Mnanguliti
JF-Expert Member
- Apr 16, 2023
- 941
- 2,759
Mangula ni mwadilifu ila Warioba kawapita mbali sana hao wazee wenzie. Wengine hawawezi kusemaPhilip Mangula vipi?
Mangula ni mwadilifu ila Warioba kawapita mbali sana hao wazee wenzie. Wengine hawawezi kusemaPhilip Mangula vipi?
KabraMnamo mwaka 1987 Nchini uingereza kuliibuka tetesi kwamba Idara ya ujajusi wa ndani MI15 kupitia kwa maafisa wake walihusika katika mpango wa kumdhoofisha aliekuwa waziri mkuu "Harold Wilson", na kumlazimisha Kuondoka Madarakani kwa kujiuzulu.
Jina la Spy Catcher Linasomeka moja ya vitabu katika Maktaba ya mzee Joseph Sinde Warioba wakati alipotembelewa na Dkt; Nchimbi tarehe 04 July 2026 na ni kabla ya kutoa taarifa ya kutaka kujiuzulu, tarehe 25 Agosti 2026.
View attachment 3669182
Nakala Original
View attachment 3669183
View attachment 3669184
Embu tuachane na picha hizo na tuegemee kwenye Kitabu chenyewe, Kinausu nini haswa..? Na kwa mtazamo wa kilichotokea Je kuna ujumbe ulitolewa kabla ya jambo husika kutokea...?
Kitabu cha Spy Catcher kiliandikwa na Afisa muandamizi wa idara ya MI15 "Peter Wright ", Afisa Muhimu katika ujasusi wa MI15 kwa wakati huo, aliandika kitabu hiki kwa kuamua kutema Bungo baada ya madudu, mabaya na mipango ya siri iliyopita miiko ya Usalama wa taifa aliyoiona, Kwaajili ya maslahi mapana ya taifa na usalama wa watu wake, pia ni kutokana na unyama na kutwezwa kwa utu wa kibinadamu ndipo akaamua kujitenga na kumwaga mboga yote.
Serikali ya Uingereza ya wakati huo, ilipambana kuhakikisha kitabu akifiki kwa walaji kwa kupiga banning za nguvu, Yaani kufungia vyombo vya habari vilivyotaja jina Spy Catcher, kuwafunga wapinzani waliotumia yale yaliyondani ya kitabu kukosoa serikali na pia walifunga movie production company zilizotumia sehemu ya kitabu hicho kuunda Movie za kipelelezi.
Lakini kama unavyojua kadri unavyowaambia watu Pombe haifai basi ndio wanaongeza kuinywa ili wajioone madhara yake wenyewe.
Nguvu zote zilizotumika kudhibiti ziliangukia Sifuri na baadae kitabu kikapenya kwa kasi kubwa sana ndani na njee ya Uingereza kiasi cha kuuza millions of Copy kwa muda mfupi sana.
Hatimae baadae, House of Lords iliondoa kizuizi kikubwa dhidi ya magazeti ya Uingereza mwaka 1988 na magazeti hayo yakaendelea kuchapisha habari kuhusiana na kitabu hicho.
Ruhusa hiyo haikutolewa hivi hivi bali ni kwa juhudi za wanasheria mbaka mahakama ikaruhusu kuachiwa huru kwa kazi za kiandishi maana si tu ilikuwa ni siri bali ilihusishwa na hakimiliki za Uandishi. (Hama kweli Mahakama yenye kuheshimu sheria, na haki za watu haiwezi kufungwa na aibu za viongozi wa kisiasa walio Madarakani).
"It's F****ng too late to catch the moving train",
Kitabu kinabeba siri kadhaa kama,
• Operation ya MI15 dhidi ya watu waliotuhumiwa kuwa ni majajusi ya Soviet..
• Tuhuma kwamba Robert Hollis aliyewai kuwa Mkuu wa MI15 kwamba alikuwa ni Mmoja wa Soviet, ....
• Tuhuma kuhusu namna Siasa ilivyoingizwa ndani ya vyombo vya Ujasusi mbaka kufikia kuwa ujasusi ni unafki na mwisho kuuwana wenyewe kwa wenyewe......
