Sri Lanka waandamanaji wajipa raha ndani ya vyumba vya Ikulu

Sri Lanka waandamanaji wajipa raha ndani ya vyumba vya Ikulu

Waandamanaji nchini Sri Lanka wamefanikiwa kuingia Ikulu na kufika mpaka chumbani kwa Rais. Waandamanaji hao wamerusha picha kwenye mitandao zikiwaonyesha wakiwa wamelala kitandani kwa Rais huku wengine wakiwa sebuleni wakiangalia 'breaking news' ya maandamano yao.
View attachment 2286097
Matokeo ya nchi kufilisika
 
Endeleeni kujazana upepo tu kuwa ipo siku mtafanya hivyo kulala kwenye vitanda vya Ikulu.

Twendeni tukalime vijana wenzangu.
Hatutaki kwenda huko Acha tuwe machawa,huoni machawa wanavyotusua,wanakuwa mpaka wageeni walikwa shuguli za kitaifa

Ova
 
Hii nilikuwa sijaelewa bado. Yaani haya ni mapinduzi ya pili baada ya yale ya miezi miwili iliyopita? Ndio maana yule rafiki yangu monk wa Sri Lanka sijamuona siku nyingi.
 
Hatutaki kwenda huko Acha tuwe machawa,huoni machawa wanavyotusua,wanakuwa mpaka wageeni walikwa shuguli za kitaifa

Ova
Kuanzia mwezi wa kumi naanza rasmi kuwa kupe sio chawa tena.
 
Wakishaandamana watapata nini? Watakaa humo njaa itawauma watarudi home, it's a foolishness in a mass order
 
Kuna wanakijiji walivamia kituo cha polisi wakachoma moto polisi walichukua silaha zao wakakimbia kesho yake waliwachangisha hao hao hana kijijini wakakikarabati, ujinga tu
 
Bongo ni pasua kichwa mkivamia magogoni Rais yuko chamwinoo
 
Asingetoka mtu hai humo
Hata kufika wangefikaje wangekuwa maiti wote Langoni tu la ikulu
Mambo yakiwa magumu kiasi hicho, hata wanaoshika bunduki hugeuka, maana hawajui hatma yao, kwani anaewaamrisha amefilisika na hana uwezo wa kulipa hata mshahara,
Tuombe Mungu tusifike huko,
 
Back
Top Bottom