Spika wa Bunge Tulia Ackson anashangaa kwanini hadi leo polisi bado inamshikilia Kada wa CHADEMA Kombo Mbwana

Hangaya alisema anasomaga
hii habari ingeandikwa kiudaku udaku angeisoma na kutolea maamuzi.
 
Kwa hili bunge la kijinga hakuna kitu kitafanyika
 
Yale yalee ya magu kuja kutulalamikia wananchi na kutamani angekuwa IGP! Nchi ina mazingaombwe hiiπŸ™†β€β™€οΈπŸ™†β€β™€οΈπŸ™†β€β™€οΈ
Ya Magu yanazungumzika.

Point yake alikuwa akiwashangaa Polisi kukosa meno, ulimaanisha uwajibikaji dhaifu wa Polisi.

Hali ilivyokuwa wakati ule, ndivyo imejirudia sasa.

Hapo katikati Polisi waliituliza nchi, majambazi wale wa kutumia silaha za moto na za ncha kali walianza 'kukamatwa harakaharaka' na bahati mbaya majambazi wote walifia njiani wakikimbizwa hospitali, hadi nchi ikapoa.
 
Hajaminywa vizuri nini? Kwanini hajatoka?

Mpaka kieleweke.
 
Spika Dr Tulia PhD alikuwa UNGA

Nadhani amejifunza mengi ukizingatia yeye ni Mlokole πŸ˜ƒπŸŒΉ
Mlokole itakuwa ina maana nyingine siku hizi ama ni mimi ndiye nazeeka kwa speed ya mwanga!!

Zaburi 1: 1 - 6.
 
Kama mkuu wa mhimili asingepaswa kushangaa anatakiwa achukue hatua ya kuruhusu bunge litoe muongozo nini kinakwamisha maendeleo hayo kwenye mfumo wa haki jinai.

Tena kama mbobezi wa sheria inasikitisha zaidi.
 
Pale Mafwele atakapokutana na mzee Kibao mbinguni
Mbinguni hakuna kilichokinyonge kitakachoingia!Tutamalizana hapa hapa na Muumba siku ya kiama :Hapo ndipo watakapomwona mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na Utukufu.Ndipo atakapowatuma Malaika na kuwakusanya wateule wake Toka Pepo nne,Toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa wa mwisho wa mbingu''(Marko13:26,27) .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…