kwamba kitu kinachoamuliwa ndicho hicho kiwe. Ninaamini kama Bunge lingeamua kusitisha shughuli baada ya kujadili hoja za pande zote mbili, Spika asingesita kusitisha Bunge. Kama hoja ya Mbowe ikishindwa, upinzani ingebidi watii maoni ya wengi, na hiyo ndiyo demokrasia. Siyo kwa sababu tu maoni yako hayakukubalika basi unaamua kufanya utakavyo, hata kama ufanyacho kinakinzana na maoni ya wengi.

Badala ya kupeleka muswada wa dharura, Mbowe alikwenda kwenye vyombo vya habari na kutolea huko maoni/maamuzi yake na kuwaagiza wabunge wa chama chake wasitishe kuhudhuria vikao vya Bunge. Hili halikumpendeza Spika na akaamuru wabunge wote wasiohudhuria vikao warudishe posho waliyopewa kwa siku ambazo hawakuwa bungeni.

Uamuzi huu nakubaliana nao kwa asilimia 100. Unapewa posho ya kuhudhuria vikao. Kama hukuhudhuria kikao, hustahili kulipwa posho. Kuna wachangiaji humu ambao walionyesha kushangaa kwa nini posho ilitolewa kabla ya vikao kufanyika. Hakuna la ajabu hapo. Mfanyakazi yo yote anaposafiri kwenda kikazi nje ya kituo chake cha kazi, hukadiria atakaa huko siku ngapi, malazi ni kiasi gani kwa siku, na vivyo hivyo kwa chakula. Hesabu zinapigwa na anapewa masurufu kulingana na hesabu hizo. Unategemea mtu huyu alipiaje malazi na matumizi mengine ya kujikimu akiwa huko nje ya kituo chake cha kazi kama hukumpa hela 'in advance'? Akirudi ana-'retire imprest' aliyopewa kwa kutoa vielelezo jinsi alivyotumia masurufu aliyopewa. Hela ambayo hawezi kuitolea maelezo inabidi kuirudisha. Hiki ndicho kinachofanyika kwa maofisi yote, likiwemo Bunge. Bunge linapangwa kuchukua siku kadhaa na posho ya mbunge ni kiasi fulani kwa siku. Hivyo mbunge anapewa posho hiyo 'in advance' kama 'imprest'. Hakuna cha ajabu hapo. kwa kuwa wabunge wa Chadema walihudhuria vikao kwa baadhi tu ya siku zilizopangwa, ile posho ya siku ambazo hawakuhudhuria inabidi irudishwe. Period.

Tatizo lilitokana na Mheshimiwa Mbowe kutumia njia zisizo za kiofisi (vyombo vya habari) kueleza mawazo yake. Kama hatua aliyochukua ilikuwa kwa ajili tu ya kuhofia afya ya wabunge, na si kwa kujipatia sifa za kisiasa, hawezi kuona shida kurudisha hayo masurufu ya siku alizokosekana bungeni. In fact angejizolea sifa sana kama angerudisha posho hiyo kabla hata Spika hajasema hivyo. Watu tungeelewa kwamba kweli mtu huyu amechomwa moyoni na hoja yake kiasi kwamba yuko radhi hata kurudisha posho yake. Sasa unasusia vikao lakini posho unaing'ang'ania. Kwa misemo ya wahenga: 'Baniani mbaya lakini kiatu chake dawa'; au 'Kigeugeu na kisebusebu papo'.
 
Wakina Mbowe&Co wameenda kujificha huko makwao sababu ya Corona kama mkulu alivyojifungia kule kwao.

PLAIN.
 
Hakuna kitu kama hicho kwenye malipo ya namna hiyo.
Hapo mwenyemakosa ni mlipaji.
Usitetee wizi.kama CDM wabunge n waungwana warudishe hela waliyolipwa

Kifuatacho utasikia wamekamatwa kwa wizi wamepelekwa mahakamani na wamekosa sifa ya kugombea ubunge
 
Usitetee wizi.kama CDM wabunge n waungwana warudishe hela waliyolipwa

Kifuatacho utasikia wamekamatwa kwa wizi wamepelekwa mahakamani na wamekosa sifa ya kugombea ubunge
Unajua maana ya neno mwizi wewe? Embu eleza wameibaje
 
Unajua maana ya neno mwizi wewe? Embu eleza wameibaje
Wizi wao kuaminiwa nao hauufahamu?

Mfano mzuri wa wizi wa kuaminiwa n kama huo wa wabunge wa CDM.Walipwa posho ya kuhudhuria bunge kwa 14 days na hawajaingia bungeni kwa kisingizio cha Corona kwa namna nyingine wametorok kazini

Kifuatacho n kugunguliwa mashtaka kwa wizi wa kuaminiwa pamoja na kutolipwa mshahara wa mwezi wa Tano kama watashindwa kutoa sababu yenye Massimo ya wao kutohudhuria bunge na mwisho wa siku kupitia hiyo kesi watakosa hata sifa ya kugombea ubunge na ndio unakuwa mwisho rasmi wa CDM

Hapo bado hujaelewa? Shindana na Serikali ukiwa una hoja ya msingi lakini ukiijaribu serkali kwaajili ya political milage you are likely to be a looser
 
Wizi wao kuaminiwa nao hauufahamu?

Mfano mzuri wa wizi wa kuaminiwa n kama huo wa wabunge wa CDM.Walipwa posho ya kuhudhuria bunge kwa 14 days na hawajaingia bungeni kwa kisingizio cha Corona kwa namna nyingine wametorok kazini

Kifuatacho n kugunguliwa mashtaka kwa wizi wa kuaminiwa pamoja na kutolipwa mshahara wa mwezi wa Tano kama watashindwa kutoa sababu yenye Massimo ya wao kutohudhuria bunge na mwisho wa siku kupitia hiyo kesi watakosa hata sifa ya kugombea ubunge na ndio unakuwa mwisho rasmi wa CDM

Hapo bado hujaelewa? Shindana na Serikali ukiwa una hoja ya msingi lakini ukiijaribu serkali kwaajili ya political milage you are likely to be a looser

ulisema wizi sasa unasema wizi wa kuaminiwa , hivyo ni vitu viwili tofauti,
hayo ni masuala ya kiutumishi zaidi , huwezi kuingiza criminality ya wizi kwenye ishu kama hiyo kwa namna yeyote ile.

ninavyofaamu mimi wamelipwa posho ya kujikimu kuwawezesha kuishi dodoma .
Watu wanalazimisha eti wapo dsm unauhakika kwamba hao wabunge wapo dsm kweli?
Mbunge anaweza kufika dodoma akapata dharura ya ugonjwa hivyo akashindwa kuhudhuria vikao

Nashangaa spika anakurupuka eti warudishe posho.
Spika hajawa mstaarabu, kiutumishi ikiwa mtumishi hajaja kazini akakutaarifu hata kwa simu kwamba anaumwa, kiustaarabu unatakiwa kumsubiri hadi atakaporudi toka matibabu ndio umshurutise akupe report ya daktari inayoeleza kuhusu ugonjwa wake pamoja na idhini ya dakatari iliyomuelekeza apate mapumziko na kama akishindwa hivyo ndio unaweza kumchukulia hatua ikiwemo kutakiwa kurudisha posho au kukatwa mashahara, ila sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom