Spika Tulia Ackson: Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali, aeleza kuhusu kurejea kwa Bunge LIVE!

Wanaweza kwebda mahakamani kupinga kufukuzwa kwao, kwa sababu Baraza la Chadema halijakaa ambalo ndicho chombo cha mwisho kuidhinisha kufukuzwa kwao, ambapo maamuzi hutolewa baada ya wao kuitwa ili wajitetee. Kwa hiyo wakienda mahakamani kupingwa kufukuzwa kwao kwa vile hawajaitwa na Baraza Kuu kujitetea wataendelea kuwa wabunge hadi mahakama itakapotoa hukumu, na inawezekana mahakama ikajatoa hukumu 2025 ambapo watakuwa wameshamaliza kipindi chao cha miaka 5 na kupewa kiinua mgongo!
 
Nani kahoji hili suala maana lilishafungwa. Bunge lilizinduliwa 2020, leo ni 2022- bado tu watu wanahoji? Au walidhani kwa vile Ndugai katoka basi huyu Tulia atakuja na kupindua meza. haiwezekani! Jamani, huu ni msimu wa masika tujikite kwenye kilimo, suala la akina Mdee kutoka au kutotoka halitakuongezeeni mkate kwenye familia zenu! Twende mashambani kujiandalia chakula chetu kwa msimu huu na ujao, mambo ya bungeni wachaneni nayo!
 
Binafsi naona waachwe waendelee, nao wale mema ya nchi. Maana tukitafuta uhalali wa wabunge mule ndani wanaweza wasifike 50. Wengi ni kazi haramu ya mwendazake! Huu ulimwengu wa tatu ni changamoto sana.


YESU NI BWANA.
Mkuu umeongea Sanaa. Nimekuelewa mno mkuu! Kumbe umeenda ndani zaidi kujua wote namna walivyoweza kuingia mle ndani. Sawa
 
CHADEMA haiwatambui sijui anataka mchakato wa chama gani?
Mkuu, mi naona yupo sahihi. Walikata rufaa huko kwenye chama chao, rufaa yao haijasikilizwa mpaka leo. Na sina shaka, hao CD 19 hii kesi ya Mbowe, ina faida kubwa sana kwao. Kwani, kuendelea kwa Mbowe kuwa ndani, ndiko kunako sababisha rufaa yao kutosikilizwa. Nina uhakika, kwa MAZINGIRA ya sasa, wakitupwa nje tu na chama chao, na huko Bungeni wataondolewa. Pia, nina imani Tulia huyu, sio yule wa MWENDAZAKE! Hata hiyo picha, kanawili kwa muda mfupi!
 
Total rubbish, wewe ukihukumia kifungo miaka 4 jela ukakata rufaa hutatumikia kifungo chako mpaka rufaa yako isikilizwe?
 
sasa si waende huko mahakamani kwa mujibu wa katiba ya chadema wameshafukuzwa uanachama na wamekata rufaa baraza kuu,
Hawa hadi sasa sio wanachama wa chadema
Huu ni uvunjwaji wa katiba ulio zahiri
Huyu bi msumali anajifurahisha
 
sasa si waende huko mahakamani kwa mujibu wa katiba ya chadema wameshafukuzwa uanachama na wamekata rufaa baraza kuu,
Hawa hadi sasa sio wanachama wa chadema
Huu ni uvunjwaji wa katiba ulio zahiri
Huyu bi msumali anajifurahisha
Walipelekwa na CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…