Kitabu kimeeleza mambo mengi sana kiasi siwezi kuyamaliza yote hapa lakini ninachoweza kusema nini tunaweza kukipata kutokana na picha hii.....?
Nawakaribisha majasusi wote wa JF, Wachambuzi wa maswala ya Demokrasia ya kisiasa, Waandishi wa habari na Raia yeyote atakaekuwa na mtazamo wa njee ya box kutoa maoni yake kuhusu hili. Mimi maoni yangu ni hayoapo chini.
Kwa maoni yangu Mimi nadhani hiki kitabu hakikuwepo kwa bahati mbaya, bali Nchimbi alienda kuchukuwa Ushauri kuhusu kujiuzulu kutokana na mashinikizo dhidi yake,.....
Kwa maoni yangu Dkt; Nchimbi alijaribu kuueleza umma kwamba Nalazimishwa kujiuzulu kama ilivyotokea kwa kile kilicho ndani ya kitabu hiki hapa,....
Kwa moani yangu na kile nilichotokea kwa gazeti la mwanahalisi kufungiwa baada ya kuandika "Nchimbi agoma kujiuzulu", napata jibu la moja kwa moja kwamba Nchimbi hakuachia ngazi kwa ridhaa yake bali kwa shinikizo,.....
Kwa maoni yangu Kauli za Nchimbi kuhusu katiba mpya ndio sababu kuu ya Kuradhinishwa kujiuzulu,........ "Pambaneni mpate katiba mpya",
vielezo Picha vilivyotumika ilikuwa ni 04 July 2026, yaani miezi miwili kabra ya Kujiuzulu, na pia vielezo picha vilivyotumika kwenye Thread hii vimepakuliwa kutokea Kwenye Tovuti iliyo nyuma ya maandishi haya Hapa
PIA SOMA:
Pendekezo la katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania lenye muundo wa dola wenye mihimili minne ya kitaifa.
***********************
Uhuru wa Mahakama Haulindwi kwa Maneno, Bali kwa Muundo: Kwanini Kauli ya kikatiba kwamba "Mahakama ni huru", bila muundo bora ni Udhaifu mkubwa..?
************************
Je wajua Taifa bila mihimili minne huru na imara ni taifa Mfu..? "Huu ulikuwa ni uzi wa mzee Pascal Mayalla nami nikaweka maoni yangu kuunga mkono hoja zake .
*************************
Thanks, hiki sikubahatika kukisoma ila sasa nitakisoma.Nyuma yake kuna kitabu hiki
View attachment 3669773
Ndugu,unaweza kunipa nchi ambayo katiba yao ndiyo imewafanya wawe industrial society ili nami nipate elimu kidogo.Kuhusu industrial Society sio makosa yetu ni mfumo mbovu wa utawala wa nchi.
Binafsi naamini kabisa kama tukipata katiba kama hii iliyopo kwenye tovuti ya www.katibampya.com ambayo rasimu hiyo ni pendekezwa yenye muundo wa dola lenye mibimili minne ya kitaifa, Yaani.
1. Baraza la usimamizi wa taifa
2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania
Muundo huu unafunga mianya yote ya ufisadi, rushwa na uonevu na inaibua maendeleo endelevu, ukweli, uwajibikaji na usimamizi madhubiti wa misingi yote ya taifa letu.
Kama utakuwa tayari kusoma katiba hiyo basi Baraza la usimamizi wa taifa limetajwa kwenye ibara ya 98 mbaka 116 .
Singapore japokuwa si katiba pekee na sheria zake, pia ni bahati kwao kuwa na waziri mkuu mwenye uchungu na mabadiriko Lee kuan YewNdugu,unaweza kunipa nchi ambayo katiba yao ndiyo imewafanya wawe industrial society ili nami nipate elimu kidogo.
