Spika Tulia, umetuaibisha Wanyakyusa kupitisha Mkataba wa Bandari. Jisahihishe haraka

CONSISTENCY

Senior Member
Joined
Feb 16, 2023
Posts
135
Reaction score
309
Spika wa Bunge Dr Tulia Mwansasu umetuaibisha na kutushushia heshima wanyakyusa wenzako kwa kitendo chako cha kukubali kutumika na kupitisha mkataba wa kitapeli wa bandari.

Unatufahamu wanyakyusa hatutaki ujinga kwenye mambo ya msingi, umepewa dhamana kubwa ya kuendesha chombo kikubwa katika nchi (Bunge) ila nasikitika kusema kwamba umetusaliti wanyakyusa kwa kukubali na kuutetea huo mkataba wa kitapeli wa bandari.

Utafanya wananchi watushushe heshima wanyakyusa kwa kutotupa nafasi nyingine kubwa ya kiuongozi katika nchi kwa sababu yako.

Tulia nakukumbusha kuna mambo ya kufanya siasa na utani lakini sio kufanya siasa na utani kwa jambo muhimu kama bandari, katika hili usipojisahihisha haraka hatutokuacha salama.

Umeshusha heshima kubwa waliyoiweka wazee wetu kina Mwandosya, Mwamunyange, Mwang'onda, Mwakibolwa n.k n.k kwenye utumishi wao wenye uadilifu katika nchi na uzalendo wao.

Kumbuka 2025 utakuja Mbeya kuomba kura kutetea ubunge wako, ila usipokataa au kurekebisha huo mkataba wa kitapeli wa bandari na sisi tutakukataa mapema.

Tumekutumia ujumbe kupitia wakili Boniface Mwabukusi ili akuoneshe taratibu na tamaduni zetu wanyakyusa, najua umemuona akikupa ujumbe kwenye hiyo video katika mtandao wa youtube, kama haujiona hiyo video nakusihi nenda kaangalie.

Unaomda wa kujisahihisha, wewe ni binti yetu tunakupenda na ndio maana tunakupa huu ujumbe wako kwa heshima yako na pia kutunza heshima ya wanyakyusa na nchi kwa ujumla.

Achana na huo mkataba wa kutaka kuuza nchi kwa kigezo cha uwekezaji, kumbuka Rungwe (Tukuyu) ni ardhi takatifu ukiendelea na huo mkataba wa bandari hautotakiwa kukanyaga Tukuyu milele.
 
Spika wa Bunge Dr Tulia Mwansasu umetuaibisha na kutushushia heshima wanyakyusa wenzako kwa kitendo chako cha kukubali kutumika na kupitisha mkataba wa kitapeli wa bandari.

Unatufahamu wanyakyusa hatutaki ujinga kwenye mambo ya msingi, umepewa dhamana kubwa ya kuendesha chombo kikubwa katika nchi (Bunge) ila nasikitika kusema kwamba umetusaliti wanyakyusa kwa kukubali na kuutetea huo mkataba wa kitapeli wa bandari.

Utafanya wananchi watushushe heshima wanyakyusa kwa kutotupa nafasi nyingine kubwa ya kiuongozi katika nchi kwa sababu yako.

Tulia nakukumbusha kuna mambo ya kufanya siasa na utani lakini sio kufanya siasa na utani kwa jambo muhimu kama bandari, katika hili usipojisahihisha haraka hatutokuacha salama.

Umeshusha heshima kubwa waliyoiweka wazee wetu kina Mwandosya, Mwamunyange, Mwang'onda, Mwakibolwa n.k n.k kwenye utumishi wao wenye uadilifu katika nchi na uzalendo wao.

Kumbuka 2025 utakuja Mbeya kuomba kura kutetea ubunge wako, ila usipokataa au kurekebisha huo mkataba wa kitapeli wa bandari na sisi tutakutaa mapema.

Mwenyewe nimefurahi kuona yake makabila ya Tanzania yaliyoelimika mapema pia yamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi mapana ya Taifa waziwazi katika sakata hili la bandari.
1. Mwabukusi
2. Tibaijuka
3. Bagonza
4. Mbowe
5. Kitima
 
Migodi,gesi,viwanda nk mbona hampigi kelele. Mkapa aliuza uza vitu kibao lakini mkikuwa komya, mtupishe hapa mmeanza kuleta udini pumbavu kweli.
Ukiuanzisha moto ujue na kuuzima anzisheni tu mkafikiri mtabaki salama.
Tutasema tu, hatuwezi kubaki kimya kwa mikataba ya hovyo.
 
