Spika Tulia ameshindwa kujibu maswali badala yake kaongea vitu ambavyo hajaulizwa kwa kupanic na mhemko

Spika Tulia ameshindwa kujibu maswali badala yake kaongea vitu ambavyo hajaulizwa kwa kupanic na mhemko

si kweli gentleman,
unapotosha. Kajibu maswali ya wabunge wenye mihemko sana kwa ufasaha mno na ameongea kimamlaka na kuwaambia ukweli wabunge kwamba wasifikiri alikotoka bado wako chini ya wakoloni na hahitaji ruhusa kutembelea Ukraine wala Russian kwa mapenzi bali ni utaratibu na wajibu wa bunge hilo kufanya hivyo kote ulimwenguni 🐒
Mkuu mambo ya kudhani anatoka nchi maskini, colonized yametoka wapi? Kwanini anatembea na mentalitu hii?

Watu wengi sana wanaenda Ulaya kufanya kazi na shughuli zingine hatimaye huwa hawafikii malengo kwa sababu kama hizi za Dr Tulia.

Akiona wazungu wamekusanyika wanakula ana hisi wanamtenga kwa sababunyeye ni Mwafrika wakati hawakumzuia. Vitu vidogo kama kula tu vinamtoa kwenye reli.
 
wale hawajatishika isipokuwa mshangao na hawatakuja chagua mjinga wanamna yake Toka afrika....
walidhani Dr Tulia ni mnyoooonge,

na watanyoroshwa mpaka wanyooke na mihemko yake.

Eti who told you to visit Russia? 🤣
mihemko ni kitu cha kijinga sana dah 🤣
 
Mkuu mambo ya kudhani anatoka nchi maskini, colonized yametoka wapi? Kwanini anatembea na mentalitu hii?

Watu wengi sana wanaenda Ulaya kufanya kazi na shughuli zingine hatimaye huwa hawafikii malengo kwa sababu kama hizi za Dr Tulia.

Akiona wazungu wamekusanyika wanakula ana hisi wanamtenga kwa sababunyeye ni Mwafrika wakati hawakumzuia. Vitu vidogo kama kula tu vinamtoa kwenye reli.
eti who told you to visit Russia?🤣

kwamba Dr Tulia alihitaji ruhusa ya huyo mbunge wa Ukraine mwenye mihemko sio 🤣
 
eti who told you to visit Russia?🤣

kwamba Dr Tulia alihitaji ruhusa ya huyo mbunge wa Ukraine mwenye mihemko sio 🤣
Sasa alitakiwa ajibu. Na sio kuongea vitu ambavyo havipo.

Swali la Mzungu la Who Told you to vist Russia ni swali pana mno na ni gumu pia.
 
si kweli gentleman,
unapotosha. Kajibu maswali ya wabunge wenye mihemko sana kwa ufasaha mno na ameongea kimamlaka na kuwaambia ukweli wabunge kwamba wasifikiri alikotoka bado wako chini ya wakoloni na hahitaji ruhusa kutembelea Ukraine wala Russian kwa mapenzi bali ni utaratibu na wajibu wa bunge hilo kufanya hivyo kote ulimwenguni 🐒
Kwani hawakujua kwamba hamko chini ya ukoloni? Hakukua na mantiki yoyote ya kuhusisha ukoloni na alipotoka katika kujibu maswali! Unaulizwa kwa nini ulienda anasema waliandika barua, kuna faida gani anafoka kwamba tuliwajulisha kwa barua, kwa nini hukwenda Ukraine kwanza anajibu Zelensky hakuwepo, nknk hapo swali gani kajibu sasa au uchawa tu unatukereketa labda tupate pia tafsiri ya ras simba
 
Naona wewe ndiyo umepanic.
Sikiliza clips zote na uzielewe.
Kapanic sana mama palikua hakuna haja ya kuanza kupayuka ohoo mara you should treat me with dignity,Kwan kuuliziwa mashwali ndo kunaonyesha wamekudharau? Kwan angejibu vizur na kuwaumbua Kwa majib mazur si angeonekana yupo vzur?? Sasa anaongea as if hataki maswali ,kama vile anataka meza zigongwe na kumsifia muda wote!!
 
Kwa sisi linguists na sychologists tathmini yetu ni kuwa spika alikasirika bila kukasirishwa akidhani wanamdharau.


Siku ilivyokuwa kuanzia dakika ya mwanzo Rais akiwakaribisha wabunge wa kikao cha 149 mwaka 2024

Mkutano wa 149 wa IPU uliofanyika Geneva, Uswisi, tarehe 13-17 Oktoba 2024.