Umeshasema ni mawazo Yako basi vizuri; endelea kuyamiliki, kwa wivu mkubwa, mawazo Yako.Mnamo mwaka 1987 Nchini uingereza kuliibuka tetesi kwamba Idara ya ujajusi wa ndani MI15 kupitia kwa maafisa wake walihusika katika mpango wa kumdhoofisha aliekuwa waziri mkuu "Harold Wilson", na kumlazimisha Kuondoka Madarakani kwa kujiuzulu.
Jina la Spy Catcher Linasomeka moja ya vitabu katika Maktaba ya mzee Joseph Sinde Warioba wakati alipotembelewa na Dkt; Nchimbi tarehe 04 July 2026 na ni kabla ya kutoa taarifa ya kutaka kujiuzulu, tarehe 25 Agosti 2026.
View attachment 3669182
Nakala Original
View attachment 3669183
View attachment 3669184
Embu tuachane na picha hizo na tuegemee kwenye Kitabu chenyewe, Kinausu nini haswa..? Na kwa mtazamo wa kilichotokea Je kuna ujumbe ulitolewa kabla ya jambo husika kutokea...?
Kitabu cha Spy Catcher kiliandikwa na Afisa muandamizi wa idara ya MI15 "Peter Wright ", Afisa Muhimu katika ujasusi wa MI15 kwa wakati huo, aliandika kitabu hiki kwa kuamua kutema Bungo baada ya madudu, mabaya na mipango ya siri iliyopita miiko ya Usalama wa taifa aliyoiona, Kwaajili ya maslahi mapana ya taifa na usalama wa watu wake, pia ni kutokana na unyama na kutwezwa kwa utu wa kibinadamu ndipo akaamua kujitenga na kumwaga mboga yote.
Serikali ya Uingereza ya wakati huo, ilipambana kuhakikisha kitabu akifiki kwa walaji kwa kupiga banning za nguvu, Yaani kufungia vyombo vya habari vilivyotaja jina Spy Catcher, kuwafunga wapinzani waliotumia yale yaliyondani ya kitabu kukosoa serikali na pia walifunga movie production company zilizotumia sehemu ya kitabu hicho kuunda Movie za kipelelezi.
Lakini kama unavyojua kadri unavyowaambia watu Pombe haifai basi ndio wanaongeza kuinywa ili wajioone madhara yake wenyewe.
Nguvu zote zilizotumika kudhibiti ziliangukia Sifuri na baadae kitabu kikapenya kwa kasi kubwa sana ndani na njee ya Uingereza kiasi cha kuuza millions of Copy kwa muda mfupi sana.
Hatimae baadae, House of Lords iliondoa kizuizi kikubwa dhidi ya magazeti ya Uingereza mwaka 1988 na magazeti hayo yakaendelea kuchapisha habari kuhusiana na kitabu hicho.
Ruhusa hiyo haikutolewa hivi hivi bali ni kwa juhudi za wanasheria mbaka mahakama ikaruhusu kuachiwa huru kwa kazi za kiandishi maana si tu ilikuwa ni siri bali ilihusishwa na hakimiliki za Uandishi. (Hama kweli Mahakama yenye kuheshimu sheria, na haki za watu haiwezi kufungwa na aibu za viongozi wa kisiasa walio Madarakani).
"It's F****ng too late to catch the moving train",
Kitabu kinabeba siri kadhaa kama,
• Operation ya MI15 dhidi ya watu waliotuhumiwa kuwa ni majajusi ya Soviet..
• Tuhuma kwamba Robert Hollis aliyewai kuwa Mkuu wa MI15 kwamba alikuwa ni Mmoja wa Soviet, ....
• Tuhuma kuhusu namna Siasa ilivyoingizwa ndani ya vyombo vya Ujasusi mbaka kufikia kuwa ujasusi ni unafki na mwisho kuuwana wenyewe kwa wenyewe......
Kitabu kimeeleza mambo mengi sana kiasi siwezi kuyamaliza yote hapa lakini ninachoweza kusema nini tunaweza kukipata kutokana na picha hii.....?