Mwenyewe nimefurahi kuona yake makabila ya Tanzania yaliyoelimika mapema pia yamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi mapana ya Taifa waziwazi katika sakata hili la bandari.
1. Mwabukusi
2. Tibaijuka
3. Bagonza
4. Mbowe
5. Kitima
Pimbi wewe hayo ni makabila
 
Migodi,gesi,viwanda nk mbona hampigi kelele. Mkapa aliuza uza vitu kibao lakini mkikuwa komya, mtupishe hapa mmeanza kuleta udini pumbavu kweli.
Ukiuanzisha moto ujue na kuuzima anzisheni tu mkafikiri mtabaki salama.

Kwa hiyo Mkapa alikuwa Mnyakyusa, angalia Mwandishi amejikita kwenye uzalilishaji wa jamii yake, sasa hapa Mkapa anaingiaje?
 
Spika wa Bunge Dr Tulia Mwansasu umetuaibisha na kutushushia heshima wanyakyusa wenzako kwa kitendo chako cha kukubali kutumika na kupitisha mkataba wa kitapeli wa bandari.

Unatufahamu wanyakyusa hatutaki ujinga kwenye mambo ya msingi, umepewa dhamana kubwa ya kuendesha chombo kikubwa katika nchi (Bunge) ila nasikitika kusema kwamba umetusaliti wanyakyusa kwa kukubali na kuutetea huo mkataba wa kitapeli wa bandari.

Utafanya wananchi watushushe heshima wanyakyusa kwa kutotupa nafasi nyingine kubwa ya kiuongozi katika nchi kwa sababu yako.

Tulia nakukumbusha kuna mambo ya kufanya siasa na utani lakini sio kufanya siasa na utani kwa jambo muhimu kama bandari, katika hili usipojisahihisha haraka hatutokuacha salama.

Umeshusha heshima kubwa waliyoiweka wazee wetu kina Mwandosya, Mwamunyange, Mwang'onda, Mwakibolwa n.k n.k kwenye utumishi wao wenye uadilifu katika nchi na uzalendo wao.

Kumbuka 2025 utakuja Mbeya kuomba kura kutetea ubunge wako, ila usipokataa au kurekebisha huo mkataba wa kitapeli wa bandari na sisi tutakutaa mapema.

Tumekutumia ujumbe kupitia wakili Boniface Mwabukusi ili akuoneshe taratibu na tamaduni zetu wanyakyusa, najua umemuona akikupa ujumbe kwenye hiyo video katika mtandao wa youtube, kama haujiona hiyo video nakusihi nenda kaangalie.

Unaomda wa kujisahihisha, wewe ni binti yetu tunakupenda na ndio maana tunakupa huu ujumbe wako kwa heshima yako na pia kutunza heshima ya wanyakyusa na nchi kwa ujumla.

Achana na huo mkataba wa kutaka kuuza nchi kwa kigezo cha uwekezaji, kumbuka Rungwe (Tukuyu) ni ardhi takatifu ukiendelea na huo mkataba wa bandari hautotakiwa kukanyaga Tukuyu milele.
Huyu spika hafai kabisa!
 
sawa ajisahihishe ila sio kigezo kiwe unyakyusa acha ukabila mkuu 🤣
 
Kumbe. Nyie shemeji zetu akina "" Mwakinani" mnajua tu kupika matoke!!!! Imbombo nghafu
ametudhalilisha sana wanyakyusa,
hakuna mnyakyusa anaweza kukubali jambo la ajabu kama lile la mkataba wa bandari kisa tu cheo.
 
Mwenyewe nimefurahi kuona yake makabila ya Tanzania yaliyoelimika mapema pia yamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi mapana ya Taifa waziwazi katika sakata hili la bandari.
1. Mwabukusi
2. Tibaijuka
3. Bagonza
4. Mbowe
5. Kitima
ndugu inabidi tupaze sauti kadiri iwezekanavyo ili huo mkataba wa kitapeli kuhusu bandari usitishwe
 
Hili suala halitaisha leo wala kesho na lazima Samia atambue. Huu MKATABA haufai na mbovu kuliko ubovu wenyewe!"
mkataba unasema Tanzania itaijulisha Dubai juu ya fursa zozote zilizopo, na zitakazokuwepo, hili ni tusi kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
upo sahihi ndugu mshana,
ule mkataba una uhaini ndani yake pia una tudhalilisha sana watanzania.
spika tulia ni mshenzi sana, yani akaanza kushambulia wabunge waliokua wanaupinga ule mkataba kwa nguvu kubwa ya kiti chake,
inasikitisha kuwa na spika kama yule.
 
Back
Top Bottom