Spika Sitta amtimua nje Cheyo (UDP) Bungeni kwa kubishana naye!

Spika Sitta amtimua nje Cheyo (UDP) Bungeni kwa kubishana naye!

suala la watu kuathirika ni very serious na hata juzi tumeona watu wameretwa kwa matibabu...hata Mh. Ndugai na Charles mwera kwa hili wameungana na kutaka tume iundwe...cheyo alikuwa anaongea kwa kuguswa na suala lile halafu Spika yeye analeta udikteta na kumfukuza mbunge ndani ya kikao....jamani tunaweka maslahi gani mbele kama sio uhai wa mtu....
naungana na wachangiaji wengine kuandaa mwisho wa suala hili la udikteta wa CCM sio tu Sitta...KATAA CCM..OKOA TAIFA..
 
spika anakuwa dictator.. ni wazi kuwa waziri hakutoa maelezo mazuri kuhusu mgodi wa north mara na spika anajibu hoja kwani yeye waziri....? waziri mwenyewe anatumia maelezo ya Barick kujibu hoja...kwa vyovyote Barick hawezi toa maelezo yanayo mgandamiza
 
Matokeo yatakuwa hayahaya. Cheyo naye ndivyo anavyoiendesha UDP yake.

Kwa hiyo ni sawa Sitta amdhalilishe eti kwa sababu anaiendesha UDP kibabe? Kama Cheyo ni chizi basi na Sitta anatakiwa awe chizi? No plse. Hakuna sababu ya msingi kwa mtu mzima kufanya maamuzi ya kitoto kama aliyoya fanya Spika Sitta, mtu anayeongoza muhimili muhimu katika nchi yetu.
 
Hili bunge la Tanzania mwaka huu kuna vituko napata wasiwasi hadi huu mkutano wa bajeti uishe watatwangana mangumi, maana kila mtu anataka ajijengee jina jimboni mwake.

Mungu linusuru bunge letu,
 
Huyu aliwahi kuchapwa Viboko na Mwalimu Nyerere na Pia wakati ule pale Mlimani kwa utomvu wa Nidhamu leo yeye anasema kuwa mwezake hawana nidhamu jamaani
 
Hili bunge la Tanzania mwaka huu kuna vituko napata wasiwasi hadi huu mkutano wa bajeti uishe watatwangana mangumi, maana kila mtu anataka ajijengee jina jimboni mwake.

Mungu linusuru bunge letu,

Inabidi ngumi zipigwe bungeni, kwa sababu kwa kauli za Sita kama zingenikuta mimi ningeamka na kwenda kumpiga Sita ngumi moja nzito na kisha ndio nitoke nje. Hatuwezi kufokeana Bungeni kama watoto wadogo, kama swali limeshindwa kujibiwa, Inatakiwa waziri husika aseme na sio kuleteana ubabe usio na maana.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MINGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kwa hiyo ni sawa Sitta amdhalilishe eti kwa sababu anaiendesha UDP kibabe? Kama Cheyo ni chizi basi na Sitta anatakiwa awe chizi? No plse. Hakuna sababu ya msingi kwa mtu mzima kufanya maamuzi ya kitoto kama aliyoya fanya Spika Sitta, mtu anayeongoza muhimili muhimu katika nchi yetu.
Taratibu na KANUNI zinazoliendesha Bunge wengi hatuzifahamu. Kama Spika Sitta kakosea atabamizwa na wengi tu. Ana "MAADUI" wengi mle Bungeni.
 
Huyu aliwahi kuchapwa Viboko na Mwalimu Nyerere na Pia wakati ule pale Mlimani kwa utomvu wa Nidhamu leo yeye anasema kuwa mwezake hawana nidhamu jamaani

Hii kali. kwikwi kwidi kwidi heheheheh ahahahahhhaaahaha

Ina maana Chuo Kikuu zamani walikuwa wanachapwa? Pia mie nakumbuka enzi hizo mkuu wa chuo cha mlimani alikuwa Rais sasa ina maana alikuwa na mamlaka ya kuchapa wanachuo wanakwenda kinyume na taratibu? naomba unipe hii kwa undani. Ila nimecheka sana maana sipati picha kama kweli Mh. Sitta alishawahi kucharazwa "mboko" tena akiwa level ya chuo kikuu
 
