SSH, Kiongozi anayetenda mazuri asubuhi ikifika jioni anavuruga kazi yake mwenyewe

SSH, Kiongozi anayetenda mazuri asubuhi ikifika jioni anavuruga kazi yake mwenyewe

Kufikia muda wa kampeni hatutakuwa na wabunge, je rais atakuwepo au hapana?? Atakuwa ni mgombea at the same time ni rais wa nchi au hapana?
 
Samia akifa nitafanya sherehe ya kumkumbuka Mdude
 
Ile ya mwanzo ilikuwa ni script. Ya sasa ndio uhalisia wake
 
Mama yetu alipoingia madarakani, alipiga kazi moja nzuri mno ya kupendeza katika miezi ya awali ya utawala wake, alikuwa ni mtu wa kuzungumzia haki, kukataa dhulma, kuunganisha Taifa, kiufupi alifanikiwa kuzikong'a nyoyo za jamii kwa kiasi kikubwa mno, na kuleta matumaini makubwa. Lakini leo sijui ni kitu gani kimejiri, mambo yamekuwa vice-versa, total confusion, hofu nchini, utekaji ambao haujawahi kufikia viwango hivi , sijui ni kitu gani kimemtokea mama yetu. It seems SSH wa April 2021 siyo SSH wa June 2025. SSH wa kipindi kile ni very empathetic, Sympathetic, huyu wa sasa anaoneka as if ni "Don't care"!. Sijui ni nani alimpa ushauri wa kujifanya bandidu wakati haiba yake na pengine asili yake siyo hiyo!- Ukiiga asili ambayo si yako lazima ukwame!.
Au sijui kipindi kile alikuwa hajakizoea kiti kwa hiyo utu wake ulikuwa mwingi, ila kwa sasa kakizoea kiti na hivyo power corrupts and absolute power corrupts absolutely?

Kiufupi mambo anayofanya SSH ni as if mtu anayefanya mambo mazuri asubuhi ikifika jioni anaharibu kazi yake mwenyewe, nitaeleza.

1. Alipoingia madarakani aliagiza kesi za watu waliobambikiziwa kesi zifutwe.
Hili lilikuwa jambo moja zuri sana, zuri mno, yaani hapa alilitendea Taifa haki kubwa sana. Ni katika kipindi hiki kesi za watu kama Mdude Nyagali zilifutwa, watu kibao waliokuwa wamewekwa ndani katika utawala uliopita kwa kesi za kubambika waliachiwa huru (Tuiite hiyo Asubuhi). Sasa Jioni ambayo ndiyo leo hii mambo yamegeuka si tu kwamba ubambikiziaji kesi upo, leo watu wanabambikiziwa zile kubwakubwa, Ugaidi, Uhaini n.k

2. Alipoingia madarakani alikemea uonevu wa jeshi la polisi na aliunda tume jinai kuchunguza maonevu wanayokumbana nayo wananchi katika vyombo vya dola (Tuiite hiyo Asubuhi). Jioni yake ambayo ni leo uonevu wa vyombo vya dola umezidi hata mara 10, watu wanatekwa mchana kweupe na usiku, maiti zinaokotwa, majaribio ya mauaji ya wazi hatusikii kauli ya SSH akijitokeza na kuagiza waziwazi kuwa anataka hayo mambo yakome na hata kuwawajibisha watu wemye dhamana kwa kushindwa kudhibiti hiyo hali nchini. Kiufupi image anayoportray ni kama vile I DON'T CARE.

MWISHO
Nimalizie kupitia mafunzo kutoka katika Qur'an tukufu.

Qur'an tukufu(16:92) inasema kuwa tusiwe kama yule mwanamke msusi ambaye asubuhi anasuka ukili wake vizuri, ikifika jioni anaanza kufumuafumua kazi yake mwenyewe, Mwenyezi Mungu akawataka waumini katika aya hiyo waheshimu VIAPO vyao wanavyokuwa wamekula.

Samia akiifanyia kazi aya hii hatoharibu kazi yake nzuri anayoifanya asubuhi pindi ikifika jioni, na ataheshimu pia kiapo alichokula cha kulinda, kuhifadhi na kutetea katiba ya Jamhuri ya muungano ambayo ndani yake inataka HAKI za Watu ikiwemo ya kuishi na FAIRNESS katika mambo ya nchi vinatamalaki katika Jamhuri.
Umeeleza vizuri lakini umechelewa kutoa hoja zako. Umekuwa kama Gwaji boy
 
Back
Top Bottom