Spika wa Bunge, Job Ndugai anamuomba Rais aitishe Kikao cha Wanaume tu

Spika wa Bunge, Job Ndugai anamuomba Rais aitishe Kikao cha Wanaume tu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Alhamis, bungeni Dodoma, amemwomba Rais wa Tanzania, Suluhu Samia kuitisha Kikao Maalum cha Wanaume pekee ili kuwawezesha kujadilia masuala mbalimbali yanayowahusu. “tunaomba Rais aite mkutano wa wanaume tu.”

Nini Maoni yako?
 
Agenda zetu ni zipi ?

1- Wanaume tunanyanyasika sana. Mke akiwa na kipato, chake ni chake na cha mume ndio cha wote🤣

2- Kunyimwa unyumba ni huzuni kwa kweliii

3- Sisi wanaume watumishi halafu tukaoa wake watumishi wenzetu, siku tukistaafu wake zetu ambao bado ni watumishi wanakataa kuhudumia familia wala kulipia watoto ada ambao bado wanasoma. Tunateseka saana. Ni huzuni

3- Kwa kweli sisi wanaume wenye kazi tukipunguzwa kazi, wake zetu wanatunyanyasa sana. Hapo usiombe wao wapate kazi, tunapata tabu sanaaaaa

4- Sisi wenye michepuko, tunachukua hadi mikopo kuwasaidia michepuko kujenga nyumba kwa nia njema kabisa ila nyumba zikiisha tunafukuzwa kama mbwa. Ni huzuni kwa kweli....

Sisi wanaume tunakufa na maumivu kwa ndani ya "rohoniiii"

Ngoma ya kusindikiza kikao:

🎶🎶Wanaume tumeumbwa Matesooo, matesoooo, kuhangaika 🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶
 
Spika vipi? Mwanamke amekutana na wanawake wenzake, mlishachelewa! Mlikuwa na nafasi ya kuomba tangu awamu ya kwanza hadi awamu ya tano kumwomba mwanaume mwenzenu (rais wakati huo) kukutana na wanaume wenzake!

Hamkuona kama kuna haja hiyo, sasa mnalazimisha mama akutane na mababa!! Kisa eti kwa kuwa mama amekutana na wamama wenzake!! Huo ni wivu sampuli mpya, wivu wa kiume!!!
 
Sidhani kama kunaweza kuwa na mjadala wenye tija labda kusikiliza hotuba yake.
 
Tuachane na Mambo ya Gender, Ni muda wa kujikita Kwenye uhalisia wa Kimaisha. Hizi Agenda Mfu za wanawake or wanaume Hazitaliokoa Taifa ili. Let us concentrates with pertinent issues in our Nation.
 
Imagine Taifa lina agenda kubwa na ngumu za kujadili halafu takataka inachomoza pua yake na kuongea upupu kama huu!Nikisema kuwa Tanzania ina laana kuna watu huwa hawanielewi lakini hizi ndiyo shahidi zenyewe.
 
Tuachane na Mambo ya Gender, Ni muda wa kujikita Kwenye uhalisia wa Kimaisha. Hizi Agenda Mfu za wanawake or wanaume Hazitaliokoa Taifa ili. Let us concentrates with pertinent issues in our Nation.
Au labda spika ameongea kiutani tu maana tushamzoea. Kama ameongea seriously basi ameongea upumbavu wa hali ya juu sana!
 
Au labda spika ameongea kiutani tu maana tushamzoea. Kama ameongea seriously basi ameongea upumbavu wa hali ya juu sana!
Kuna utani gani Kwenye Mambo ya Kimsingi, Hakuwa anatania Maana lile ni Bunge sio Kijiwe cha Kahawa. Huyu Speaker wetu Hajui hizo dakika alizompatia huyu Mbuge na yeye Kuongezea Upupu ni Matumizi Mabaya ya Kodi zetu. Tunae speaker wa ajabu sana.. Daah!!!!
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Alhamisi, bungeni Dodoma, amemwomba Rais wa Tanzania, Suluhu Samia , kuitisha kikao maalum cha wanaume pekee ili kuwawezesha kujadilia masuala mbalimbali yanayowahusu. “tunaomba Rais aite mkutano wa wanaume tu.”

Nini Maoni yako??
Kikao hicho kitahudhuriwa na wanaume warefu na wenye utimamu wa akili sifa ambazo yeye hana
 
Back
Top Bottom