Hii ni Hatari sana kwa Taifa letu hata Mazingira yetu na pia kuna ajenda ya siri kati ya North Mara na Serikali, Hivyo Wataalamu wetu wako Wapi, Kumbukeni yake mabaki ya meli ya Kifaransa iliyotupa kule Sierra Leoni jinsi walivyolipa Fidia, Kuna haja ya waziri kuondoka katika nafasi yake
 
Aliwahi kuchapwa Viboko na Mwalimu Nyerere kwa kufanya maandamano na kudai haki yao wao na wakti ule hata Yoweri Mseveni, Leo naye anageuka na kuwa kama hawa, Alishawahi kufukuzwa hata Chuo na kwa msamaha wa Mw Nyerere ndio akarudi Chuo na Kumaliza LLB yake
 
Ni kweli kabisa spika Sita alichapwa viboko na Nyerere kwa maswala ya migomo Mlimani...huyu tokea enzi hizo alikuwa ana utovu wa nidhamu mnategemea ukubwani atabadilika kweli?
 
Aliwahi kuchapwa Viboko na Mwalimu Nyerere kwa kufanya maandamano na kudai haki yao wao na wakti ule hata Yoweri Mseveni, Leo naye anageuka na kuwa kama hawa, Alishawahi kufukuzwa hata Chuo na kwa msamaha wa Mw Nyerere ndio akarudi Chuo na Kumaliza LLB yake

hahahahahhhhahahahaha. haki ya mungu kumbeeeeee
 
hahahahahhhhahahahaha. haki ya mungu kumbeeeeee

Nyie mnategemea mna spika hapo? Na mwl mzee Julius aliiiapa huyu Sita hata shika uongozi wowote labda yeye afe. Si mmeona ameanza kuibuka gafla baada ya mzee Julius kufariki. huyu hakuna kitu mle.
 
Hivi spika hasa anatakiwa awe na elimu ya masuala gani? maana kama kuna uwezekano angeandaliwa muda huu ili 2010 apatikane?
 
Awe najua hata Sheria, lakini kuwa na elimu ya Chuo Kikuu kwake ni faida kubwa sana ni sheria, maana hata miongozo yake huwa inatafisiriwa na sheria, Hivi kumbe nyinyi mnategemea atabalika kama sio ubabe ule ule enzi zile za UDSM, Hivi ndio Hulka yake ya Ubabe na Ndio Spika wa Viwango vipya, Naombeni ile kauli yake ya SITA(...........)
 
Siamini kuwa Spika aliuliza kama jamaa ni CHEMISTRY! Anasingiziwa.

Amandla......

Swali la kwanza toka kwa spika (la kijinga of course) aliuliza --Kwani acid haiunguzi mara moja! --Hapa akijaribu kumuzuia Cheyo asieleze kwamba ni matokeo ya matatizo yaliyoanza siku nyingi.

Swali la pili akauliza kama maelezo ya Cheyo ni ya Kisayansi. Ndo Cheyo akajitaja yeye ni mkemia. ---

Tusipoteze muda kujiuliza kama hayo yalisemwa na Sita au la. Ukiona yaliyotokea, hutataniki kumwita Sita jina la '*****'
 
Jamani Serikali iwaokoe wananchi huko Northmara wanateketea kwa kemikali si muafaka kubishana kuhusu hilo kwa sasa.
 
Na hata Spika naye ana makosa kibao huyu waziri anayehusika au vipi nduguzangu
 
Kwa hili Spika Sitta yupo sahihi kabisa. Bunge linaendeshwa kwa kanuni na taratibu zake kile sio kijiwe cha kahawa watu wanakuja kupiga soga.

Spika anaposimama kuongea ki kanuni mbunge au msemaji mwingine anatakiwa akae chini. Kitendo cha Mh Cheyo kuendelea kusimama na kutaka kuongea na hatimae kuchukua makabrasha yake na kutoka nje ni uvunjaji wa kanuni. Iukumbukwe na izingatiwe Mh Cheyo kaanza kutoka kabla hata ya kuombiwa atoke kwa kifupi alizira, hivyo Sitta alikuwa sahihi kabisa kumtimua na pengine kumpa adhabu kubwa zaidi ya hiyo.

Kama mna chuki zenu na Mh Sitta tafuteni mahala pengine pa kuzitolea kwenye hili mmenoa!
 
Back
Top Bottom