Nawakaribisha majasusi wote wa JF, Wachambuzi wa maswala ya Demokrasia ya kisiasa, Waandishi wa habari na Raia yeyote atakaekuwa na mtazamo wa njee ya box kutoa maoni yake kuhusu hili. Mimi maoni yangu ni hayoapo chini.
Kwa maoni yangu Mimi nadhani hiki kitabu hakikuwepo kwa bahati mbaya, bali Nchimbi alienda kuchukuwa Ushauri kuhusu kujiuzulu kutokana na mashinikizo dhidi yake,.....
Kwa maoni yangu Dkt; Nchimbi alijaribu kuueleza umma kwamba Nalazimishwa kujiuzulu kama ilivyotokea kwa kile kilicho ndani ya kitabu hiki hapa,....
Kwa moani yangu na kile nilichotokea kwa gazeti la mwanahalisi kufungiwa baada ya kuandika "Nchimbi agoma kujiuzulu", napata jibu la moja kwa moja kwamba Nchimbi hakuachia ngazi kwa ridhaa yake bali kwa shinikizo,.....
Kwa maoni yangu Kauli za Nchimbi kuhusu katiba mpya ndio sababu kuu ya Kuradhinishwa kujiuzulu,........ "Pambaneni mpate katiba mpya",
vielezo Picha vilivyotumika ilikuwa ni 04 July 2026, yaani miezi miwili kabra ya Kujiuzulu, na pia vielezo picha vilivyotumika kwenye Thread hii vimepakuliwa kutokea Kwenye Tovuti iliyo nyuma ya maandishi haya Hapa
PIA SOMA:
Pendekezo la katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania lenye muundo wa dola wenye mihimili minne ya kitaifa.
***********************
Uhuru wa Mahakama Haulindwi kwa Maneno, Bali kwa Muundo: Kwanini Kauli ya kikatiba kwamba "Mahakama ni huru", bila muundo bora ni Udhaifu mkubwa..?
************************
Je wajua Taifa bila mihimili minne huru na imara ni taifa Mfu..? "Huu ulikuwa ni uzi wa mzee Pascal Mayalla nami nikaweka maoni yangu kuunga mkono hoja zake .
*************************
Pongezi kwake, vipi Mzee anaendeleaje?Mangula ni mwadilifu ila Warioba kawapita mbali sana hao wazee wenzie. Wengine hawawezi kusema
🔥🔥🔥🔥🔥SPY CATCHER, POWER OF WOMAN & THE ICARUS AGENDA: Je, Huu ni Ujumbe Uliotangulia Tukio.?
UPDATE YA UZI HUU BAADA YA KUCHIMBA ZAIDI
Nilipoanzisha uzi huu nilianza na kitabu kimoja tu nilichokiona kwenye picha ya Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Mzee Joseph Sinde Warioba tarehe 04 July 2026.
Kitabu hicho kilikuwa ni SPY CATCHER cha Peter Wright
Swali langu lilikuwa rahisi lakini lenye uzito:
Je, kitabu hiki kilikuwa tu sehemu ya maktaba ya Mzee Warioba, au kulikuwa na ujumbe ambao ulipaswa kusomwa na mtu mwenye uwezo wa kuunganisha dots?
Lakini baada ya kuangalia picha kwa umakini zaidi, wadau wakaibua vitabu vingine viwili vilivyokuwa kwenye eneo hilo:
1. Spy Catcher
2. The Power of Woman
3. The Icarus Agenda
Hapo ndipo jambo likaanza kubadilika Kwa sababu sasa hatuongelei tena kitabu kimoja Bali tumebaini Mzizi wa Bamboo Tree.
Tunaongelea vitabu vitatu, vyenye themes tatu tofauti lakini zinazoweza kukutana kwenye eneo moja: MADARAKA.
Na kabla mtu hajaniambia nimeamua kwamba vitabu hivyo viliwekwa kwa makusudi, ngoja niseme wazi kwamba:
"Ninachofanya hapa ni kuweka mezani kile nilichokiona, kile kilichotokea baadaye, kisha kuacha kila mwenye akili yake ajaribu kuunganisha dots".
