Spika Zungu: Wananchi hawajawa na hamasa ya kuchagua Upinzani kipindi hiki

Mzee wa kiingereza tuje kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 kwa akili yako uliona kitu kizuri? Hautaki tumlaumu magufuli kisa eti Kuna mazuri aliyafanya halafu unasahau hata wakoloni tunaowalaumu Kuna mema mengi waliyafanya
 
Walifungwa kwa ushahidi, kulikuwa na ‘actus reus’ and ‘mens rea’ kwenye kesi zote. Mengine ilikuwa makelele yenu watu waliokutwa ushahidi wa madumu ya kuchoma moto vituo vya mafuta na text message kutoka Kwa viongozi wa CDM mkawa mnapindisha ukweli.

Leo hii jamaa wanawaua hovyo na kirahisi tu illogically.
 
Kuanzia 2019 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa alituonyesha unaweza kupora uchaguzi na watu wasifanye lolote...
Bila ya kufahamu akili kama hizi ndio zinazo encourage; uhuni wa genge la wahuni linalo mzunguka Samia.

Kwa sasa wapore tu hizo chaguzi, lakini hii tabia ya kuchukulia uhai wa binadamu wengine poa hapana.

Sasa dereva wa Heche kwanini apoteze uhai wake, kama unaweza pora uchaguzi. Uoni kama kuna watu wanapenda kuuwa tu.
 
Kama yapi mazuri ya magufuli?
Huo sio msingi wa hoja yangu kwa sababu uhalisi kiongozi yeyote yapo mambo ambayo atapatia na kukosea, na watu hutofautiana mitazamo kuhusu viongozi kuna watu wanaweza kukwambia Kikwete ndio alikuwa kiongozi wa hovyo wakati wake ila wengine wakawa na mtazamo tofauti na ndio maana nasema mwisho wa siku ni kwamba kila kiongozi atakuwa na mazuri na mabaya.

Kuna mambo yanahitaji kuwekewa misingi na si kutegemea aina ya kiongozi, haya mambo ya sijui fulani alifanya hivi ila fulani ndio alifanya vile ni upuuzi mtupu.
 
 
Kwa kifupi, kwa ujumla, Magufuli alikuwa kiongozi bora au mbovu? Tofauti yake ya kimsingi na huyu wa awamu ya sita ni ipi hasa?
 
We mwarabu koko waheshimu wabunge wa upinzani, hawakujiweka bungeni, walichaguliwa na walishindana na wanaccm waliokataliwa.
 
Kuwe na tume huru ya uchaguzi hapo ndio majibu yatapatikana toka kwa wananchi
 
Kivipi Magufuli alianza kuhujumu wapinzani?
Magufuli ndio alikuwa anawaagiza wasimamizi wa uchaguzi kuwatangaza ccm hata kama box la kura limewakataa. Na sehemu nyingi zoezi hilo aliagiza liendeshwe kwa ukatili mkubwa. Wakati huo huo wafuasi wa upinzani waliokataa kura zao kutoheshimiwa aliagiza wabambikiwe kesi.
 

..hapana ndugu yangu.

..mahakama ya rufaa ilitupilia mbali hukumu na ikatoa kauli za kuwa na mashaka na mwenendo wa mahakama kuu.

..mbowe na wenzake walirudishiwa fedha zote walizolipishwa kama faini walipohukumiwa.

..Jpm ndiye muanzilishi wa udhalimu wa waziwazi dhidi ya vyama vya upinzani. Ndiye aliyekwenda mbali na kusema Jecha apewe nishani kwa kufuta uchaguzi wa Znz.

..Ninaposema haya simaanishi kwamba namsafisha Ssh. Hata yeye ameendeleza na kufanya udhalimu mkubwa zaidi wakati alitakiwa kuliponya taifa.
 
Huyu jamaa anazeeka vibaya saja
 

..Sheria haielekezi kwamba mikutano au shughuli za kiasiasa ziwe wakati wa kampeni za uchaguzi peke yake.

..Kama Jpm aliona si busara kufanya siasa kipindi ambacho si cha kampeni za uchaguzi alitakiwa afanye katika chama chake na sio kulazimisha vyama vyote.
 
Afrika hatuamini kwenye strong institutions bali tunaamini kwenye strong personalities ndio maana unakuta watu wanaishia kuwa machawa wa mtu fulani na mtu huyo akiwa nje ya mfumo anaonekana kama 'nya yaani kinyesi, chawa wote wanamkwepa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…