Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru
Rais John Pombe Magufuli akihutubia leo Musoma amesema gesi asili ya Tanzania tayari mabepari wameshaigawana kwa mikataba yao kwa sababu tu walishiriki kuivumbua.
Akiongea hayo mjini Musoma leo amesema bomba la gesi ya Mtwara lililojengwa mpaka Dar es Salaam linatumika kwa 30%, huku asilimia nyingine zilizo baki zikienda kwa mabepari.
Amesema pia kuwa aliamua kupambana yeye kama yeye kupata fedha kwa ajili ya kujenga Stigler's Gauge ambao ni mradi wa umeme mwingi ili kukwepa matumizi ya gesi asilia kutoka Mtwara kwa kuwa tayari gesi wakubwa wamegawana tayari.
Pia ameongeza kuwa Uranium iliyoko Mkoa wa Ruvuma haiwezi kutumika kwa manufaa ya Taifa kwa kuwa tayari nayo wakubwa washaigawana kwa kuwa tu waliivumbua wao katika tafiti, na hata kama akisema serikali itumie fedha kuinunua bado wataigomea.
Kauli hii ya Rais Magufuli imethibitisha kauli ya Dr Wilbrod Slaa aliyoitoa mjini Iringa mwaka 2014 kuwa " Tunaambiwa mabomba ya gesi ya Mtwara yanaelekea Dar, kumbe yameelekezwa Ulaya, wanachukukua gesi yetu."
Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru - JamiiForums