Spika Tulia, umetuaibisha Wanyakyusa kupitisha Mkataba wa Bandari. Jisahihishe haraka

Spika Tulia, umetuaibisha Wanyakyusa kupitisha Mkataba wa Bandari. Jisahihishe haraka

Spika wa Bunge Dr Tulia Mwansasu umetuaibisha na kutushushia heshima wanyakyusa wenzako kwa kitendo chako cha kukubali kutumika na kupitisha mkataba wa kitapeli wa bandari.

Unatufahamu wanyakyusa hatutaki ujinga kwenye mambo ya msingi, umepewa dhamana kubwa ya kuendesha chombo kikubwa katika nchi (Bunge) ila nasikitika kusema kwamba umetusaliti wanyakyusa kwa kukubali na kuutetea huo mkataba wa kitapeli wa bandari.

Utafanya wananchi watushushe heshima wanyakyusa kwa kutotupa nafasi nyingine kubwa ya kiuongozi katika nchi kwa sababu yako.

Tulia nakukumbusha kuna mambo ya kufanya siasa na utani lakini sio kufanya siasa na utani kwa jambo muhimu kama bandari, katika hili usipojisahihisha haraka hatutokuacha salama.

Umeshusha heshima kubwa waliyoiweka wazee wetu kina Mwandosya, Mwamunyange, Mwang'onda, Mwakibolwa n.k n.k kwenye utumishi wao wenye uadilifu katika nchi na uzalendo wao.

Kumbuka 2025 utakuja Mbeya kuomba kura kutetea ubunge wako, ila usipokataa au kurekebisha huo mkataba wa kitapeli wa bandari na sisi tutakukataa mapema.

Tumekutumia ujumbe kupitia wakili Boniface Mwabukusi ili akuoneshe taratibu na tamaduni zetu wanyakyusa, najua umemuona akikupa ujumbe kwenye hiyo video katika mtandao wa youtube, kama haujiona hiyo video nakusihi nenda kaangalie.

Unaomda wa kujisahihisha, wewe ni binti yetu tunakupenda na ndio maana tunakupa huu ujumbe wako kwa heshima yako na pia kutunza heshima ya wanyakyusa na nchi kwa ujumla.

Achana na huo mkataba wa kutaka kuuza nchi kwa kigezo cha uwekezaji, kumbuka Rungwe (Tukuyu) ni ardhi takatifu ukiendelea na huo mkataba wa bandari hautotakiwa kukanyaga Tukuyu milele.
Bora hata Uspika kama ilikuwa lazima uende Mbeya wangempa Dk. Harrison Mwakyembe
 
Huyu tulia kazaliwa na kukulia Bulyaga Tukuyu Rungwe amemaliza darasa la saba shule ya msingi Mabonde ....leo hii kapata nafasi anawasaliti wanyakyusa walomlea akakua na kufika hapo alipo

Ajitafakari.
 
Huyu tulia kazaliwa na kukulia Bulyaga Tukuyu Rungwe amemaliza darasa la saba shule ya msingi Mabonde ....leo hii kapata nafasi anawasaliti wanyakyusa walomlea akakua na kufika hapo alipo

Ajitafakari.
Nenda tukuyu kamseme tulia vibaya uone, TULIA TRUST FUND imewasaidia sana wana tukuyu kiuchumi
 
Back
Top Bottom