Mnamo mwaka 1987 Nchini uingereza kuliibuka tetesi kwamba Idara ya ujajusi wa ndani MI15 kupitia kwa maafisa wake walihusika katika mpango wa kumdhoofisha aliekuwa waziri mkuu "
Harold Wilson", na kumlazimisha Kuondoka Madarakani kwa
kujiuzulu.
Jina la
Spy Catcher Linasomeka moja ya vitabu katika Maktaba ya mzee
Joseph Sinde Warioba wakati alipotembelewa na
Dkt; Nchimbi tarehe 04 July 2026 na ni kabla ya kutoa taarifa ya kutaka kujiuzulu, tarehe 25 Agosti 2026.
View attachment 3669182
Nakala Original
View attachment 3669183
View attachment 3669184
Embu tuachane na picha hizo na tuegemee kwenye Kitabu chenyewe,
Kinausu nini haswa..? Na kwa mtazamo wa kilichotokea
Je kuna ujumbe ulitolewa kabla ya jambo husika kutokea...?
Kitabu cha
Spy Catcher kiliandikwa na Afisa muandamizi wa idara ya MI15 "
Peter Wright ", Afisa Muhimu katika ujasusi wa MI15 kwa wakati huo, aliandika kitabu hiki kwa kuamua kutema Bungo baada ya madudu, mabaya na mipango ya siri iliyopita miiko ya Usalama wa taifa aliyoiona, Kwaajili ya maslahi mapana ya taifa na usalama wa watu wake, pia ni kutokana na unyama na kutwezwa kwa utu wa kibinadamu ndipo akaamua kujitenga na kumwaga mboga yote.
Serikali ya Uingereza ya wakati huo, ilipambana kuhakikisha kitabu akifiki kwa walaji kwa kupiga
banning za nguvu, Yaani kufungia vyombo vya habari vilivyotaja jina
Spy Catcher, kuwafunga wapinzani waliotumia yale yaliyondani ya kitabu kukosoa serikali na pia walifunga movie production company zilizotumia sehemu ya kitabu hicho kuunda Movie za kipelelezi.
Lakini kama unavyojua kadri unavyowaambia watu Pombe haifai basi ndio wanaongeza kuinywa ili wajioone madhara yake wenyewe.
Nguvu zote zilizotumika kudhibiti ziliangukia Sifuri na baadae kitabu kikapenya kwa kasi kubwa sana ndani na njee ya Uingereza kiasi cha kuuza
millions of Copy kwa muda mfupi sana.
Hatimae baadae,
House of Lords iliondoa kizuizi kikubwa dhidi ya magazeti ya Uingereza mwaka 1988 na magazeti hayo yakaendelea kuchapisha habari kuhusiana na kitabu hicho.
Ruhusa hiyo haikutolewa hivi hivi bali ni kwa juhudi za wanasheria mbaka mahakama ikaruhusu kuachiwa huru kwa kazi za kiandishi maana si tu ilikuwa ni siri bali ilihusishwa na hakimiliki za Uandishi. (
Hama kweli Mahakama yenye kuheshimu sheria, na haki za watu haiwezi kufungwa na aibu za viongozi wa kisiasa walio Madarakani).
"
It's F****ng too late to catch the moving train",
Kitabu kinabeba siri kadhaa kama,
• Operation ya MI15 dhidi ya watu waliotuhumiwa kuwa ni majajusi ya Soviet..
• Tuhuma kwamba Robert Hollis aliyewai kuwa Mkuu wa MI15 kwamba alikuwa ni Mmoja wa Soviet, ....
• Tuhuma kuhusu namna Siasa ilivyoingizwa ndani ya vyombo vya Ujasusi mbaka kufikia kuwa ujasusi ni unafki na mwisho kuuwana wenyewe kwa wenyewe......
Kitabu kimeeleza mambo mengi sana kiasi siwezi kuyamaliza yote hapa lakini ninachoweza kusema nini tunaweza kukipata kutokana na picha hii.....?
Nawakaribisha majasusi wote wa JF, Wachambuzi wa maswala ya Demokrasia ya kisiasa, Waandishi wa habari na Raia yeyote atakaekuwa na mtazamo wa njee ya box kutoa maoni yake kuhusu hili. Mimi maoni yangu ni hayoapo chini.
Kwa maoni yangu Mimi nadhani hiki kitabu hakikuwepo kwa bahati mbaya, bali Nchimbi alienda kuchukuwa Ushauri kuhusu kujiudhuru kutokana na mashinikizo dhidi yake,.....
Kwa maoni yangu Dkt; Nchimbi alijaribu kuueleza umma kwamba Nalazimishwa kujiudhuru kama ilivyotokea kwa kile kilicho ndani ya kitabu hiki hapa,....
Kwa moani yangu na kile nilichotokea kwa gazeti la mwanahalisi kufungiwa baada ya kuandika "
Nchimbi agoma kujiudhuru", napata jibu la moja kwa moja kwamba Nchimbi hakuachia ngazi kwa ridhaa yake bali kwa shinikizo,.....
Kwa maoni yangu Kauliza Nchimbi kuhusu katiba mpya ndio sababu kuu ya Kuradhinishwa kujiuzulu,........ "
Pambaneni mpate katiba mpya",
vielezo Picha vilivyotumika ilikuwa ni 04 July 2026, yaani miezi miwili kabra ya Kujiuzulu, na pia vielezo picha vilivyotumika kwenye Thread hii vimepakuliwa kutokea
Hapa
PIA SOMA:
Pendekezo la katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania lenye muundo wa dola wenye mihimili minne ya kitaifa.
***********************
Uhuru wa Mahakama Haulindwi kwa Maneno, Bali kwa Muundo: Kwanini Kauli ya kikatiba kwamba "Mahakama ni huru", bila muundo bora ni Udhaifu mkubwa..?
************************
Je wajua Taifa bila mihimili minne huru na imara ni taifa Mfu..? "Huu ulikuwa ni uzi wa mzee
Pascal Mayalla nami nikaweka maoni yangu kuunga mkono hoja zake .
*************************