1. TUANZE na SPY CATCHER
Spycatcher iliandikwa na Peter Wright, aliyekuwa afisa wa MI5, na ni kumbukumbu ya yale aliyoyaona na kuyafahamu akiwa ndani ya mfumo wa ujasusi wa Uingereza.
Lakini kinachonifanya kitabu hiki kiwe interesting kwenye picha ya Nchimbi na Warioba si neno SPY Bali ni kile ambacho kitabu kinachohusisha.
Ndani ya kitabu hichi kuna mada kama:
- counterintelligence
- spies ndani ya taasisi
- suspicion
- internal investigations
- Tuhuma za double agents
- secrecy
- power structures
- conflict ndani ya security establishment na namna ukweli wa ndani wa taasisi unavyoweza kuwa tofauti na picha yake ya nje.
- operesheni za ujasusi,
- migongano ndani ya taasisi,
- kuingiliwa kwa siasa katika mfumo wa usalama,
- na madai ya mambo yaliyokuwa yakifanyika nyuma ya pazia ambayo hayakuonekana kwa umma.
Kwa hiyo kama mtu angeamua kutumia kitabu hiki kama alama au symbolism, ujumbe wake usingekuwa lazima uwe, “Mimi ni jasusi.” La Unaweza pia kuusoma kama, “Usiangalie kinachoonekana mbele tu kuna mambo yanaweza kuwa yanaendelea ndani ya mfumo ambayo umma hauyaoni wala kuyajua.”
Na hapa ndipo mambo yanaanza kuwa mazito Kwa sababu picha hiyo haikupigwa baada ya Nchimbi kujiuzulu, Ilichukuliwa 04 July 2026.
Karibu wiki saba kabla ya taarifa yake ya kujiuzulu ya 25 August 2026.
Kwa hiyo kama tunataka kuiangalia kama clue, basi ni clue iliyotokea kabla ya tukio. Na hilo ndilo linalofanya swali liwe interesting zaidi.
2. THE POWER OF WOMAN
Hiki ni kitabu cha Pamela R. Durso, kinachohusu maisha na maandishi ya Sarah Moore Grimké.
Sarah Grimké hakujulikana kwa kukaa kimya mbele ya mamlaka yeye dhuruma, na kitabu chake hichi kilikuwa kinahusu mamlaka ya mwanamke, usawa, upinzani dhidi ya mamlaka kandamizi, haki za kisiasa na mabadiliko ya kijamii
Sarah Grimké alikuwa mpiganiaji wa mageuzi ya kijamii, haki za watu waliokuwa watumwa, na baadaye akawa mtetezi mkubwa wa usawa wa wanawake katika elimu, kazi, siasa na maisha ya kijamii.
Kwa hiyo neno POWER kwenye kitabu hiki si mapambo bali ni mjadala wa mwanamke, mamlaka, usawa, haki, siasa na mabadiliko ya mfumo.
Sasa jiulize:
Kwa nini kitabu kinachozungumzia Power of Woman kiko kwenye frame ile ile?
Sitaki kusema kinamaanisha mtu fulani Lakini hebu tukubali kwa muda kwamba mtu alikuwa anatafuta symbolism.
Hapo ndipo kitabu hichi kinanivuta mbaka kwenye ukweli kwamba Tanzania hiko chini ya uongozi wa mwanamke mwenye mamlaka ya juu kabisa katika nchi na hapo ndipo swali linaibuka Je, Uwepo wa kitabu hicho kwenye picha hizi ni coincidence?
Je, linaweza kuwa ni symbolism?
Nakuachia wewe na Uchambuzi Wako Kuhusu Hilo.
3. THE ICARUS AGENDA
Hapa ndipo mimi binafsi nilianza kujiuliza maswali mazito zaidi.
Kwa sababu The Icarus Agenda si story tu ya kawaida ya action japokuwa ni kitabu cha riwaya lakini chenyewe Kinazunguka kwenye siasa, madaraka, viongozi na watu wenye nguvu wanaofanya mambo nyuma ya pazia.