Bunge linaanza kwa Rais Dr. Tulia Ackson akifungua kikao na kusema dunia nzima inatutizama na inatutegemea kuhusu amani dunia na jumuiko letu leo linaneba jukumu zito kuja na azimio kuhusu amani :


View: https://m.youtube.com/watch?v=T5jXc99xYI8

Maswali na majibu : Mashirika yote ya kisheria ya IPU, (Governing Council) Baraza la Uongozi, Kamati za Kudumu, Kamati za Haki za Kibinadamu za Wabunge na Maswali ya Mashariki ya Kati hoja za wabunge kutoka UAE, Kuwait, Ukraine, Russia, Turkey kususia mjumbe wa Israel ....majibu ya Rais Dr. Tulia Ackson... kuhusu mambo mbalimbali yaliyoibuliwa na wabunge n.k n.k
 
Ukiacha ushabiki na mihemko ya uchawa ukweli ni kuwa spika ameshindwa kujibu moja kwa moja maswali aliyoulizwa badala yake aka[anoc na kuhemka na kuanza kunibu maswali kwa maswali badala ya majibu.

Hakukuwa na haja ya kuunda dhana zisizo kuwepo kwamba wanaomuuliza kwamba labda wanamdharau au kunafikra za kikoloni au wanadhani kwakuwa anatoka nchi ya chini kabisa hivuo hawezi kuongoza nk.

Spika kajibu na kuongea vitu vingi visivyokuwa na maana kuonesha kuwa anauwezo na kwamba waulizaji wanamdharau.

Yeye alitakiwa kutoa ufafanuzi wa moja kwa moja kukingana na swali na siyo kuanza kulalama na kufoka. Kwa sisi linguists na sychologists tathmini yetu ni kuwa spika alikasirika bila kukasirishwa akidhani wanamdharau.

Spika tayari alikuwa na inferiority complex akataka kuwaonesha kuwa yeye ni strong wakati waulizaji hawakutaka na hawakuwa na mawazo havyo. Spika ajitahidi kuwa mtulivu na kuto kujibu kwa makelele kulalamika na kufoka lile siyo bunge la CCM kama alivyozoea kuwafurusha akina Mpina.

Wengi wanaomsifia ni kuwa hawana uelewa wao ni kama mashabiki wa Simba na Yangu they are not analytical.

Pia soma
- Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin
Elewa mjadala ule kwa kina sio kuishia kupingapinga tu kila jambo. Kaulizwa kwanini kaipa kipaumbele Russia ambaye ni mtuhumiwa akiiacha Ukraine ambayo ni mhanga.

Akajibu kwamba alifuata mialiko kwenda Russia pia Ukraine katika kipindi kile Rais Zelensky na Spika wake walikuwa wamealikwa kwenye kikao cha NATO huko USA hivyo asingeweza kuonana nao wawili kwa sababu asingemkuta mgeni/wageni wake pale Ukraine.

Pia akasema kuonana na Russia ni katika kutafuta suluhisho la mgogoro huo huo wa Ukraine, alikwenda kumfikishia ujumbe Putin juu ya mateso wanayokutana nayo raia wa Ukraine.

Hapakuwa na tofauti yoyote iwapo angeanza kwanza kuonana na Zelensky kisha akamalizia na Putin au kinyume chake.

Pia tupunguze huu 'uchawa' kwa taasisi za kizungu, tupunguze hii hulka ya kilofa ya kujiona hatuwezi katika kila suala.

Hii huwa ni hulka yenye kuwarahisishia kazi ya kututawala wazungu na taasisi zao. Hata wakoloni walitutawala kiurahisi kwa sababu walitukuta tayari tunazo tabia za kutopendana sisi kwa sisi, wakaanzisha sera ya wagawanye ili uwatawale.
 
Kwani hawakujua kwamba hamko chini ya ukoloni? Hakukua na mantiki yoyote ya kuhusisha ukoloni na alipotoka katika kujibu maswali! Unauliwa kwa nini ulienda anasema waliandika barua, kuna faida gani anafoka kwamba tuliwajulisha kwa barua, kwa nini hukwenda Ukraine kwanza anajibu Zelensky hakuwepo, nknk hapo swali gani kajibu sasa au uchawa tu unatukereketa labda tupate pia tafsiri ya ras simba
Ras Simba pale Magomeni Mapipa.
 
IPU sio kama lile Bunge letu la Dodoma. Huko lazima anyukwe maswali na ajiandae kikao cha pili maana wamekwisha mjua ni mtu wa emotions na lazima wamchokoze huko mbeleni
 
Back
Top Bottom