St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Bado humjasaidia mtoa mada. Wamekuwa wakifanya vizuri kwa muda mrefu,Hakuna wa kushtuka kweli kama Kuna kitu kisicho cha kawaida!!!
 
Endelea kukataa ila ungewah kusoma private kwenye shule inayofanya vzr hata usingeshangaa

Mm nimesoma prvt inayofanya vzr na form four yetu tulikuwa wa 18 kitaifa huku tukiwa na division 2 moja pekee

But nikusaidie tu mchujo wa kuingia form one walikuja watoto zaid ya 3000 ila shule ikachagua 200 tu ambao walipitia mchujo mara tatu kisha wakawekwa darasan dec nzima then january walim waliokuwa wanawafundisha ile dec wakasort watoto 150 pekee wengine 50 wakasepa home

Hapo kidato cha pili na cha tatu mchujo ni mkubwa sana

Tulipokuwa tunaingia kidato cha tatu tukaambiwa kabisa form four haizid watu 40 na hapo tuko 90 ivyo kupambana kwako ndo kufaul kwako

Wastan wa kuingia kidato cha nne ilikuwq 65 ufaul wetu ukawa mkubwa wakapandisha mpk 78 ndo tukapita watu 40 pekee

Hapo usisahau tukiwa kidato cha tatu tulimaliza topic zote za kidato cha tatu na cha nne

So form four hatukusoma topic yoyote tulishacover huko nyuma

Kidato cha nne tulifanya mitohani kama huo wa taifa 16 kabla ya necta yenyewe(na haikuwa inatungwa wala kusahihishwa na walim wetu walikuwa wanaenda mikoa tofaut kukodi walim bora ndo wanafanya hilo)

Usisahau kuwa tangu tuneingia kidato cha nne kazi yetu ilikuwa kufanya marudio ya topic za nyuma zenye shida/kujisomea na kubwa kabisa kuna walim ambao mara nyingi wanachaguliwaga kwenda kusahihisha mitihan ya taifa(walikuwa wanakodiwa kuja kutufundisha mitihan ya taifa inasahihishwaje? Marking scheme zao zinakuwaje? Hii ilitujenga namna ya kujibu mitihan ya taifa tofaut na mitihan ya shule

Bro kubali shule bora zina vitu vingi zina offer kwa mwanafunzi bora(ukumbuke pale hawaendi vilaza)
 
A anapata yeyeto tu awe kata au senti inategemea na siku hio mwanafunzi aliamkaje.
Hizi shule type hizo wanafundishwa zaidi kujibu mitihani na sio kuelewa masomo thus wakija vyuoni uburuzwa vizuri tu na kuku wa kienyeji waliosoma kata.
 
Mkuu sio rahisi sana kila mwaka ununue mitihani na Mamlaka zikae kimya tu.

Lazima watachukua hatua.
Mkuu hao ni walimu wako kwenye mfumo mzima ....


Unajua mitihani ya necta form four inatugwa vip? Kama unajua mtihani unatugwa vip ndio utaweza kukubaliana na Mimi kuwa kuvujisha maswali yanayotoka kwenye mtihani wa necta ni simple Sana....


Kama mnadhani ni uongo ....

Naomba mkafuatilie pepar wanazofanya hawa watoto kabla ya necta ...hapa namaanisha "pre -necta examination na "ready for necta"....

Baada ya kupitia hizo Pepar njoo uangalie necta ,ndio utajua hujui ....

Kwenye physics ,biology na chemistry practical ndio usiseme [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]yaani hapa uanaambiwa live kabisa kuwa ,swali la volumetric analysisi volume of acid (Va=23.6 ) hakuna haja ya kuhangaika na pipete ,Wala measuring cylinder ...

Biology sample zote za viumbe wanaambiwa ,na ndio vinatoka ..

Physics kwenye equilibrium ,electric current ,sample zote wanaambiwa ...

Watoto wanatafuniwa kila kitu kuanzia ,bwenini kufanya usafi ,shule kufagia wanafanyiwa ,kutandika vitanda ,vyooni kudekiwa ,Hadi kufuliwa nguo ,walimu wanawatafunia material darasani ,Hadi mitihani ya necta wanatafuniwa .....hao watoto wanachojivunia ni uelewa wa mambo mbalimbali kutokana na tour ,na safari mbalimbali mbunga za wanyama n.k ....Ni mayai mayai tu

Lakin mtoto wa vidumu na maji ni more powerful and creative ,ni vile tu kiingereza ndio inakuwa tatizo ...


Msiwe wajinga Sana ,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Waliopo huko ulipopataja ni vipanga maskini. Mtu asome primary za mamilioni na aongoze halafu apelekwe shule za serikali akale maharage yaliyooza kweli? Ama vyakula vibovu vya wazabuni wasiolipwa kwa wakati
Na hao vipanga masikini ndiyo magenius halisi ambao wame strive kwa minimal resources halafu waka prosper.
 
Hili la Essay hata mimi mtoka shule za kajamba nani Magamba Boys na Tosamaganga Boys nilikuwa naandika hivyo kitambo
 
Hili la Essay hata mimi mtoka shule za kajamba nani Magamba Boys na Tosamaganga Boys nilikuwa naandika hivyo kikitambo
Ila huwafikii ST mwanangu hapo unatupanga😂😂😂😂😂😂
 
Tunakutana nao vyuoni, wala hawana maajabu, au watoke huko waende serikali wanakua weupee, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wanastahili kwa kweli
Your browser is not able to display this video.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tukisema hivi tunaambiwa wivu au roho mbaya, kumbe ni kweli kabisaa.
 
Ni vema ungewasilisha ushahid wa unayoyasema. Ikiwemo signed confession ili mwanga uwepo.
Zaidi ya hapo utaonekana tu mpiga porojo
 
Uko sahihi mkuu. Nakumbuka Ilboru form four ya 2001 walipiga hizo one kama vichaa wakati shule nyingi zilikuwa kupata one ni miujiza. Kimsingi watu wanatakiwa wazingatie tu kuwa kwenye elimu hakuhitajiki mizaha. Mtoto akiwa serious lazima apasue tu.
 
Nidhamu wanaisingiziaga sana
Haujui tu

Binti zangu wamesoma hapo, najuwa ninachokisema.

Wana nidhamu ya hali ya juu.

Hata kama una mtoto legelege, akifika pale utashangaa likizo ya kwanza akirudi kwako atakavyokuwa amebadilika.

Wanastahili
 
Majina ya kizungu tu ndiyo yametawala majina ya kiarabu lipo Moja tu makobazi mnakwama wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…