Katika hadithi hiyo kuna kundi la watu wenye nguvu wanaojaribu kuathiri kwa siri nani atafika kwenye nafasi ya juu ya uongozi na mwelekeo ambao uongozi huo utachukuliwa.
Kwa lugha rahisi ni Sawa na kusema "Mamlaka nyuma ya Mamlaka, Serikali Nyuma ya Serikali, Kiongozi nyuma ya Kiongozi", nikimaliza Kwa kukazia Kwa wino Mzito hapa Naweza kusema ni kama vile ambavyo H.Polepole aliposema Kuhusu "Mondopalale state, Futungo Kule Angola, na Wahuni hapa Tanzania". (Mtoto mdogo uwezi Elewa Remote control yenye button Moja "Kuzima na Kuwasha")
Naomba nimwage Vitabu vyote vitatu mezani kisha Tu-connect the dots
1. Spy catcher ni kitabu kinachohusu Siri, Ujasusi, Migongano ya Ndani ya Mfumo, Etc
2. Power of woman ni kitabu kinachohusu Mamlaka ya Mwanamke, Madaraka, Usawa, Mageuzi ya Kijamii na Kisiasa Etc
3. The Icarus Agenda ni kitabu kinachohusu Siasa, Madaraka, Watu wenye Nguvu, Mamlaka iliyo nyuma ya Panzia Etc
Let's Connect the Dots Hivi kweli tunapaswa kuangalia hivi kama vitabu vitatu vilivyokaa tu kwenye shelf au kuna ujumbe Mzito ulitolewa?
Tarehe 4 July 2026 Dkt. Emanuel Nchimbi alimtembela Mzee Joseph Sinde Warioba na kupiga picha Iliyokuwa na Vitabu hivyo vitatu, Hakuna Mwenye ukweli wa kina nini kiliongereka katika kukutana kwao.
Tarehe 23 July 2026, Dkt. Emmanuel Nchimbi alitoa kauli iliyozua mjadala mkubwa kuhusu Katiba Mpya. Kwa upande mmoja akasema Serikali inataka Katiba Mpya, Rais anataka Katiba Mpya, CCM inataka Katiba Mpya. Lakini akamalizia kwa kuwaambia wananchi:
“PAMBANENI MPATE KATIBA MPYA.”
Hapo ndipo maswali mengi yakaibuka.
Tupambane na nani?
• Ikiwa Serikali inataka.
• Ikiwa Rais anataka.
• Ikiwa chama tawala kinataka.
• Ikiwa Katiba Mpya ipo kwenye ajenda.
• Ikiwa wananchi wanaidai.
Ni nani anaye izuia isipatikane?
Na kama kuna anayezuia, Je ni Nani huyo mkubwa zaidi ya Rais anaeiitaji?
Maswali ni mengi Sana na Kiukweli si Mimi nimeuliza Bali yaliulizwa na wengi Sana lakini hayakuoata Majibu mbaka Hivi sasa.
Kauli hiyo ilianza kuchambuliwa hadharani na wadau wa kisiasa na demokrasia. Abdul Nondo, kwa mfano, alihoji wazi contradiction iliyopo kati ya kusema Serikali/Rais/CCM wanataka Katiba Mpya na wakati huo huo kuwaambia wananchi “pambaneni” kuipata.
Na hapa ndipo mimi ninapoona kuna swali ambalo halipaswi kukimbiliwa kulijibu:
Je, Nchimbi alikuwa akizungumza kama sehemu ya mfumo aliokuwa akiuwakilisha, au alikuwa akisema kitu ambacho kilionyesha kwamba hata yeye alikuwa anaona kuna tofauti kati ya kile kinachosemwa na kile kinachoweza kufanyika ndani ya mfumo?
Tarehe 6 - 12 August 2026 Gazeti la MwanaHALISI lilichapisha taarifa yenye kichwa:
“NCHIMBI AGOMA KUJIUZULU.”
Taarifa hiyo ilidai kwamba Nchimbi alikuwa akikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu lakini alikuwa akikataa.
