SportPesa: Yanga walituzunguka, usiku wakatangaza mdhamini mpya

SportPesa: Yanga walituzunguka, usiku wakatangaza mdhamini mpya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Maelezo ya SportPesa

Sisi tunajua kuwa hatua ya makundi hatuwezi kukaa kwenye jezi za Yanga na tulijadiliana cha kufanya ikiwamo kuwapa LiveScore ambayo walisema inahusika na beting na imekataliwa na CAF, tukaomba ushahidi wa maandishi kwa kujua hii inaonyesha matokeo ya mechi na sio kubeti,” amesema Sabrina na kufafanua kuwa, wakati wakisubiri kujua cha kufanya wakaona wenzao usiku wakizindua jezi na kumtangaza mdhamini mpya.

Amesema, tayari wameanza kuchukua Hatua ya kuhifadhi haki yake kutoka kwa mamlaka, kwa kuzingatia wana mkataba na haki ya kuwa kifuani mwa jezi za Yanga kwa miaka ya soka ya 2022 -2025.

My Take
🤣🤣🤣🤣🤣 Yanga inachekesha
 
Kwa timu inayoongozwa na wavulana wanaotegemea mawazo ya wazee kuendesha mambo yao, hata siwashangai kwa huo usanii wa kitoto waliofanya, wao wanategemea ujinga wa mashabiki wao kuwatetea.

Uongozi wa Hersi utaacha alama isiyofutika ya ujinga utopolo, hii mikataba wanayoingia itawavua nguo kila siku, expect more to come.
 
tony92
Kobello
Njooni mbishane na mkataba huku
Huyo wakwanza nina mashaka naye

Nadhani ni mmoja ya washiriki waliochangia wazo la kuwazunguka SportPesa

Mwingine huyu changaule ye hoja yake kuu ni bonus, hana hoja nyingine.

Kwake yeye anaona bonus ya 100M ni kitu kikubwa sana kuliko 1B wanayoipata kwa mwaka mzima kutokana na mkataba waliosaini.
 
Kwa timu inayoongozwa na wavulana wanaotegemea mawazo ya wazee kuendesha mambo yao, hata siwashangai kwa huo usanii wa kitoto wanaofanya, wao wanategemea ujinga wa mashabiki wao kuwatetea.

Uongozi wa Hersi utaacha alama isiyofutika ya ujinga utopolo, hii mikataba wanayoingia itawavua nguo kila siku, expect more to come.

Rais wa timu anashinda kambini anapiga story na wachezaji wanamzoea wanamuona kama mwana tu.

Kina morrisson hawamuogopi ndio maana wakijisikia kwenda kwao wanaenda tu huku mechi za timu zinaendelea
 
Rais wa timu anashinda kambini anapiga story na wachezaji wanamzoea wanamuona kama mwana tu.

Kina morrisson hawamuogopi ndio maana wakijisikia kwenda kwao wanaenda tu huku mechi za timu zinaendelea
Hapo ndio naonaga maoni ya watu waliopendekeza jina la cheo cha Hersi libadilishwe waite hata Mwenyekiti

Jina la cheo chake na mambo yanayofanyika yanadhalilisha hadhi ya uraisi na kuona kama uraisi ni kitu fulani cha kijinga tu
 
Uharibifu umeshafanyika. Hata wakibandua wanaweza kutakiwa kulipa faini kali.

Mtaji wao kwenye sakata hili ni wanasiasa wao waitishie kuifanyia michezo michafu Sportpesa au mashabiki wao watishie kuiadhibu kibiashara. Maana ukifuatilia utaona lugha wanayotumia mashabiki ni ile ya kisasi au kutaka huruma na siyo kuangalia haki hasa iko wapi.
 
Tatizo ni umasikini wa vilabu vyetu,njaa mbaya sana.vilabu viajiri wanasheria na watu wa taaluma husika katika kila jambo,siyo kuajiri washabiki na wanazi katika mambo nyeti.
 
Yanga hana hasara kwa jezi za wachezaji,hasara kwa mzigo alokuwa awauzie mashabiki.Ye abandue kisha wakae wajadiliane, huku mtaani waziachie tu.
 
Maelezo ya SportPesa

Sisi tunajua kuwa hatua ya makundi hatuwezi kukaa kwenye jezi za Yanga na tulijadiliana cha kufanya ikiwamo kuwapa LiveScore ambayo walisema inahusika na beting na imekataliwa na CAF,...
Kwa fikra zako unahisi Yanga hakuna wanasheria na hawakujua hilo?

Think again ilo suala linakuja kutolewa ufafanuz very soon
 
Hizi timu ni janja janja, baba Mmoja mama mmoja wana ishi kwa babu yao kariakoo
 
Huyo wakwanza nina mashaka naye

Nadhani ni mmoja ya washiriki waliochangia wazo la kuwazunguka SportPesa

Mwingine huyu changaule ye hoja yake kuu ni bonus, hana hoja nyingine.

Kwake yeye anaona bonus ya 100M ni kitu kikubwa sana kuliko 1B wanayoipata kwa mwaka mzima kutokana na mkataba waliosaini.
We jamaa naona umehama kwenye mada umekuja kwenye personal attack.

Mambo ya bonus tumejadili kwenye Uzi mwingine umeamua kuleta Hadi huku na hakuna sehemu nimesema bonus ni bora kuliko mkataba yaani umetunga maneno Ili mradi uonekane uko sahihi.
 
Back
Top Bottom