Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu , amesema si sahihi kulinganisha Bunge la sasa na Mabunge yaliyopita kwa kuzingatia ukubwa wa mijadala pekee.
Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari leo Jumatano katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya Miaka 100 ya Chimbuko la Bunge la Tanzania na masuala mbalimbali yanayolihusu Bunge, Spika Zungu amesema Bunge la mwaka 2015 lilikuwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani, hali iliyochangia mijadala mikali iliyovutia wananchi wengi kufuatilia shughuli za Bunge.
Hata hivyo, ameeleza kuwa hali ya sasa imebadilika kutokana na mwelekeo wa kisiasa na namna wananchi wanavyofanya maamuzi yao wakati wa uchaguzi.
“Viongozi wa vyama vya siasa waliopo sasa ni wazuri, lakini bado sijaona hamasa kubwa kwa wananchi ya kuwachagua kwa wingi kuingia Bungeni katika kipindi hiki,” amesema.