Baadaye, tarehe 19 August 2026, MAELEZO ilitangaza kusitisha leseni ya MwanaHALISI kwa miezi sita, ikisema miongoni mwa sababu ni habari hiyo na madai kwamba gazeti halikuzingatia usahihi, mizania na uthibitishaji wa taarifa.
Hapa sas sitaki kusema kwamba “MwanaHALISI ilikuwa sahihi.” au la, Lakini pia sitaki kulifunga jambo kwa kusema “Kwa sababu walifungiwa, basi walikuwa wanadanganya.”
Swali la msingi ni Gazeti lilipata wapi taarifa kwamba Nchimbi alikuwa akikataa kujiuzulu, wakati huo huo akiwa bado madarakani?
Na kama taarifa hiyo ilikuwa ya uongo, ilitoka wapi?
Na kama ilikuwa ya kweli kwa kiwango fulani, kwa nini baadaye mambo yakabadilika?
Tarehe 25 August 2026 Nchimbi akatangaza kujiuzulu.
Tarehe 26 August 2026 CCM ilimfukuza Nchimbi Katika Chama na taarifa zilizofuata zikaanza kuweka wazi kwamba kulikuwa tayari na mchakato wa kinidhamu ndani ya CCM kabla ya resignation yake.
Kuna mambo mengi yaliyokea Baada ya hapo lakini Mimi Naishia hapa nakuachia wewe mwanajamvi uendelee kuunganisha dots mbaka upate Jibu lako lakini Mimi namalizia Kwa kusema kwa lugha ya picha ni kwamba.
SPY CATCHER
“Kuna mambo ndani ya mfumo ambayo hayako wazi kwa umma.”
POWER OF WOMAN
“Mamlaka ya mwanamke na nguvu ya kisiasa ya mwanamke si jambo dogo.”
THE ICARUS AGENDA
“Watu wenye nguvu wanaweza kuwa na uwezo wa kuathiri mwelekeo wa siasa nyuma ya pazia.”
Embu Jiulize Mwenyewe.
Kwanini Vitabu hivyo vilionekana kabra ya kujiuzulu Kwake, na Je kutokana na dots hizi Je Vitabu Hivi vilikuwa vina ujumbe uliotolewa kabra ya matukio kutokea....?
Ooh yeah, however clear patterns are obvious.Dot ni nyingi sana but ukijaribu kuzi-connect you got something deeper.
Ofisi ya makamu wa rais mstaafu? Unamaanisha ofisi ya nchimbi? Kwani Nchimbi yuko wapi? Kumbe makamu wa rais mstaafu ana ofisi? Iko wapi? Mbona makamu wa rais wastaafu wako wengi wanatumia wote ofisi moja?Umesahau Jambo zito
Ofis ya Makamu wa Rais mstaafu na waziri Mkuu Mstaafu haina picha ya anayejiita Rais wa sasa
State rejection code spy level 6
Britanicca
Basi nishaelewa kumbe unazungumzia ofisi ya WariobaUmesahau Jambo zito
Ofis ya Makamu wa Rais mstaafu na waziri Mkuu Mstaafu haina picha ya anayejiita Rais wa sasa
State rejection code spy level 6
Britanicca
Ndugu katiba ya Singapore aijafanya chochote kuifanya Singapore kua moja ya Asian Tiger .. kuna mambo muhimu zaidi ya ili ulilotaja. Singapore hamna wapingaji wa kila kitu bali kuna washauri na watekelezaji basiSingapore japokuwa si katiba pekee na sheria zake, pia ni bahati kwao kuwa na waziri mkuu mwenye uchungu na mabadiriko Lee kuan Yew
Hii ni hatari... Hivi vitabu vilipangwa kupeleka ujumbe....Chini tena kuna The Icarus Agenda nitakisoma na kuona je kina dots zozote kuhusu swala hili.
Hapa ngoja niulize kama wale watoto wa "afu2" walamba lips wanasemaga "Like serious"!?Umesahau Jambo zito
Ofis ya Makamu wa Rais mstaafu na waziri Mkuu Mstaafu haina picha ya anayejiita Rais wa sasa
State rejection code spy level 6
Britanicca