Nilikuwa naenda kulala kitandao nikaona mada hii , bora nichangie kabla sijasahau pengine kesho nikawa na ratiba ngumu kidogo za kufanya kazi
alichojaribu kutetea mh cheyo ni sahihi , tena wengine wale wabunge wanaotoka karibu na north mara walitakiwa ndio wawe wakwanza kutoa kilio chao bungeni , wanancho wa kule walitakiwa wawe wakwanza kutoa kilio chao hata kukifikisha katika vyombo vya kimataifa kwa matatizo yanayotokana na sehemu ile .
Wiki 2 zilizopita tuliona nchini nigeria kampuni ya shell imelipa watu fulani karibu dola mil 15 kwa hasara walizopata watu hao za kimazingira kutokana na utendaji wa kampuni ya shell walifikisha swala mahakamani na wakashinda kesi wakalipwa fidia kubwa sijui nchi yetu inajifunza nini kutokana na kile kinachoendelea
mfano mwingine ni ule wa nile delta huko huko nigeria wale waasi wa eneo lile wanapigania haki zao za kupata maendeleo pamoja na mazingira yanayoharibiwa kutokana na uzalishaji wa mafuta bila wao wazawa wa eneo lile kufaidika na chochote sasa hivi eneo lile ni kuwindana tu .
Juzi hapa tumesikia wapiganaji wa mau mau kenya wakienda kuishitaki serikali ya kikoloni kwa mambo waliyoyafanya miaka karibu 50 iliyopita , subiri tusikie kesi yao itakuwaje hata ikichukuwa miaka 100 wana nafasi kubwa zaidi ya kushinda .
..
Kwa serikali ya tanzania na watanzania wanatakiwa wajue kuna mambo karibu 3 ya kuyaweka akilini kutokana na sakata hili sasa hivi .
1 ) mradi wa north mara ambao sumu yake unaingia katika ardhi pamoja na mito ya karibu na eneo hilo hili ni kesi tena kubwa waziri anayeshugulikia afya na mazingira anatakiwa atoe ufafanuzi wa hili haraka
2 ) kuna viwanda vya bia na viwanda vingine vinavyomwaga maji ziwa viktoria , tunakumbuka maradi wa ziwa viktoria kupeleka maji mikoa jirani kama shinyanga --- yale maji yanayoingiwa ziwani yameathirika kwa kiasi kikubwa , bado watu wetu wananyweshwa na kupelekewa kwa kiasi kikubwa watu wanashangilia mradi wa maji bila kuangalia athari zake za muda mrefu .